Trend Reading: Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Tulway Sumaye, Yuko Njiani Kurejea Nyumbani CCM?. Asiporejea Ampokee Mbowe Uenyekiti!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,550
Wanabodi,
Mimi ni miongoni mwa members humu niliyejibainisha ni trend Reader mzuri. Kusoma trends sio utabiri bali ni kusoma mielekeo.

Trend ya leo ni maandalizi ya mwisho mwisho ya Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tulway Sumaye kurejea nyumbani CCM .

Trend hii ni kufuatia kuotazama na kuisikiliza program hii.


Trend hii ni kufuatia kurejea nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu mwingine, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa.

Kwanza Lowassa aliomba kumuona rais Magufuli, bila kuwaeleza Chadema nia yake hiyo akidhani mkutano wake na
Magufuli ungekuwa discreet.

Baada tuu ya Lowassa kutinga Ikulu na kuonana na Rais Magufuli, Chadema walikuja juu, Lowassa akajifanya yeye ndie aliitwa na Magufuli na hakujua
ameitiwa nini na kudai Magufuli alimuita Lowassa ili kumuomba kurejea CCM.
Ili kuwazuga Chadema mimi niliuliza humu


Ndipo nikamshauri Lowassa kabla hajarejea CCM afanye hivi

Baada ya sarakasi hizi, Lowassa alirejea rasmi CCM. Sasa tusubirie sarakasi za Sumaye.

Sasa ni zamu ya Frederick Sumaye, ameomba kumuona Magufuli na Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli ameisha mkubalia bado tuu kumpangia siku.Swa

Kwa sababu Lowassa alishtuliza, Sumaye hatashtukiza. Jee wana Chadema mnataarifa kuwa Mhe. Sumaye anamtafuta Magufuli?.

Sio kila trends ni lazima zitokee, inawezekana kabisa Sumaye akawa ni mpinzani wa kweli na anachomtafutia rais Magufuli ni ili kuimarisha upinzani kwa kumkabili na kumueleza rais Magufuli kuwa nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba, haki ya mikutano ya siasa ni haki ya kikatiba, haiwezekani rais Magufuli aliyechaguliwa kwa mujibu wa katiba na kuapa kuilinda na kuitetea katiba halafu yeye huyo huyo akawa wa kwanza kuisigina katiba.

Kama hii ndio lengo la Sumaye kumtafuta rais Magufuli, then huyu ni mpinzani wa kweli mwenye nia njema, thabiti na ya kweli kuimarisha upinzani.

This being the case, then the only deserving position kwa Sumaye ndani ya Chadema ni kumpokea Mhe. Mbowe uenyekiti wa Chadema.

Jumamosi Njema.
Paskali
Rejea za Trends za Paskali






 
Pascal Mayalla

Ukiwa "UNBIASED" hua unatabiri, kuelezea, kuchambua na kupendekeza mambo ambayo kwa asilimia 95% kama sio 100% hutokea na huwa sahihi. Mfano: Makala zako ulizowahi kuandika kama ya Mh Bashe, Lowassa na Sekta za Habari kukandamizwa (No doubt ulipigilia msumari kwenye vichwa vya watu, na yalitokea ulioandika tukashuhudia).

Hili pia uliowashauri CHADEMA, kama watasikiliza ushauri wako na kumwachia Mh Fredrick Sumaye "KITI" cha kumrithi Mh Freeman Mbowe. Watakua wamefanya maamuzi sahihi kwa 100% na yatakayosaidia wasiyumbe uchaguzi ujao.

Ila at times "UKIWA BIASED" watu wanafikia hatua kuamini unatafuta "CHEO" kwenye serikali hii.
 
Lolote linawezekana kwa sasa, lisilowezekana ni Bashite kutumbuliwa, hata akitumbuliwa itakuwa ni kwa makubaliano maalum.
So, just chill

Zungumzia Chama chenu kushindwa kujiendesha na kujinasibu mnaishia tu kuichongea nchi yenu mnapoishi,mnataka nn kama sio shali na machafuko ambayo hayatawakumba wanaccm tu ata nyinyi mtakuwemo.
Makonda tuachieni sisi tunajua wapi pa kumshurutisha.
 
Hakuna mwanaccm au aliyewahi kuwa mwanaccm anaweza siasa za upinzani, hasa siasa hizi za Magufuli zenye chuki za wazi za kiitikadi.

Sio Sumaye tu, hata Nyalandu ni kama anakusanya mizigo yake tayari kwa kurudi kwenye siasa za mbeleko.

Kwa hili wakulaumiwa ni Mbowe na viongozi wenzake kuwapokea hao wanaCCM na kuwapa nafasi, wakati inafahamika wazi wanaccm wengi hawawezi siasa bila mbeleko ya vyombo vya dola.

Sumaye aondoke haraka cdm maana hana lolote jipya, kwani umri wake ni wa kulea wajukuu, na hata ujana wake hakuwahi kufanya siasa za kashikashi zaidi ya kubebwa.
 
Sasa Paskali, hata bado hujaiona 'trend' ya views and comments ya huu uzi,tayari umeshaubatiza trend reading! Anyways hiyo video imenikera sana especially hapo mwishoni mwishoni, eti utaratibu uliharibika!

mbunge anaenda kutukana kwenye jimbo jingine, Halafu Mwinyi anatikisa kichwa kwa namna ya kukubali! hakuna katiba wala sheria yoyote inayozuia mtu kwenda jimbo lolote kutoa hotuba, kama ni matusi sheria iko wazi! Watanzania tuache unafiki!

Huyo mtu aambiwe ukweli,hizi decree zake ni kinyume na katiba.
 
Hata kuwa wa kwanza kurudi CCM alipokuwa na wala hata kuwa wa mwisho!

Kama ilivyo watatoka wengine CCM na kwenda upinzani!

Hiyo ndio siasa!

Kila la heri kwa maamuzi atakayoona yanafaa!
 
Back
Top Bottom