Treni ya Mwakyembe inapata hasara ya milioni 10 kwa siku 5

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,644
2,000
Kuongea sio kazi saana. Tunaomba mchanganuo hasara hiyo inasababishwa na nini na inatokeaje. Msituletee mambo ya kijinga kila sehemu. Msifikiri tunafurahi shida tunazipata sisi wao wanakula per day tu, na huku watu wengine wanawabwetere kila siku.

Good point.
Mnyika hawezi kuona adha za usafiri wa umma kwa kuwa ana shangingi. Huo utafiti wake kaufanya wapi haraka haraka namna hiyo. Reli imekuwa ikiboreshwa almost kila siku, na hata ukipita kando ya reli ya kati hadi Ubungo kuna matengenezo yanaendelea. Wamwache waziri afanye kazi ya wananchi
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,750
kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977
sehemu ya 3 haki na uhuru wa mawazo kifungu cha 18(1)
kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake....
 

Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,398
1,225
Ujumbe huu umfikie mnyika,hajachaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuleta mawazo hasi(negative),amechaguliwa ili alete maendeleo,badala ya kushauri nini kifanyike kuboresha yeye anaanza kuleta negativity we don't want such kind of leaders,'mnyika don't just sit there and complaining/murmuring do something'
inasikitisha kuona viongozi wetu wanakuwa na mwelekeo hasi.
Mbunge ukilalamika mwananchi unategemea afanye nini?mbunge ama kiongozi unatakiwa uchukue malalamiko na uyafanyie kazi upate solution.familia yako ipo inalala njaa na wewe kama baba wa familia unakuja kuwaambia kuwa unajua sababu zinazofanya walale njaa,hizo ni akili?watakula ripoti ama ulete chakula mezani wale?kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977
sehemu ya 3 haki na uhuru wa mawazo kifungu cha 18(1)
kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake....
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,750
sidhani kama mbunge alikuwa na nia mbaya kwa usafiri huu wa treni wakati mwingine kukosoa ni namna nyingine ya kuweka sawa au kutaka jambo liwe sawa . sijui kwa nini watu wamechukulia vibaya namna hiyo.
 

malaka

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,328
1,500
kuna biashara unaweza vumilia hasara huku ukitarajia faida soon. Ila kwa hili la tren jm yupo sawa hata hela ya kujiendeshea sijui kama itapatikana. Ingawa sijauona mchakato mzima ila hasara haikwepeki pale.
 

mbish

Member
Oct 27, 2011
85
125
wakat mwingine wanasiasa hasa wabunge waache unafiki kama ameona mapungufu anashindwa kwenda kwa waziri au kumuandikia na kumpa hizo taarifa za utafiti wake?, hiyo siasa mbofumbofu aache atalikosa jimbo kizembe, yeye kama mbunge ana uwezo wa kwenda kwa waziri na kumpa hizo taarifa za utafiti wake wa hizo hasara. By the way mwakyembe amefanya kitu tofauti na waliomtangulia. Dar es salaam usafiri ni shida sana amekuja na wazo lililo ndani ya uwezo wake.
 

Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,398
1,225
Nimekumbuka msemo wa masaburi 'viongozi(wabunge ) wa dar wanafikiria kwa kutumia makalio'
 

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,826
2,000
Binafsi natamani nione hoja ya mnyika kama ilivyo, vinginevyo kama hoja yake ni kuingiza siasa kukosoa mradi wa treni per se, basi mnyika ameacha kuwa kiongozi makini na rational tuliyemzoea na sasa na yeye ameanza kuiga wengine kutafuta tu umaarufu wa kisiasa; Vinginevyo bado naamini kwamba taarifa Rasmi ya Mnyika haijalenga kubeza mradi huu bali kwanza kutanguliza hoja juu ya umuhimu wake/faida zake kabla ya kurukia hoja juu ya hasara za mradi husika, kwani ni dhahiri mradi huu unahitajika sana na ulikuwa way past due, na zipo changamoto ambazo zilitarajiwa; Muhimu zaidi, ni kwa Mnyika kuja na mawazo juu ya jinsi gani mradi huu unaweza kuboreshwa zaidi na kupunguza changamoto husika;

Kama mnyika kasema yanayosemwa humu, basi ni muhimu aelewe mambo matatu muhimu:


  1. A proper approach ya kuangalia mradi huu ni kufanya a cost - benefit analysis, na ni dhahiri kwamba the benefits outweigh the costs;
  2. Miradi ya namna hii utengeneza faida pale tu inapopata ruzuku kubwa ya serikali, na ukweli huu ni kwa nchi zote, sio Tanzania tu;
  3. Iwapo na yeye anaita treni hii ni ya 'mwakyembe', ni muhimu asahihishe hilo kwani treni hii ni ya umma wa watanzania bila ya kujali itikadi zao za siasa;
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,958
2,000
Sasa Mnyika nini kifanyike? Sie wapiga kura wa Ubungo gogo limetuokoa sana na mafoleni.
 

Osia

Member
Sep 1, 2012
57
0
Tusimukumu mnyika labda amefanya cost-benefit analysis.pia mali ya umma inafanywa shamba la bibi ktk utawala wa CCM.
Lkn c jambo la busara kuupima mradi kwa cku za usoni, hasa kwa hili ya mwakyembe. Lazima kuwe na gharama na changamoto nyingi sana, alichotakiwa kufanya mnyika ni kutoa m'badala wa nn kifanyika ili kunusuru hio hasara kuliko kuanika na kutotoa suluhisho la tatizo unakuwa hujawa msaada bali umekuwa sehemu ya tatizo
 

Jalem

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
217
0
Nathubutu kusema huyo mbunge ni mp.....mbavu,na mjue kuwe kuanza kula hasara mwanzoni sio tatizo,angalieni makampuni makubwa kama google,amazon,etc nyingi zilianza kula hasara for over 5 years mpaka zikaja kupost profit na kuwa mega companies,hilo lilikuwa wazo la waziri kutaka kupunguza tatizo,suala la utendaji,mkurugenzi wa trc si yupo?yeye ndio anatakiwa atoe mchanganuo wa namna ya kuendeleza huo usafiri uje kuwa profitable,huyo mbunge wa ubungo inaonyesha uwezo wake wa kufikiri kwa sababu asijaribu kujitoa hapo kwani yeye sio serikali?yeye akiwa kama kiongozi ametoa ushauri gani ili kuboresha?hii inaonyesha ana upeo finyu wa kufikiri.yeye alitoa wazo gani ili kupunguza tatizo la usafir?ama kajiona baada ya kukaa kwa dakika kadhaa na watu wake akinywa kahawa na kucheza bao anaona aikandie serikali,,mbunge wa ubungo chapa kazi,leta mawazo chanya katika kuboresha usafiri wa treni ama furaha yako ni kuona usafiri wa treni unakufa na wananchi wanarudi katika matatizo yao?samahani kama nimewaudhi lakini penye ukweli yatubidi tuseme ukweli
Big up mwana wane, nimekukubali kwa ukweli wote, na mm nasema hv, siyo lazima serikali ifanye kila kitu, mbunge ni mtu muhimu sn kutengeneza mazingira yawe safi ukijua wazi kuwa hao ni wapiga kura wake, kama kunahasara aonyeshe namna ya kuiondoa nakusaidia usafiri uboreshwe, atoe hata pesa zake kusaidia watu wake,
Yeye ni kijana sana, khy atatumia tu huo usafiri kwani mashangingi tunaachiana,
namshuri sn awe karibu sn na mwakiemebe amsaidie sn ili kuboresha siyo kukandia wananchi ndio wanaoumia.
 

december

Member
Jul 31, 2011
66
0
Humu vijana wetu wangekuwa wanapita mbona wangekuwa wanafaulu maana wanapata practical training na wakichanganya na za kwao wanatoka na kitu kizuri, nimependa maoni yako ila bado na maoni ya Mnyika yanatakiwa yachukuliwe kama tahadhari japokuwa alitakiwa aje na sotution au kubainisha hayo mapungufu kwa undani ili wayafanyie kazi yasitokee
Hiyo nyekundu ndo kitu gani sasa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom