Treni ya mwakyembe Ubungo-stesheni ilikuwa zianze 10/9/12

Pilimi

Member
Mar 23, 2009
67
14
Kuna waziri wa uchukuzi mh Mwakyembe alisema train itaanza tarehe 10/9/12. Kwa walio karibu na hayo maeneo ya ubungo maziwa au buguruni,vipi train hiyo imeanza?
 
Ok,labda nilisikia vibaya inaweza kuwa labda alisema mwezi wa kumi.Ngoja tusubiri
 
Jana nilishuhudia Treni ikiwa na wafanyakazi wanatengeneza Reli mitaa ya Mabibo ndani nafikiri wako kwenye process za kurekebisha, Let give him more time
 
mimi pia nilisikia kuwa tarehe 10/09/2012. na leo kulikuwa foleni ubungo kubwa sana nikadhani kuwa ni kwasababu ya treni.
 
Nimepishana na treni hapa tabata imebeba abiria kweli jamaa kasimamia ahadi yake
 
jamaa anaasilimia kubwa ya kutekeleza ahadi yake, watu wa Relwe wapo bize sana kurekebisha njia hiyo ya train nawaona maeneo ya Tabata na mabibo wakichakarika na kubomoa nyumba zilizojengwa mita chache kutoka kwenye rail
 
Ikianza operation na ku sustain biashara. Kichaa ya kubeba abiria dar ndo nitarudi kutoa maoni yangu.
 
Hayawi hayawi huwa. Treni ya abiria katikati ya jiji la Dar es Salaam imeanza rasmi mazoezi ya daladala leo.
Treni hiyo ambayo ilitokea Stesheni na kwenda Ubungo kisha kurudi stesheni ilishangiliwa na mamia ya watu wafanyao biashara maeneo ya Buguruni Mnyamani.
Katika zoezi hilo, usalama kwa waenda kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara haukuzingatiwa, kwani kwenye makutano ya reli na barabara hakukuwa na kizuizi chochote kuzuia watu, magari, pikipiki nk
Pia treni ilipita kimyakimya bila kupiga honi kitu ambacho ni hatari kwa usalama.
Tunaomba mamlaka zinazohusika na usalama zihakikishe usalama kwanza kabla daladala treni hizo hazijaanza kazi rasmi.
Hata siku moja sijawahi kuona TUME IKIRUDISHA UHAI WA MAREHEMU
 
Back
Top Bottom