Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,433
Wanabodi,

Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa trends na visions. Trends ni kusoma mielekeo, na visions ni kuona mambo yajayo ya mbali, hivyo trends za rais Magufuli anazokwenda nazo, kwa sisi waona mbali, tuliojaaliwa kupata visions za yajayo, tunaona kabisa mambo mazuri huko tuendako, ikiwemo katiba mpya!. Magufuli ni kama Nyerere, hivyo baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuacha legacy kubwa kwa taifa letu Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutupatia ya uhuru, umoja, amani, upendo na mshikamano wa Watanzania, rais Magufuli ndiye kiongozi mwingine atakayeacha the biggest legacy kubwa kabisa Tanzania ikiwemo kuitoa Tanzania katika kundi la nchi masikini na kuigeuza tajiri na kwenye siasa, atakuza demokrasia na kutuachia Katiba mpya!.

Mkutano wa Jana Pale UDSM
Mimi nikiwa ni alumni wa UDSM, nilipousikia mkutano huo, nami nilipanga kuhudhuria physically ili kusikia kwa masikio yangu mwenyewe, na kuona kwa macho yangu mwenyewe, hivyo nikapania lazima niende, lakini nilipoamka nikajisikia mzito na kuamua muufuatilia kwenye TV.

Kwa kweli mkutano ule ulikuwa well staged vizuri sana hadi rais Magufuli kukaa na wananchi kama mwananchi kabisa, ila stage setter alikosea kidogo kuweka kiti cha ikulu pale, the perfect stage, ilikuwa ni rais Magufuli kukalia kiti cha kawaida tuu ili isionekane ni pre arranged.

Watoa mada na wachangia mada were all well set ili wote kazi iwe ni moja tuu, kuunga mkono juhudi, na kufagilia kila kitu as if there is nothing wrong!, angalau Father Kitima, is the one and only who spoke the naked truth. Kama chuo kikuu ndio kisima cha maarifa na chemchem ya fikra, na hakukuwepo fikra zozote mbadala, hivyo unapokuwa na kongamano la kisomi la kutathmini miaka 3 ya utawala wa Magufuli, then kila presentation ni kusifu tuu bila critical thinking yoyote, unategemea nini?!, all and all, the arrangement was good kuhakikisha critical thinkers hawasogolei kipaza sauti, kwa kweli ni igizo zuri la onyesho zuri, la uzuri wa awamu ya 5, well staged, well planned na well executed and implemented, onyesho lilipendeza!.

Hatuba ya Rais Magufuli
Kama ilivyoelezwa, rais Magufuli hakupanga kuhutubia, alipanga kuwa msikilizaji tuu, ila uharaka wa kusimama alipoombwa tuu kuja kuhutubia huku hakupanga kuzungumza, na hotuba hile ya dakika 85 impromptu, leaves much to be desired!.

Nimekumbuka kisa kimoja cha Mwalimu Nyerere alialikwa gala dinner ya Rotary Club of Dar es Salaam, pale Serena, enzi hizo Sheraton, baada ya dinner Mwalimu akaombwa kusalimia na kusema machache, akasimama akasalimia, baada ya kusalimia, akasema "asanteni sana", Mwalimu alirudi kukaa, watu hawakuamini, ila ukumbi mzima ulipiga makofi kwa standing ovation.

Hivyo kama rais Magufuli hakupanga kuzungumza, halafu akazungumza impromptu kwa dakika 85!, then mtakubaliana na mimi, rais Magufuli speaks best impromptu, asipoandikiwa. The speech was so good, so natural, so genuine so touchy na kiukweli kabisa imenigusa, haswa his simplicity, it was very powerful speech, na hapo ndio hakupanga kuzungumza, jee angepanga?!

Katiba.
Kama alivyozungumza na sisi waandishi pale ikulu, alisema katiba mpya sio kipaumbele chake, jana pale USDM, rais Magufuli amerudia msimao huo kuwa hata tenga budget ya kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Nawaomba wapenda demokrasia, wasikatishwe tamaa na kauli hii, mimi nawahakikishia miongoni mwa legacy kubwa ambazo rais Magufuli ataziacha siku akiondoka madarakani, ni pamoja na kutuachia katiba mpya.

Ili kujua kuwa rais Magufuli atatuachia katiba mpya, angalieni hizi baadhi ya kauli zake na alikuja kufanya nini. mfano ile ya "sitateua wapinzani katika serikali yangu" na angalia nini kimetokea, hivyo hata hata hii kauli ya katiba sio kipaumbele changu, ni kauli tuu, sio kila anachofanya rais Magufuli ni lazima kiwe kipaumbele chake, vipaumbele vingine ni over and above vipaumbele vyake, kwani unadhani yeye rais Magufuli alijua kuwa ndiye atakuwa rais wa nchi nchi hii 2015?, yeye hakujua, alijaribu tuu, na ikatiki, akijihesabu imetokea tuu, lakini kuna watu tulijua!.

Leo wakati nayazungumza haya, inawezekana hata rais Magufuli mwenyewe, bado hajui wala hajajijua kuwa ni yeye ndiye atakayetuachia katiba mpya, kwa jinsi ile ile akina sisi tulipojua siku nyingi kabla kuwa rais wetu wa 2015 ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, wakati huo hata yeye mwenyewe atakuwa alikuwa hajui, alipoamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, yeye alikuwa anajua kuwa anajaribu tuu kwa ku beep, kumbe kuna watu siku nyingi waliishampangia bila mwenyewe kujijua. Angalia tarehe ya bandiko hili, na sababu zilizofanya rais wetu wa 2015 akawa ni Magufuli, ndizo sababu hizo hizo zitamfanya rais Magufuli atuletee katiba mpya kabla ya 2025!.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Mambo ya visions ni maono sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, ni mambo ya ulimwengu wa roho, hivyo nawaomba sana wanabodi, msiniulize chochote kuhusu maono haya hadi tutakapokumbushana ile siku yanatimia.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
 
Yaani unajaribu kutushawishi na sisi tuingie kwenye hiyo nyumba yenu ya ibada kumuabudia huyo jamaa?
mtu anayeona sheria kwake ni kikwazo cha kufikia malengo? Mtu anayependa kutawala kwa amri na mabavu ya kijeshi eti leo akuletee katiba mpya?
Una ruhusa ya kutoa maoni yako lakini usijitwishe jukumu la kutushawishi kukubaliana na demokrasia ya kikanda. Huyo anayetamani bunge lisiwepo au lote liwe ni la kuunga mkono hoja ndiyo unataka kuotesha watu kuwa ataleta katiba mpya? Labda katiba ya kiimra
 
Kama kawaida yako.. the last nail on the coffin......
Mkandala alikuwa anasifia lakini Kwa tahadhari kubwa, ni kama mwalim aliekupa 40% ili kukuepusha na carry over lakini baado somo hujalielewa vizur
Nadhani hata Shivji alijitaid Sana...
Mungu akulinde na watekaji mkuu....
 
Kwa heshima na taadhima naunga suala la Magu kuachana na suala la katiba mpya kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee itakayohakikisha kwamba JPM ataondoka madarakani hapo 2025!

Ukweli ni kwamba, naogopa sana suala la mchakato wa Katiba Mpya kufanyika kipindi cha Magufuli! Napata shida sana kumtofautisha huyu jamaa na akina Museven!

Does anyone believe kwamba Katiba Mpya under Magufuli Administration itakuwa ni Katiba Mpya kwa ustawi wa taifa na sio kwa ustawi wa Magufuli Administration?!

Ni nani atakayeweza kuuzima moto wa wale wendawazimu wanaotaka JPM aendelee kutawala kwa miaka 40?! Ni nani atakayeweza kuuzima moto wa Bunge lijalo ambalo litakuwa at least 90% ni CCM... bunge ambalo litajaa wendawazimu ambao bila shaka nao wataota Katiba Mpya iondoe ukomo wa uongozi?

Au mnadhani JPM's conscious is 100% pure kama ilivyokuwa kwa JK au BM kwamba, akimaliza tu muda wake atatamani kuondoka?! Guys... huyu jamaa akipata support kwamba atawale milele, atatawala kama wanavyofanya maswahiba wake! Ogopa watu wanaotawala kwa kaulimbiu za "uzalendo" huku wakijaribu kuficha madudu yao kwenye kichaka chao cha uzalendo!

Watu wa aina hii hawaamini kama kuna mtu mwingine somewhere anayeweza kuongoza "vizuri" kama yeye! Hawa akina Kagame na akina Museveni ni kwa sababu tu wanaamini hakuna anayeweza kuongoza nchi zao "vizuri" kama wanavyoongoza wao!

So, thanks Magufuli kwa kupiga chini Katiba Mpya manake, bila kujijua, nadhani watu wanataka wakuhalalishie udhalimu mwingi wa kisiasa unaofanywa na utawala wako ili hatimae udhalimu huo uwe kwenye katiba!!

Na kama ni Katiba Mpya, basi mchakato uanze somewhere from 2023 na ianze kutumika baada ya kuwa ameshaondoka 2025! Kwa sasa muhimu kwangu labda mabadiliko ya kifungu kinachokataza kupinga matokeo ya urais mahakamani!

I still believe mabadiliko yoyote ya katiba kwa sasa yatalenga sana kuhalalisha yale yanayopingwa na Wanademokrasia na Wanamageuzi kuliko vinginevyo! Ingawaje JK hakuwa mtu wa ku-interfere Bunge lakini lilipokuja suala la Katiba Mpya ali-interfere Bunge la Katiba only to defend Serikali Mbili!! What about this Guy ambae tayari haaminiki linapokuja suala la interference?!

Hata hivyo, kwa kiasi fulani nakubaliana na Pascal kwamba JPM anaweza kuacha katiba! Imani yangu hii inatokana na silika ya JPM kutaka kufanya yale yanayoonekana wenzake walishindwa!
 
Watoa mada na wachangia mada were well set ili wote kazi iwe ni moja tuu, kuunga mkono, na kufagilia kila kitu as if there is nothing wrong!, angalau Father Kitima, is the one and only who spoke the naked truth. Kama chuo kikuu ndio kisima cha maarifa na chemchem ya fikra, na hakukuwepo fikra mbadala, then the arrangement was good kuhakikisha wenye fikra mbadala hawasogolei kipaza sauti, ni onyesho zuri, well staged, well planned na lilipendeza.
Nimependa hii para kwenye bandiko lako, good observation
 
Kama wale ma Professor wa udsm yale ndo walikua wanayatoa moyoni jana kwenye kongamano bas sipotezi tena mda wa kuomba kutuma maombi ya kusoma kumbe ki diploma changu kutoka chuo cha kata na GPA yangu ya 2.7 kinaweza kukocompete kabisa na hao wa udsm. Aibu sana
 
Nakubaliana na wewe. muda utatueleza maana jana kasema anajua tunataka katiba mpya kwa kinywa chake.
 
Kama wale ma Professor wa udsm yale ndo walikua wanayatoa moyoni jana kwenye kongamano bas sipotezi tena mda wa kuomba kutuma maombi ya kusoma kumbe ki diploma changu kutoka chuo cha kata na GPA yangu ya 2.7 kinaweza kukocompete kabisa na hao wa udsm. Aibu sana
Huwezi kumchalleng anayekulipa,kumbuka wengi wako kwenye jicho la uteuzi, pale ndo sehemu ya kujulikana ni bidii yako tu kusifu na kuabudu
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa trends na visions. Trends ni kusoma mielekeo, na visions ni kuona mbali, hivyo trends za rais Magufuli anazokwenda nazo, kwa sisi waona mbali, tunaona kabisa mambo mazuri huko tuendako, ikiwemo katiba mpya!. Magufuli ni kama Nyerere, hivyo baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuacha legacy kubwa kwa taifa letu Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutupatia ya uhuru, umoja, amani, upendo na mshikamano wa Watanzania, rais Magufuli ndiye kiongozi mwingine atakayeacha legacy kubwa kabisa Tanzania ikiwemo Katiba mpya!.

Mkutano wa Jana Pale UDSM
Mimi nikiwa ni alumni wa UDSM, nilipousikia mkutano huo, nami ningeweza kuhudhuria ili kusikia kwa masikio yangu mwenyewe, na kuona kwa macho yangu mwenyewe, hivyo nikapania lazima niende, lakini nilipoamka nikajisikia mzito na kuamua muufuatilia kwenye TV.

Kwa kweli mkutano ule ulikuwa staged vizuri sana hadi rais Magufuli kukaa na wananchi kama mwananchi kabisa, ila stage setter alikosea kidogo kuweka kiti cha ikulu pale, the perfect stage, ilikuwa ni rais Magufuli kukalia kiti cha kawaida tuu ili isionekane ni pre arranged.

Watoa mada na wachangia mada were well set ili wote kazi iwe ni moja tuu, kuunga mkono, na kufagilia kila kitu as if there is nothing wrong!, angalau Father Kitima, is the one and only who spoke the naked truth. Kama chuo kikuu ndio kisima cha maarifa na chemchem ya fikra, na hakukuwepo fikra mbadala, then the arrangement was good kuhakikisha wenye fikra mbadala hawasogolei kipaza sauti, ni onyesho zuri, well staged, well planned na lilipendeza.

Hatuba ya Rais Magufuli
Kama ilivyoelezwa, rais Magufuli hakupanga kuhutubia, alipanga kuwa msikilizaji tuu, ila uharaka wa kusimama alipoombwa tuu kuja kuhutubia huku hakupanga kuzungumza, na hotuba hile ya dakika 85 impromptu, leaves much to be desired.

Nimekumbuka kisa kimoja cha Mwalimu Nyerere alialikwa gala dinner ya Rotary Club of Dar es Salaam, pale Serena, enzi hizo Sheraton, baada ya dinner Mwalimu akaombwa kusalimia na kusema machache, akasimama akasalimia, baada ya kusalimia, akasema "asanteni sana", Mwalimu alirudi kukaa, watu hawakuamini, ila ukumbi mzima ulipiga makofi kwa standing ovation.

Hivyo kama rais Magufuli hakupanga kuzungumza, halafu akazungumza impromptu kwa dakika 85, then mtakubaliana na mimi, rais Magufuli speaks best asipoandikiwa. The speech wa so natural, so genuine na kiukweli kabisa imenigusa, haswa his simplicity, it was very powerful speech.

Katiba.
Kama alivyozungumza na sisi waandishi pale ikulu, alisema katiba mpya sio kipaumbele chake, jana pale USDM, rais Magufuli amerudia msimao huo kuwa hata tenga budget ya kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Nawaomba wapenda demokrasia, wasikatishwe tamaa na kauli hii, mimi nawahakikishia miongoni mwa legacy kubwa ambazo rais Magufuli ataziacha siku akiondoka madarakani, ni pamoja na kutuachia katiba mpya.

Ili kujua kuwa rais Magufuli atatuachia katiba mpya, angalieni hizi baadhi ya kauli zake na alikuja kufanya nini. mfano ile ya "sitateua wapinzani katika serikali yangu" na angalia nini kimetokea, hivyo hata hata hii kauli ya katiba sio kipaumbele changu, ni kauli tuu, sio kila anachofanya rais Magufuli ni lazima kiwe kipaumbele chake, vipaumbele vingine ni over and above vipaumbele vyake, kwani unadhani yeye alijua ndiye atakuwa rais wa nchi nchi hii 2015?, kuna watu tulijua!.

Leo wakati nayazungumza haya, inawezekana hata rais Magufuli mwenyewe, bado hajajijua kuwa ni yeye ndiye atakayetuachia katiba mpya, kwa jinsi ile ile akina sisi tulipojua siku nyingi kabla kuwa rais wetu wa 2015 ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, wakati huo hata yeye mwenyewe hajui, alipoamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, yeye alikuwa anajua kuwa anajaribu tuu kwa ku beep, kumbe kuna watu siku nyingi waliishampangia bila mwenyewe kujijua. Angalia tarehe ya bandiko hili, na sababu zilizofanya ni Magufuli, ndizo sababu hizo hizo zitamfanya rais Magufuli atuletee katiba mpya
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Mambo ya visions ni maono, nawaomba sana msiniulize chochote kuhusu maono haya hadi tutakapokumbushana ile siku yanatimia.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Asante Paskali, Lakini angalia maneno haya ( " could be" John Pombe Magufuli) yalinganishe na " ni John Pombe Magufuli". Na siku ukishinda kamali sitashangaa.
 
Mkuu atakubali kiurahisirahisi kubadili katiba na kuruhusu katiba itakayopendwa na watanzania walio wengi hususan wapinzani?
Maana kuna sheria ambazo zinaweza kubadilisha na kumuadhibu matendo yake aliyoyafanya kipindi yupo madarakani.
Labda ataruhusu mchakayo ufanyike alafu wataitia kapuni na kuleta katiba iliyopendekezwa kama alivyotifanyiaga Sita.
 
Back
Top Bottom