Treni ya Mwakyembe inapata hasara ya milioni 10 kwa siku 5

Treni za abiria ni mara chache sana zikaendeshwa kwa faida...mara nyingi mizigo ndio inalipia gharama za kuendesha mashirika ya reli.
 
Mnyika Ana madaladala yake kama 15 hivi ya ubungo kariakoo sasa yanamchanganya na hii train ya mwakyembe. Na hivi ana mtoto kazaa nje na mwanafunzi basi ndio balaa
 
wewe lazima uwe ccm, kwanini usiulize upate mchanganuo.. Haya mfano akitoa mchanganuo na kweli ukaonekana kuna hasara utasema nini??? Hata kama wazo halikuwa lake kweli hakuwa na uwezo wa kucheleweshwa kuanzisha hiyo train at least hadi miundombuni ikae sawa???? Au mwakyembe alikuwa anajijenga kisiasa??? Hebu tufikirie vyema mstakabali wa hivi vitu tunavyo vifanya na isije ikawa kama wale walokuwa wanamuomba mg. Raisi aidhinishe kituo cha muda cha tsh. 2 bil.... Akawagomea hata kingekuwa cha mil 2.... Tuache ushabiki tujiulize why kasema hivyo alivyosema coz naye sio mjinga...
wakati mwingine dogo huwa anachemka ....kitu kina mwezi mmoja tu !hakuna sababu ya kulaumu tunatakiwa tushuri .....mimi naona mwakyembe anastahili pongezi tunapoona mapungufu tuyaseme
 
Kwani nani alimwambia Mnyika serikali unafanya biashara?! Serikali kazi yake ni kutoa huduma kwa wananchi wake, ndio maana katika baadhi ya maeneo serikali hutoa ruzuku ili kuhakikisha wananchi anapata huduma kwa affordable price
 
Jama mi sioni faida za malamiko yanayozidi kutolewa na baadhi ya watu,hakuna faida cha muhimu ni kutoa mawazo nini kifanyike ili kuboresha na sio kumsema mh.Mnyika kwan naye ni binadamu some times hua anakosea kama wengine wanavyo kosea.
chakufanya ni kuongeza kukusanya kodi ili serikali iwe na pato kubwa iweze kutengeneza miundombinu bora.zaidi ya hapo cha kufanya ni kuiongezea ccm miaka 5
 
hapa mnyika katoa mwanga. kama wakazi wa dar es salaam nmataka muendelee kufaidi usafiri wa treni basi mwakyembe hana budi kufanyia kazi mapungufu yaliyopo. vinginevyo itabaki stori.
Hivi mtu akikwambia hiyo barabara nzuri unayo tembelea mwishoni imefungwa, utakasirika kwakua umetokea kwenye barabara mbaya?.
ni hayo tu. mia

ilikukava hiyo pungufu waongeze bei.
 
Mnyika katoa hoja nzuri,tukubali kila kitu ili kiendelee lazima mapungufu yawepo na hilo Mnyika katupa njia.Hatuna budi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopo ili kuboresha usafiri wa treni,tuache porojo na propaganda zisizojenga wanandugu tufanye kazi chanya kwa hoja zetu.
 
Namkubali sana Mnyika ila kwa hili nahisi kapotoka kidogo kwa sababu huduma kwa umma zinakuwa na ruzuku. Kwa hiyo hapo ukianza kutafuta hasara na faida kwenye huduma za umma utachanganyikiwa. Na iwapo serikali itaamua ipate faida kwa kila huduma ya umma kodi tunazolipa zitakuwa zinafanya kazi gani. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, Mwakyembe hongera (japo umetimiza wajibu wako wa kazi) kwa hili la treni wewe umefanya kweli wengine kama wakina Nundu na mawaziri waliotangulia walikuwa wanapiga bla bla tu zaidi ya miaka kumi iliyopita.Ila hiyo treni inabidi waongeze mabehewa kwa sababu yaliyopo 8 sasa hivi yanazidiwa abiria hayatoshi angalau yafike 12 na wakatisha tiketi ndani ya mabehewa hawapo makini pesa zinapotea kwa uzembe wao. Tunasubiri boti ya abiria bagamoyo via Tegete/kunduchi to Posta.
 
Back
Top Bottom