Treni za kizamani zina umuhimu sana bado kwenye uchumi

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,598
8,738
Nilienda likizo TZ kutoka hapa Dallas, Texas ninapoishi na kufanya kazi. Watu wengi walikuwa wananiambia tuna reli kama huko kwenu inakuja. Kitu ambacho hawajui Reli nyingi hapa sio za abiria ni za kiuchumi na zinabeba mizigo na mafuta kutoka sehemu mbalimbali kuja Texas kwa usafishaji wa mafuta. Lakini vilevile Teaxas kuna vitalu vingi vidogo vidogo vya mafuta ambavyo wanatumia reli kusafirisha.

Reli nyingi sio ambazo tunaziona mijini za umeme bali reli nyingi ni za kizamani na zinabeba mafuta, mazao, ngombe, magari na vifaa vya viwandani. Hivyo Serikali ya Tanzania isiache kutengeneza reli ambazo ni za bei rahisi kama zile za Tanga-Arusha kusaidia ubebeji wa mazao, chuma, makaa ya mawe na vitu vingine vingine mihimu kwa taifa.

Tusidanganywe sana na treni za umeme tukafikiria huku USA watu wana treni za umeme tu na kila kitu kitu ni kipya!. Hizi treni za zamani ziko kwa miaka mingi sana na ni muhimu sana kwa uchumi. Hapa USA kuna vijiji na wakulima wengi sana huku nje ya mji na hao ndiyo wanalisha na kufanya uchumi uendelee lakini Tanzania tunaonyeshwa treni za mijini na magorofa na kufikiri haya ndiyo maisha pekee ya huku.

Nimeandika hii message kwa kuhimiza serikali itengeneze reli za kimkakati ambazo zina gharama nafuu kwenye kwenye mashamba makubwa na sehemu za uchimbaji. Mfano kubeba chuma ni vizuri kutimia reli maana barabara zitakuwa zinaharibika kila siku au gharama za usafirishaji zitakuwa kubwa kwasababu ya uzito. Lakini ukanda wote wa kilimo unataka reli ili gharaza za ushafirishaji wa mazao ziwe ndogo. Lakini vilevile hizi treni zinaweza kuwekwa na kuwa na uwezo wa kufanya connection na treni za umeme.

Tumshukuru hayati Magufuli kwa kuonyesha mfano watu wengi hawajui kwamba ile reli za Tanga mpaka Arusha ni reli mpya sasa sijaona ugumu wa kuweka reli upande huu wa wakulima. Lakini kingine Serikali inatakiwa kuwa na sehemu za mkakati za ufugaji yaani serikali iweke sehemu kama ilivyo kwenye mbuga lakini iwe na wafugaji na iwe na section za kufugwa na kufunguliwa ili isije ikawa jangwa. Lakini serikali iwawekee mabwawa, visima vya maji na kuwe na urataibu wa kupanda majani na miti . Hii inawezekana badala ya sasa wafugaji hawana sehemu au hata wakipewa sehemu bila mikakati itaaribika
 
Umenena vyema, shida nchi yetu ni kila kitu siasa, wananchi wanavamia misitu halafu wanasiasa wanaanza kupigania msitu umegwe ili wananchi wapate pa kuchungia
 
Upo sahihi sana kuna kazi zinahitaji vitu vya kisasa kama treni za mjini ambazo ni za haraka na starehe.
Ila kuna vitu vya kazi kama hizo reli za zamani huko ulaya wanajua sana umuhimu wa hizo reli na wanazitunza sana.
 
Sawa nesi, hatimaye umefanikiwa kumwaga povu lako lingine la kijinga jinga. Haya, nenda kahudumie vizee vya kizungu wodini
 
Back
Top Bottom