Treni ya Dar es Salaam; Safari mbili tu kwa siku, kwa nini?!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni ya Dar es Salaam; Safari mbili tu kwa siku, kwa nini?!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Oct 2, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Nimesoma maneno yafuatayo kutoka kwa msemaji wa TTL, Midladjy Maez, na kushindwa kuamini macho yangu;

  “Tayari mabehewa 14 yamekamilika ambapo kutakuwa na treni mbili ambazo kila moja itakuwa na mabehewa sita pamoja na mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.”

  Akizungumzia ratiba ya treni hiyo, Maez alisema kuwa kutakuwa na safari mbili kwa siku.

  “Asubuhi kutakuwa na treni kutoka Ubungo Maziwa hadi mjini, jioni treni hiyo itatoka mjini hadi Ubungo Maziwa. Vituo vya treni vitakuwa vinane na itakuwa ikibeba abiria 950 na kila behewa litapakia abiria 160.”

  Nashindwa kuelewa kama hapa kweli kuna jitihada makini za kutatua tatizo la msongamano Dar, au labda tumeanza kuhujumiana na wale wanaomiliki daladala; safari mbili tu kwa siku, why??????????
   
 2. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mkuu hiyo ni sawa kwa kuanzia kwa kuwa wanatakiwa kuangalia mazingira kwanza na kujua ni wakati gani wanapaswa kufanya kuongeza idadi ya safarfi. hata katika baadhi ya nchi za jirani nilizowahi kufika nimekuta wakifanya hivyo, inabdi tushukuru kwa kuanza watabadilika baadaye kadiri mahitaji yakakavyoongezeka mkuu.
   
 3. awp

  awp JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mi naona imeanzishwa kwa ajili ya msaada kwa wanafunzi tuu, thats why times 2 per day. si unajua Alichoki academy wanavyopata shida?
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hata kama safari mbili ni kwa majaribio lbado hai-make sense. Safari mbili wakati wa peak hours ni chini sana. Watasababisha msongamano kwenye train ambao utaleta hatari, watu wakijua kuna nafasi moja tu ya kupanda treni toka mjini au kwenda mjini. Hawajafikiria kwamba hiyo asubuhi au jioni karibu dunia yote ya Dar inayotumia daladala itatataka kwenda kupanda train? Hali haitakuwa salama!
   
 5. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Sumatra yakwamisha usafiri wa treni Dar
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 01 October 2012 20:27
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]USAFIRI wa treni ya abiria uliokuwa umepangwa kuanza jijini Dar es Salaam jana umekwama kufuatia Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutopewa leseni na kutoidhinishiwa viwango vya nauli na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

  Uongozi wa TRL ulisema jana kuwa, inasubiri kauli ya mwisho ya Sumatra kuhusu usafiri huo ili itoe taarifa rasmi kwa umma juu ya treni hiyo kuanza huduma ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

  Msemaji wa TRL, Midladjy Maez aliliambia gazeti hili jana kuwa usafiri huo unatarajiwa kuanza kazi siku yoyote kuanzia sasa, lakini mpaka Sumatra watakapotoa leseni ya usafirishaji na kuweka viwango vya nauli.

  Alisema tayari wamewasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vya nauli na kuomba leseni ya usafirishaji Sumatra, ikiwa ni pamoja na kuitaka mamlaka hiyo ikague treni hiyo kujiridhisha na usalama wake.

  “Hatuwezi kusema usafiri utaanza lini, lakini tayari kila kitu kimekamilika kwa sababu tulishapeleka Sumatra mapendekezo ya nauli na maombi ya leseni ya usafirishaji na sasa tunachosubiri ni majibu...,” alisema Maez na kuongeza;

  “Tunafahamu kuwa, watu wengi wanataka kujua siku ya kuanza usafiri wa treni, ila tunaomba wasubiri maandalizi yakikamilika kila kitu kitawekwa wazi…”

  Maez alifafanua kuwa usafiri huo utajumuisha mabehewa 14 ambayo kwa sasa yote yapo tayari na kwamba kutakuwa na treni mbili zitakazokuwa na mabehewa sita kila moja, mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.

  “Tayari mabehewa 14 yamekamilika ambapo kutakuwa na treni mbili ambazo kila moja itakuwa na mabehewa sita pamoja na mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.”

  Akizungumzia ratiba ya treni hiyo, Maez alisema kuwa kutakuwa na safari mbili kwa siku.

  “Asubuhi kutakuwa na treni kutoka Ubungo Maziwa hadi mjini, jioni treni hiyo itatoka mjini hadi Ubungo Maziwa. Vituo vya treni vitakuwa vinane na itakuwa ikibeba abiria 950 na kila behewa litapakia abiria 160.” alisema Maiz.

  Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya TRL, Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema taarifa zitawekwa wazi baadaye na kusisitiza kuwa usafiri huo uko chini ya taasisi mbalimbali za Serikali.

  “Taratibu za kuhakikisha treni inaanza kutoa huduma zinaendelea na taarifa rasmi itatolewa.”

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo alisema kuwa, pamoja na kuchelewa, usafiri huo wa treni utaanza ndani ya mwezi huu kama ilivyopangwa.

  “Hatukusema kuwa usafiri utaanza Oktoba Mosi, bali tulisema utaanza mwezi Oktoba na hakuna kilichobadilika mpango huo bado upo palepale,” alifafanua Chambo.

  Hivi karibuni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema usafiri huo utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika ukarabati wa reli kutoka Ubungo hadi Stesheni.

  Alisema kufikia mwezi huu, treni hiyo itaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.

  Mabasi ya Dart
  kubeba abiria 140

  Wakati huohuo; aina saba za mabasi yenye uwezo wa kupakia abiria 60 hadi 140 yanatarajiwa kutumika katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) unaotarajiwa kuanza katika hatua ya majaribio mwezi huu.

  Mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Jiji la Dar es Salaam mwaka 2014.

  Dart ni mfumo mpya wa usafiri wa umma unaoanzishwa jijini hapa utakaotumia mabasi makubwa yaendayo haraka kwa kutumia njia maalumu.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usafirishaji na Maendeleo wa Dart, Asteria Mlambo alisema; “Dira yetu ni kuwa na mfumo wa usafiri wa umma wa gharama nafuu unaowapatia faida waendeshaji.”

  Alisema mabasi hayo lazima yakidhi viwango vya ubora wa huduma hususan unaozingatia uhifadhi wa mazingira na utumiaji wa njia maalumu.

  Alisema mpango madhubuti wa DART ni kuboresha matumizi ya barabara ili kupunguza msongamano usio wa lazima kwa kuweka njia maalumu .

  Alisema huduma bora inayopatikana katika mradi huo itachangia kuondoa au kupunguza umaskini, kuinua hali ya maisha, kuleta ukuaji wa uchumi jijini Dar es Salaam na itachochea ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi katika nyanja ya usafirishaji.
  Mradi wa mwendo kasi unatarajiwa kuokoa Sh4 bilioni, ambapo utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Muungano wa Wenye Viwanda nchini (CTI) umebainisha msongamano wa magari unasababisha hasara ya asilimia 20 kwa wafanyabiashara na wafanyakazi kuchelewa kazini.

  CHANZO:MWANANCHI

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 6. b

  bdo JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Mimi nilijua hii kitu itakuwa inafanya kazi atleast 12hrs kwa siku, sasa ina maana gani - treni mbili, halafu moja inakuwa asubuhi na ingine jioni basi, na inawezekana hakuna cha mabehewa 14 ila yapo hayohayo 6 tu, labda tujulishwe kuna sababu gani za kiufundi zinazozuia hii kitu isiwe inafanyakazi hata kwa masaa 12? hivi nauli inakuwa ni kiasi gani?

  Pia angalieni kituko kingine hicho: ina maana SUMATRA walijua ni utani? Jamani unajua mie nilishaapa kabisa katu sitakuja fanya kazi serikalini, kwa sababu ya mambo haya ya urasimu, they dont believe in team work, hata hawategemeani, ni wavivu wa kuamua, tusubiri tuone, utaambiwa sheria hazikufutwa, je walikuwa wapi kuona sheria zinafuatwa
   
 7. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 01 October 2012 20:27
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]USAFIRI wa treni ya abiria uliokuwa umepangwa kuanza jijini Dar es Salaam jana umekwama kufuatia Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutopewa leseni na kutoidhinishiwa viwango vya nauli na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

  Uongozi wa TRL ulisema jana kuwa, inasubiri kauli ya mwisho ya Sumatra kuhusu usafiri huo ili itoe taarifa rasmi kwa umma juu ya treni hiyo kuanza huduma ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

  Msemaji wa TRL, Midladjy Maez aliliambia gazeti hili jana kuwa usafiri huo unatarajiwa kuanza kazi siku yoyote kuanzia sasa, lakini mpaka Sumatra watakapotoa leseni ya usafirishaji na kuweka viwango vya nauli.

  Alisema tayari wamewasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vya nauli na kuomba leseni ya usafirishaji Sumatra, ikiwa ni pamoja na kuitaka mamlaka hiyo ikague treni hiyo kujiridhisha na usalama wake.

  “Hatuwezi kusema usafiri utaanza lini, lakini tayari kila kitu kimekamilika kwa sababu tulishapeleka Sumatra mapendekezo ya nauli na maombi ya leseni ya usafirishaji na sasa tunachosubiri ni majibu...,” alisema Maez na kuongeza;

  “Tunafahamu kuwa, watu wengi wanataka kujua siku ya kuanza usafiri wa treni, ila tunaomba wasubiri maandalizi yakikamilika kila kitu kitawekwa wazi…”

  Maez alifafanua kuwa usafiri huo utajumuisha mabehewa 14 ambayo kwa sasa yote yapo tayari na kwamba kutakuwa na treni mbili zitakazokuwa na mabehewa sita kila moja, mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.

  “Tayari mabehewa 14 yamekamilika ambapo kutakuwa na treni mbili ambazo kila moja itakuwa na mabehewa sita pamoja na mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.”

  Akizungumzia ratiba ya treni hiyo, Maez alisema kuwa kutakuwa na safari mbili kwa siku.

  “Asubuhi kutakuwa na treni kutoka Ubungo Maziwa hadi mjini, jioni treni hiyo itatoka mjini hadi Ubungo Maziwa. Vituo vya treni vitakuwa vinane na itakuwa ikibeba abiria 950 na kila behewa litapakia abiria 160.” alisema Maiz.

  Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya TRL, Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema taarifa zitawekwa wazi baadaye na kusisitiza kuwa usafiri huo uko chini ya taasisi mbalimbali za Serikali.

  “Taratibu za kuhakikisha treni inaanza kutoa huduma zinaendelea na taarifa rasmi itatolewa.”

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo alisema kuwa, pamoja na kuchelewa, usafiri huo wa treni utaanza ndani ya mwezi huu kama ilivyopangwa.

  “Hatukusema kuwa usafiri utaanza Oktoba Mosi, bali tulisema utaanza mwezi Oktoba na hakuna kilichobadilika mpango huo bado upo palepale,” alifafanua Chambo.

  Hivi karibuni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema usafiri huo utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika ukarabati wa reli kutoka Ubungo hadi Stesheni.

  Alisema kufikia mwezi huu, treni hiyo itaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.

  Mabasi ya Dart
  kubeba abiria 140

  Wakati huohuo; aina saba za mabasi yenye uwezo wa kupakia abiria 60 hadi 140 yanatarajiwa kutumika katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) unaotarajiwa kuanza katika hatua ya majaribio mwezi huu.

  Mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Jiji la Dar es Salaam mwaka 2014.

  Dart ni mfumo mpya wa usafiri wa umma unaoanzishwa jijini hapa utakaotumia mabasi makubwa yaendayo haraka kwa kutumia njia maalumu.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usafirishaji na Maendeleo wa Dart, Asteria Mlambo alisema; “Dira yetu ni kuwa na mfumo wa usafiri wa umma wa gharama nafuu unaowapatia faida waendeshaji.”

  Alisema mabasi hayo lazima yakidhi viwango vya ubora wa huduma hususan unaozingatia uhifadhi wa mazingira na utumiaji wa njia maalumu.

  Alisema mpango madhubuti wa DART ni kuboresha matumizi ya barabara ili kupunguza msongamano usio wa lazima kwa kuweka njia maalumu .

  Alisema huduma bora inayopatikana katika mradi huo itachangia kuondoa au kupunguza umaskini, kuinua hali ya maisha, kuleta ukuaji wa uchumi jijini Dar es Salaam na itachochea ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi katika nyanja ya usafirishaji.
  Mradi wa mwendo kasi unatarajiwa kuokoa Sh4 bilioni, ambapo utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Muungano wa Wenye Viwanda nchini (CTI) umebainisha msongamano wa magari unasababisha hasara ya asilimia 20 kwa wafanyabiashara na wafanyakazi kuchelewa kazini.

  CHANZO:MWANANCHI

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tz KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KILA KITU KUJARIBIA HAPO
   
 9. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Safari mbili kwa siku sio mbaya, kwani hii ni huduma mpya na muda huo uliotajwa wa asubuhi na jioni ndio muda unaokua na abiria wengi barabarani, Sio rahisi kupata abiria 900 saa sita mchana pale ubungo wanaoelekea mjini.
  Ila SUMATRA wajipange kwa ukaguzi na waidhinishe nauli, sio wasubiri boti zizame ndio watoe tamko.
   
 10. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilidhani lengo la hii treni ni kupunguza pia msongamano wa magari barabarani kutokana na wingi wa barabara. Ikiwa treni itafanya safari kila wakati nina uhakika daladala kwenda mjini zitapungua, ambalo ni jambo nzuri tu. Sio lazima treni ijaze abiria 900 kila tripu. Nina uhakika wakifanya safari za mara kwa mara watu wakazoea hii huduma watakuwa na wastani wa abiria karibu 500 kila tripu. Waweke vituo vya daladala karibu na stesheni za hiyo treni ili abiria waunganishe safari zao kirahisi kwenda Mwenge, Kimara , Siza nk
   
 11. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Tutatesa kimtindo manake madaladala yanachukua masaa 2 kufika mjini.
   
 12. p

  pilau JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Bila shaka Shirika la reli linao wataalamu na wameshafanya utafiti wa kina, labda ni kupokea ushauri wa hapa na pale kwa wadau. ... Hapa cha kuangalia na kuzingatia ni uwezo wa kubeba watu wengi kwa wakati mmoja, hasa asubuhi na jioni kama kila behewa watu 160 x 6(behewa) = watu 960 watu 960 ni wachache mno, kama coaster kijaza inachukua wastani wa watu 50, au DCM, yale magari makubwa ya injini nyuma yanapakia zaidi ya watu 100 wazingatie kwamba safari moja ya asubuhi ya kuwatoa watu ubungo kwenda kariakoo + Posta watu hawapungui 10,000 wanaokuwa tayari asubuhi kwenda mjini
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hii ngoma imekaa kisiasa zaidi trust me train itakuwa inajaa Ubungo Maziwa hao wa vituo vya mbele hawatapata nafasi na tusipokuwa makini kulimit idadi ya abiria, watu watapoteza maisha kwa kukosa hewa kutokana na msongamano wa watu.
  Bado sijapata mantiki ya kufanya safari 2 kwa siku, inatakiwa safari zianze saa 11 alfajiri
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Suala zima la usafiri wa treni linabidi liangalie kwa kina gharama za huduma hiyo kwa serikali. Wananchi kimsingi hatutaki kuanza kulipia huduma hii kutoka kodi zetu, kwa hiyo kuangalia ni wakati gani abiria wataweza kufidia gharama ni suala la msingi sana

  Asubuhi safari za kwenda mjini, matreni yanaweza kujaa sana, lakini matreni hayo yatakosa watu kabisa kutokea mjini kurudi kituoni kuchukua wengine kupeleka mjini.

  Sasa hapa nauli iweje hata iweze kufidia gharama za treni kurudi nje ya mji likiwa tupu?

  Suala hilo, ninadhani ndio sababu ya kulitaka treni libakie mjini, hadi litakapopata abiria wa kurudi nalo nje ya mji wakati wa jioni
   
Loading...