Treni kubeba abiria 5000

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
“Kwa kutambua hilo Mikakati ya kuboresha huduma hii ipo na kuanzia alhamisi ya Novemba 22, mwaka huu,TRL imeongeza mabehewa mawili zaidi na hivyo kuwa manane kutokana na ongezeko la abiria wanaosafiri kufikia zaidi 300 kwa kila mzunguko wa safari”alisema Kisamfu.

KAMPUNI ya Reli Tanzania(TRL) imesema abiria wanaopata huduma ya usafiri wa Treni katika Jiji la Dar es Salaam wanafikia idadi ya 5000 kwa kila siku kupitia mizunguko yote miwili.
Akijibu maswali kwa njia ya mtandao Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo, Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema kila mzunguko mmoja treni inabeba abiria 300 kwa nauli ya mwanafunzi na mtu mzima ambapo inadaiwa idadi ya abiria inazidi kuongezeka.

“Kwa kutambua hilo Mikakati ya kuboresha huduma hii ipo na kuanzia alhamisi ya Novemba 22, mwaka huu,TRL imeongeza mabehewa mawili zaidi na hivyo kuwa manane kutokana na ongezeko la abiria wanaosafiri kufikia zaidi 300 kwa kila mzunguko wa safari”alisema Kisamfu.

Kisamfu aliongeza kuhusu uharibifu wa mabehewa hali hiyo ni tatizo la usafiri wowote kwa umma ambapo hata Waziri wa Uhukuzi Dk Harrison Mwakyembe aliwahi kutoa wito akiwataka Wakazi wa jiji kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa viti na vifaa vingine katika mabehewa vitendo .

Aliongeza kuwa hata suala la usalama wa abiria ndani ya treni kila abiria anapaswa kutoa udhirikiano wa kulinda uharibifu kutokana na uhaba wa askari wanaosimamia usalama katika treni hizo.

“Wito kwa wale abiria wema wawadhibiti wenzao ambao wanawashuhudia wakitoboa viti na kuvunja vioo kwa vile kila behewa linakuwa na wastani wa abiria 150 ni vigumu askari mmoja kuwaona hao abiria watukutu kirahisi bila ya 'kuchongewa na wenzao waadilifu”alisema Kisamfu.

Akizungumzia ukarabati wa mabehewa machakavu yanayoonekana katika karakana za TRL Kisamfu alise mabehewa hayo hukarabatiwa kutokana na kiasi cha fedha zikipatikana na kurejeshwa tena katika huduma za reli.

“Kwa mfano katika mradi wa mabehewa 31 ambayo yameanza kukarabatiwa tokea mwezi Juni mwa huu, 14 kati ya hayo ni ya mradi wa treni ya jiji na 17 ni kwa ajili ya treni kutoka Dar kwenda Mwanza”alisema Kisamfu.

Kuhusu usumbufu unaojitokeza kupitia malipo ya chenji Kisamfu alisema TRL kwa sasa inajadiliana na Kampuni ya Selcom Wireless kuboresha huduma ambapo muda sio mrefu kutawepo utaratibu mpya wa kununua tiketi kwa wingi ambazo abiria ataweza kuzitumia kwa muda mrefu.

“Endapo Abiria atakutwa na tiketi haina alama ya mashine atahesabika kuwa amepanda bure na kustahili adhabu kwa mujibu wa taratibu,Hata hivyo kwa sasa Wakaguzi wanaendelea kukagua tiketi zetu na tahadhari tunayoitoa kwa wateja kuwa tiketi za huduma hii zinazotumika ni zile zenye tarehe ya siku husika ”alisema Kisamfu.Treni kubeba abiria 5000 - Biashara - mwananchi.co.tz






 
Ningekuwa na uwezo wa kukutana na kisamfu ningemueleza kuhusu cover za coach mafundi wanaweka kava za muda wangekuwa wanaweka cover ngumu,katk viti vya kukalia maana hv chukui muda kuchanika
 
Sijawahi Kupanda huu usafiri ila Nasikia hauna Muda maalumu wa kuondoka au kipita katika Vituo!! Kama ni kweli nawaomba wahusika watuondolee hii kero kwani ni sawa na kuwepo na watu wasiokuwa na upeo!! Wajue wazi hili sio changamoto ila ni suala la kutatua!! Wasituletee uswahili Hapa!!
 
Back
Top Bottom