TRENI ya SHIRIKA la RELI TAZARA itakayotumika kwa USAFIRI wa MWAKANGA-KURASINI majaribioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRENI ya SHIRIKA la RELI TAZARA itakayotumika kwa USAFIRI wa MWAKANGA-KURASINI majaribioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3]TRENI YA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA(TAZARA) ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO.[/h]


  [​IMG]

  Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jana mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.
  [​IMG]

  Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akiangalia eneo la Stesheni ya Mwakanga,wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yatakayofanya Safari zake Dar es Salaam-Mwakannga na Dar-Kurasini mnamo mwezi Oktoba 2012.Majaibio hayo yalifanyika jana kuanzia Dar-Mwakanga-Kurasini.
  [​IMG]
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam.
  [​IMG]
  Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akishuka kwenye Kichwa cha treni kitakachofanya Safari zake Dar-Mwakanga-Kurasini mapema mwezi wa kumi.Majaribio ya sehemu ya mabehewa hayo yalifanyika jana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Vizuri Sana... TRENI SAFI KWELI... TUzitunze Vizuri tuzipende hizo Treni zetu...
   
 3. commited

  commited JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  YAP, LICHA YA KWAMBA TUMECHELEWA SANA KATIKA HILI, NA KWA UZEMBE WETU HASA WATU WACHACHE KWA TAMAA ZAO WALIAMUA KULIUA SHIRIKA HILI, LAKINI SI MBAYA TUKAFUFUA TENA HIII RELI, NI UKOMBOZI MKUBWA SANA.. HAYA NDIYO MAONDELEO TUNAYOYATAKA.. KODI ZETU TUZIONE ZIKIFANYA KAZI, NA HAKI/SHERIA ZIONEKANE ZIKIFANYA KAZI, SIYO MWIZI NDIYE ANAYEPEWA UONGOZI, MWIZI KWAKE NI GEREZANI.. ASANTE SANA MKUU nngu007 ni kweli tuzitunze
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  haya ndo mambo tunayotaka.
  Big up sana.
   
 5. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na hatuishi kwa kuponda tu vitu vizuri tutavisifia hongereni wazalendo mliofanikisha hili
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Magufuli
   
 7. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hiyo hiyo reli itatumika kwa long distance i.e Tanzania&Zambia na shunting za bandari au siyo? Dah! Ndo Tz yetu hiyo
   
Loading...