Kwanza habari hizi zinafurahisha na kutia moyo sana kwani usafiri wa Dar-Moro utakuwa mzuri sana. Lakini angalizo kubwa kwa serikali yetu kuhusu mradi huu:
Tafadhali tusifanye mambo kwa kulipua kwa gharama ya walipa kodi. Naona kwamba tunajenga standard railway lakini tunachokosea kutokana na kutokujua kwetu ni kwamba tunajenga single railway lines, hili ni tatizo kubwa mno! Ni sawa na kujenga single lane roads kutoka Ubungo kwenda Posta.
Kama serikali inataka tufaidike na standard gauge railway lazima iwe na njia 2, ya kwenda na ya kurudi. Vinginevyo dhana nzima ya treni ya mwendokasi haitawezekana. Kwani itabidi treni hizo zisubiri katika vituo vya kupishana na hivyo zitachelewa kama kawaida. Tunapaswa kujenga standard railway gauge yenye njia 2 kila mahali Tanzania. Ndivyo ilivyo nchi zilizoendelea kama UK nk. La sivyo tutapoteza mamilioni ya fedha kwa kitu kisichofanya kazi.
Mambo kama haya yametokea katika mradi wa BRT kwani pamoja na mabilioni yote kuna makosa makubwa sana yamefanya kazi yote mpaka sasa kutoleta matokeo yanayotegemewa.