Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,752
139,556
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
 
Hii Treni Mara ya mwisho kufanya kazi Waziri wa Mambo ya ndani alikuwa Mbunge wa Moshi vijijini Ndg Augustine Lyatonga Mrema wakati huo Ndg Magufuli alikuwa zake Viwandani Mwanza

Kwa niaba ya Ndugu zangu wa kichaga wenye roho za Mengi na wenye roho ya Ufo saro tunakupongeza sana
 
Hii Treni Mara ya mwisho kufanya kazi Waziri wa Mambo ya ndani alikuwa Mbunge wa Moshi vijijini Ndg Augustine Lyatonga Mrema wakati huo Ndg Magufuli alikuwa zake Viwandani Mwanza

Kwa niaba ya Ndugu zangu wa kichaga wenye roho za Mengi na wenye roho ya Ufo saro tunakupongeza sana
Hii Treni ilihujumiwa na ccm na sasa wanajifanya kuifufua halafu wanataka wasifiwe hahaa mabingwa wa kutengeneza tatizo halafu kuja kulitatua kwa mbwembwe.
 
Mtu unaondoka dar saa 10 jioni unafika moshi saa 2 asubuhi. Si bora kupanga gari za "MAGAZETI".
Tehe tehe,pinga pinga hamkosi la kusema
Treni ipo fully booked mpaka 31 dec
Hakuna mchagga atakusikiliza wewe wakati anafika moshi kwa 15,000
Waendao moshi miezi ya december ilikua ni kilio na kusaga meno,hayo masaa ulioyataja ndio walikua wanayatumia kulala ubungo kusubiri basi lije halafu nauli ilikua 90,000
 
Moja kati ya faida ya upinzani...kama upinzani ingekua haujakomaa Arusha na Moshi hii reli isingelifufuliwa.
Serikali ya ccm inaumiza kichwa wafanye nn ili wapiga kura wabadilishe mwelekeo kwenye chaguzi zijazo..Mwisho wa siku watu wanapata maendeleo.

Action and Reaction are equal and opposite.

NOTE; MOSHI NA ARUSHA ENDELEENI KUCHAGUA UPINZANI MUPATE MAENDELEO.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom