Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Bandiko hili ni angalizo nililitoa kitambo, kuwa wanaohamia CCM wasibezwe!. Makamanda waliokuwa Chadema na kuhamia CCM sasa ndio wanakwenda kuwa mwiba kwa upinzani
P
Mabibi na mabwana, heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wahenga walisema staajabu ya Mussa lakini siyo ya Firauni.

Je, huyu si ndiye aliyemtuhumu jiwe kununua wabunge?

View attachment 1575679
Ama kweli staajabu ya Mussa!
Endelea kustaajabu, kwa taarifa tuu na kukusaidia, Joshua Nasari, amejitambua na kuchukua hatua kwa kujiunga na the best party in Tanzania!.
P
 
Hii kitu bado kinaendelea akili kwa pascal au umebadilisha mawazo ??
Mpaka tuna kila sababu zikuwadharua watu walioamia CCM, hakuna faida yeyote ile waliyopata zaida ya hasara.
Tukianza na wabunge wote walioama, kila mtu anajua wajumbe waliwafanya nini na hata hao ambao walifanikiwa kupita kwa kubebebwa na JPM bado hali zao siyo za kujivunia kama wanauhakika wakushinda kula kwenye uchaguzi huu.
Kwa mtazamo wangu naona chadema imekuwa na nguvu zaidi, na CCM imefanya funzo kubwa sana kwa vijana wenye tamaa na uchu wa madaraka, matumaini yangu uchaguzi zijazo viongozi wateule hawatakuwa teyari kuunga juhudi tena.

pascal upo kimya sana kwenye uchaguzi huu, au ndio umeamua kukata mkia wako ili kusubiri nafasi za vitu maalum kama mzee akishinda? Mzee hatashida kaka, wewe endelea kuwa huru na bora ujipendekeze kwa chadema sasa kwani wanao uhakika wa kuchukua dola hapa 28 OCTOBER.
 
Wanabodi.

Wapinzani poleni sana!, CCM hongereni sana kwa ushindi huu, na hongereni kubwa in advance kwa chaguzi nyingine ndogo zitakazofuatia, na hongera kubwa zaidi in advance ni hongera ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, 2019 ambapo CCM itakomba kila mtaa na kila kata, lila kitongoji na kila kijiji na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ndio yatawafungua macho, wengi, hiki kitu mimi ninachokizungumzia humu kwa sasa, na matokeo ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa Tanzania kutabadili kabisa structure ya mfumo wa vyama vingi kwa Tanzania kuwa ni nchi ya vyama vingi kwa sababu kiukweli Tanzania kuendelea kuitwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini in actual facts, Tanzania post 2020, inakwenda kuwa ni nchi ya chama kimoja!, 2020, Tunakwenda kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya chama kimoja, Tanzania ya CCM tuu and only CCM!.

Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...

Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?.
Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidemokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
 
hopeless kabisa
 
Hii kitu bado kinaendelea akili kwa pascal au umebadilisha mawazo ??
pascal upo kimya sana kwenye uchaguzi huu, au ndio umeamua kukata mkia wako ili kusubiri nafasi za vitu maalum kama mzee akishinda? Mzee hatashida kaka, wewe endelea kuwa huru na bora ujipendekeze kwa chadema sasa kwani wanao uhakika wa kuchukua dola hapa 28 OCTOBER.
Mkuu Mr.mzumbe , haya bana na tusubiri matokeo
P
 
Wanabodi.

Politics is a game of hide and seek and the changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya siasa za Tanzania ya Magufuli, wanasiasa karibu wote walioko upinzani, with very few exceptions, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends za kisiasa kwa kuangalia mwelekeo wa 2020, kwa matokeo haya, watakuwa wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa zetu za Tanzania na siasa za upinzani nchini katika kipindi hiki cha Tanzania ya Magufuli na their chances ya upinzani kushinda kata yoyote au jimbo lolote kuelekea 2020, hivyo, wenye kuona mbali, wameamua kufanya uamuz wa mapema kwa kuvihama vyama vyao sasa kwa kujiunga CCM!, ili ku secure their positions mapema badala ya kusubiri kifo hiyo 2020!

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then mtu huyo, atajiunga CCM now!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani wa kata 43 kwa jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then siasa za Tanzania kwa sasa, CCM ndio mpango mzima!, kama kuna mwanasiasa yoyote, au wowote, wanataka future ya politics ambao politics kwao sio past time baada ya kustaafu, au wito wa utumishi wa umma, bali politics kwao ni kama ajira yao ya kudumu na kukamata ulaji, kujitafunia keki ya taifa, chama cha kujiunga nacho ni CCM pekee!.

Hapa nazungumzia ukweli halisi wa kitu kilichopo, ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho tuu, ya kitu kilichotokea, ambacho ndicho kilichopo, ni CCM imeshinda!, bila kujalisha imeshindaje au imeshinda kwa mbinu gani, ziwe ni mbinu halali au haramu, CCM imeshinda kihalali kwa kufanya siasa safi, au kiharamu kwa kubebwa na wasimamizi wa uchaguzi, au upinzani umeshindwa kihalali kutokana na udhaifu wa kukosekana upinzani imara, ama upinzani umechezewa faulo za waziwazi, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho ya mshindi ni nani.

Aliyetangazwa mshindi ndiye aliyeshinda, na mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, the looser standing small, aliyeshinda kashinda, ndiye mshindi na ni mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justify the means".

Wapinzani poleni sana!, CCM hongereni sana kwa ushindi huu, na hongereni kubwa in advance kwa chaguzi nyingine ndogo zitakazofuatia, na hongera kubwa zaidi in advance ni hongera ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, 2019 ambapo CCM itakomba kila mtaa na kila kata, lila kitongoji na kila kijiji na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ndio yatawafungua macho, wengi, hiki kitu mimi ninachokizungumzia humu kwa sasa, na matokeo ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa Tanzania kutabadili kabisa structure ya mfumo wa vyama vingi kwa Tanzania kuwa ni nchi ya vyama vingi kwa sababu kiukweli Tanzania kuendelea kuitwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini in actual facts, Tanzania post 2020, inakwenda kuwa ni nchi ya chama kimoja!, 2020, Tunakwenda kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya chama kimoja, Tanzania ya CCM tuu and only CCM!.

Hongera sana rais Magufuli kuturudishia Tanzania ya Nyerere kwa kuirudisha Tanzania yetu kuwa ni nchi ya chama kimoja cha siasa, CCM, hivyo baada ya 2020 kwa Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja, (vyama vingi vina kelele nyingi), kazi itabaki ni moja tuu, kuleta maendeleo na tutapata maendeleo kama China. China ni nchi ya chama kimoja cha siasa na ina maendeleo makubwa, na sasa ndio inaelekea kutawala uchumi wa dunia, na sisi Tanzania we can follow its foot steps, tuna kila kitu cha kutuwezesha kutawala uchumi wa Africa Mashariki, uchumi wa SADC na uchumi wa Bara la Africa.

Viva Magufuli
Viva Tanzania
Mungu Ibariki Tanzania.

Jumatatu Njema.

Paskali
Sina uhakika wangapi humu walisoma hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
 
Sina uhakika wangapi humu walisima hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
Hili ni la wazi lakini uwezo wa Magufuli kuipeleka Tanzania level za China ni wa kutilia shaka. Yuko busy kujenga misingi ya kulinda siasa za CCM na si kujenga mifumo ya kazi ambayo China imewapaisha. Uzalishaji mdogo na uchumi mdogo utaturudisha kuhitaji mbadala unless mrithi wake aboreshe hiyo sehemu.

Kwa sababu hii pia siasa za upinzani za matembezi na kutegemea msaada nje zitajifia. Na wale wapinzani maarufu wa tangu 1995 hii ni mara ya mwisho kwao kimantiki.
Endapo kutaibuka sura mpya za wahanga wa mfumo huu, nazungumzia kizazi ambacho wana miaka 25-35 kwa sasa zinaweza kubadilisha trend za 2025.
Pamoja na kushindwa upinzani bado wana karibu nusu ya kura halisia.

Pamoja na hayo, sisi bado tunategemea upepo wa dunia na Afrika. Ikiendelea huko kwingine hali basi fikra zake zitadumu.

Pia endapo akiweza kuweka mifumo ya kazi ambayo itatuhakikishia fursa za maisha bila kujihusisha na siasa basi atakuwa amefanikisha ndoto yake ya kuelekea China.
 
Sina uhakika wangapi humu walisima hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
Nimekusoma mkuu..kwa hiyo tutegemee maendeleo ya kiwango cha juu sio? Kuna haja hata ya kufuatilia bunge lijalo? Kama ndivyo tutakua tunafuatilia nini?
 
Pia endapo akiweza kuweka mifumo ya kazi ambayo itatuhakikishia fursa za maisha bila kujihusisha na siasa basi atakuwa amefanikisha ndoto yake ya kuelekea China.
Mkuu double R , kwanza asante kwa objectivity yako, hili la kujenga mifumo, systems, naungana na wewe asilimia 100% kwa 100%. Mimi pia niliwahi kulizungumzia hapa,
P
 
Kaka pascal ni ngumu sana kwa CCM kurudisha majimbo yote

Hali ya CCM ni mbaya sana, na Pamoja na Jitihada za Mtukufu Rais kumbambana na Ufisadi, Rushwa nk, lakini nachelea kusema kuwa HAKUBALIKI, sio ndani wala nje ya CCM, kwa jitihada alizozifanya mtukufu raisi ule uchaguzi wa madiwani wala CCM wasingefanya kampeni, lakini matokeo yake nguvu kubwa sana imetumika
Kwa nini nasema ni Vigumu CCM kurudisha majinbo
1: Mtukufu Rais itambidi apambane sana na Hali yake, uoinzani kutoka chamani na nje, so hatakiwa na muda wa kuwaangalia watu wa chini kama aliokuwa nao sasa
2: uchaguzi wa Zanzibar, msimu uliopita Lowassa aliwababaisha sana ikafikia kipindi wakaisahau Zanzibar na hatimae Hamad akajitangaza Mshindi (Asante Jecha), so uchaguzi ujao CCM hawawezi kamwe kuisahau Zanzibar
3: Chadema sasa ina Wapenzi wa chama waliopo Royal kwa kiasi fulani, na tunalipima hilo kwa sababu pamoja na kuondoka kwa Zitto, Slaa nk, bado Chadema iliweza kujikusanyia Wabunge wengi zaidi, na Madiwani wengi mpaka kupelekea kushika baadhi ya Halmashauri kwenye miji mikubwa
Mkuu Kituko , hapa ni katika kukumbushana tuu, hoja hii niliirudia hapa
Naamini umeona kilichotokea!.

P
 
Back
Top Bottom