Trend reading zaonyesha Tanzania njema kisiasa, Rais Magufuli is changing for the better!. Je, soon kukaa na wapinzani, kuruhusu mikutano ya siasa?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,844
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,844 2,000
Wanabodi,
Mode: Kunapotokea jambo kubwa, jema, zuri lenye manufaa kwa mustakabali wa taifa leo, naomba ruhusu free flow of information kuhusu jambo hilo kwa kuruhusu hata threads 100 zenye mawazo na mitazamo tofauti tofauti zipande, kisha zitakuja kuunganishwa mbele ya safari, lakini isiwe kwa vile rais Magufuli amehutubia Mwanza, hivyo chochote kumhusu Magufuli Mwanza leo kitaunganishwa!.

Kufuatia ukubwa wa tukio la leo, mimi na makala zangu za Kwa Maslahi kwa Taifa, nimeona kuna maslahi makubwa kwa taifa, hiki kilichotokea leo, kiandikiwe makala ya Kwa Maslahi ya Taifa, kwasababu hiki kilichofanyika ni jambo kubwa, jambo la heri, jambo la neema na lenye maslahi makubwa sana kwa mustakabali wa siasa za nchi yetu. Rais Magufuli hongera sana kwa hili la leo.

Kwanza tukubaliane, yule Magufuli aliyelizindua Bunge jipya na kusema, asitegemewe kufanya kazi na Wapinzani, wala kuteua Wapinzani, na Magufuli huyu aliyehutubia hotuba bora kuliko zote katika Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru pale Mwanza, ni Magufuli mwingine tofauti. Huu ni uthibitisho kuwa this man is changing for the better towards the direction ya kuelekea kuwa the best president this nation had ever had!.

Baada ya kilichofanyika leo pale Mwanza, Rais Magufuli amefungua ukurasa mpya wa siasa za ushirikiano, na trends zinaelekeza soon atakaa na Wapinzani kuwasikiliza malalamiko yao, kama alivyokaa na wafanyabiashara, na huenda akaruhusu mikutano ya Siasa kwa nchi nzima na ushindani sawa na haki kwa vyama vyote kwenye medani za kisiasa, ili angalau uchaguzi mkuu wa mwakani, usiwe kama huu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa CCM kupata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani kuweka mpira kwapani, bali uchaguzi wa 2020, CCM itapata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwa kipute cha dakika 90 za uwanjani na sio kwa ushindi wa mezani.

Wiki iliyopita, mimi na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, tulialikwa katika Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kushriki mjadala wa kutathmini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia Star TV. Wote wawili tulikubaliana kuwa japo CCM imeshinda kwa kishindo cha asilimia 99.9%, sio ushindi mtamu kwasababu legitimacy ya uchaguzi wa kidemokrasia ni ushindi unaopatikana kwa kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na sio ushindi wa mezani wa kupita bila kupigwa.

Balile akazungumzia madhila yanayowakuta viongoz wa upinzani kwenye awamu hii ya 5, kwa kuzuiwa kufanya mikutano, huku wakikabiliwa na mlolongo wa kesi. Sote tukakubaliana kuwa rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, wanafanya kazi nzuri ya kuwaletea Watanzania, maendeleo, na sote tukakubaliana kuwa rais Magufuli bado anaweza kuleta maendeleo huku akiruhusu demokrasia kushamiri.

Sote tukashauri, kama rais Magufuli ameweza kumshauri DPP kuwasamehe hata mafisadi, basi anaweza kumshauri DPP kufuta kesi zote za jinai zinazowakabili viongozi wa upinzani, na kuruhusu mikutano ya kisiasa nchi nchi nzima.

Kwa kuwasamehe na kufuta kesi zote zinazowakabili viongozi wa upinzani, na kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa, rais Magufuli, CCM na serikali yake, have nothing to loose and everything to gain ikiwemo trust, peace, harmony and tranquility.

Magufuli yule aliyelihutubia Bunge kulizindua, ndiye aliyesema asitegemewa kama atateau mpinzani, lakini Magufuli huyu wa sasa, ndiye aliyemtea Mama Anna Mngirwa na Dr. Kitila Mkumbo ndani ya serikali yake tena wakiwa bado upinzani. Ndiye aliyemtea Dr. Wilbroad Slaa kuwa balozi, bila kutangaza kuwa amejiunga CCM, ndiye amepokea makumi kwa mamia ya wabunge, madiwani na wapinzani wanaoviacha vyama vyao, na kuwapokea CCM ikiwemo kuwatea katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Sasa huyu Magufuli wa leo, ndio anazidi kubadilika and getting better and better towards the direction of being the best, kwa kuwaalika viongozi wa upinzinzani kusalimia Watanzania katika sherehe ya kitaifa, kuonyeshea, pamoja na tofauti zote za kisiasa, lakini tunapokuja kwenye jambo lenye maslahi ya kitaifa, sisi Watanzania ni wamoja, na leo rais Magufuli amelithibisha hili.

Kufuatia tukio hili la leo ambao limefungua ukurusa mpya katika siasa za Tanzania, trends zinaelekeza, soon rais Magufuli atawafungulia milango ya ikulu wapinzani kusikiliza malalamiko yao, na naamini kabisa, soon ile marufuku ya mikutano ya kisiasa itaondolewa.

Tena to be honest, something tells me rais Magufuli ataacha legacy ya ajabu atakapokamilisha ngwe yake ya pili ya 2020-2025, naiona kabisa ile Katiba ya Wananchi, tena ile rasimu ya Warioba, ikiachwa. Amini usiamini, kufikia 2025, kuna uwezekano rais Magufuli akawa ndie the best president this nation has ever had, na msishangae kama Watanzania nchi nzima watajitokeza kuandamana kushinikiza kipengele cha ukomo wa urais kiondolewe kwenye katiba yetu, Magufuli aendelee mpaka tutakapoona tumetosheka naye kwa mazuri atakayo tutendea na kulitendea taifa letu.

Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli, hongera sana for changing for the better, utabarikiwa sana na taifa litabarikiwa.
Mungu Ibariki Rais Magufuli,
Mungu Ibariki Tanzania.
 

Msubhate

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Messages
1,056
Points
2,000

Msubhate

JF-Expert Member
Joined May 11, 2012
1,056 2,000
Wapinzani wameona mbali mno maana katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020 wapinzani walikuwa wanapoteza majimbo yao yote mbele ya CCM...

Kwa upande wangu naona CHADEMA wameangalia ugali wao mezani, na ni ya kutafuta suluhu kwa Mh. Rais ni janja yao ili chama kiendelee kubaki maana baada ya uchaguzi chadema ndio ilikuwa inakufa rasmi...

Kwa huruma ya Mh. Rais naona wataachiwa baadhi ya majimbo ili waendelee kuwepo bungeni...

Mungu Mubariki Mh. Raisi JPM

Mungu Ibariki Tanzania

Amina..
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,230
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,230 2,000
Wapinzani wameona mbali mno maana katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020 wapinzani walikuwa wanapoteza majimbo yao yote mbele ya CCM...

Kwa upande wangu naona CHADEMA wameangalia ugali wao mezani, na ni ya kutafuta suluhu kwa Mh. Rais ni janja yao ili chama kiendelee kubaki maana baada ya uchaguzi chadema ndio ilikuwa inakufa rasmi...

Kwa huruma ya Mh. Rais naona wataachiwa baadhi ya majimbo ili waendelee kuwepo bungeni...

Mungu Mubariki Mh. Raisi JPM

Mungu Ibariki Tanzania

Amina..
Nadhani ww umedhibitisha kile kilio chetu kuwa huwa kuna wizi wa kura, na wale wanaotangazwa washindi wengi kutoka ccm huwa hawashindi bali hutangazwa washindi, ndio maana unasema kwa huruma ya rais wapinzani wataachiwa baadhi ya majimbo. Kama rais ndio huwa anatoa huruma ya watu kuwa wabunge, huwa mnatumia fedha za umma kwa uchaguzi ili iwe nini?
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,230
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,230 2,000
Binafsi nisingekubali Raisi Magufuli akubali kushirikiana na chadema kama iko na Tundu Lisu, kwanza wamtose Tundu Lisu kama precondition hata ya kukaa meza moja, hakuna mtu aliyeifanyia hii nchi damage kuanzia kuanzishwa kwake labda kama Tundu Lisu,...
Tundu lissu hahitaji fadhila ya cdm wala ya rais ili kuendeleza maisha yake. Labda uje na sharti jingine.
 

Chikwuemeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Messages
10,647
Points
2,000

Chikwuemeka

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2018
10,647 2,000
Tz ni yetu sote, kutofautiana hata kwenye familia kupo ila kwasababu sisi wote ni watz inafikia mahala lazima kuweka mbali tofauti zetu.

Angalizo: awamu hii viongozi wengi hasa wateule wa Rais wanawaona wapinzani (ambao mm nawaita watu wenye mawazo mbadala kwa ktk ujenzi wa taifa) kana kwambani watu wabaya,jambo ambalo Si kweli.Mawaziri,RC,DC na wengine wamechangia sana kuleta migawanyiko isiyo na tija ktk taifa letu,hasa kwa matamko yao yasiyo na afya kwa Taifa
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,230
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,230 2,000
Je hili tukio limewapendeza pia wafurukutwa wa CCM akina Le mutuz na wale akina Godbless Lema wa upinzani?!
Halijatupendeza wengi maana tunajua Magu sio mtu wa hayo maridhiano na ni mrahihisi kutumia hali hiyo kuhadaa umma na dunia kuwa ni mtu mwema. Kwa maneno marahisi Mbowe kaenda kujidhalilisha na kutoa pointi za mezani kwa Magu.
 

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Messages
3,398
Points
2,000

kizaizai

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2010
3,398 2,000
Kwa kazi anayofanya Mh. Rais ni vyema vyama vya upinzani vikamuunga mkono, hakuna haja tena ya kukosoana nchi inaenda vizuri...
Kukosoana kukopalepale, malengo ya kukosoa ni kurekebisa pale ulipokosea. Hakuna binadamu asiye kosea. Ukikosoa leta maboresho.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,230
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,230 2,000
Wapinzani akina Mbowe wana njaa, kila siku wanatamani tuuane ili wachukue nchi, kila siku wana muomvea rais mabaya ili wafurahi, hakuna wapinzani Tanzania ila waovu tu wachumia tumbo
Umeishiwa na hoja, wanaotoka na mabox ya kura vituoni tunawaona kwa macho yetu. Huenda kwako rais ni Mungu hivyo unaamini anapaswa kusujudiwa. Ww baki kuonyeshwa jinsi makomandoo wanavyoweza kumuokoa mtu maarufu, huku Mo alitekwa na hao makomandoo hawakumuokoa. Tetea upuuzi kwa kuwachafua hao akina Mbowe kwa propaganda za kizee.
 

Forum statistics

Threads 1,379,890
Members 525,596
Posts 33,760,151
Top