Trend Reading, Taifa Stars Kualikwa Ikulu Kupongezwa. Ushindi Huu Ni Dalili Njema Kwa Rais Magufuli. Please Don't Politicise!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,
Declaration of Interest
Kufuatia kukaza kwa vyuma, ile nusu bei leo imetuwezesha sisi baadhi yenu tuliofulia, angalau kupumua kwa kupata kanguvu kidogo angalau kuweza kuamka na kujikongoja kwa kutembea na Joni Mtembezi, hivyo ikitokea ukajiona kama bandiko hili hulielewi elewi, nisamehe bure, ni mambo tuu ya nusu bei, hivyoi hili ni bandiko la Siasa za michezo, siasa za ushindi kwa kutumia a collective will powers.

Angalizo.
Naomba kuanza na angalizo. Kama wewe ni miongoni mwa wale wenye allergies na mafanikio yoyote ya rais Magufuli na awamu ya tano, hivyo alipongezwa, wewe unakasirika, then nakushauri bora uishie hapa ili tusiharibiane siku, kwa sasa taifa liko kwenye a happy mood kutokana na ushindi wa taifa Stars, hivyo naombeni msilete frustrations zenu mkatuharibia mood zile nusu bei zikakata.

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu kuipongeza Timu yetu ya Taifa, Taifa Stars kututoa kimasomaso, hongereni sana!, naomba ushindi huu usiwe ni nguvu ya soda ukaishia kuwa ushindi wa ngama!.

Najua kupitia kitu kinachoitwa Trend Reading, Timu yetu ya Taifa Stars, soon Itaaalikwa Ikulu ili kupongezwa na rais kwa ushindi huu. Ushindi huu ni dalili njema ya kung'aa kwa nyota ya Rais Magufuli, kuirudisha Tanzania kwenye ramani ya kimataifa katika medani za michezo kiAfrica na kimataifa.

Naombeni kutoa angalizo, katika pongezi hizo, ushindi huo utawianishwa na mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM upande wa sera ya michezo kama ilivyo ainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM, rais Magufuli apongezwe kwa mafanikio haya kama ilivyo ada all credits zienda kwa Baba kwa jinsi ile ile ya mkubwa ni jalala, lakini nawaomba sana, don't politicise it. Tusipoliticise kila kitu for political mileage, tuanze kujenga utamaduni wa kutukuza utaifa bila kuingiza politics kwenye maslahi ya taifa, tuweke pembeni siasa na tofauti zetu zote Tutangulize utaifa wetu, umoja wetu na Utanzania wetu.

Somo la Ushindi
Siri ya ushindi wa leo ni the collective will powers za Watanzania wote wa vyama vyote kudhamiria Tanzania ishinde, dhamira hiyo ikatengeneza nguvu ya will ya ushindi collectively toka kwa Watanzania wote kutokana na kuhamasishwa, hivyo ikajenga a strong momentum na kutuletea ushindi.

Upendo, amani, umoja na maendeleo pia yakihamashishwa hivi tukaweka a collective will powers za kuleta maendeleo, tutapata maendeleo na tutaendelea!

Ukitokea ni kweli vyama vingi winatuletea migogoro na kuchelewesha maendeleo, Watanzania tukihamashishwa katika umoja wetu, na zikatolewa hoja za msingi za kuvikataa vyama vingi, Watanzania watavikataa vyama vingi na kuichagua CCM pekee, vyama vya upinzani vinakufa, na uchaguzi wa 2020 tunaichagua tuu CCM pekee, tunarejea kwenye nchi ya chama kimoja, tunapata maendeleo tarajiwa.

Lakini pia kama ni kweli chanzo umasikini huu wa Tanzania ni sera mbovu za CCM, chanzo cha rushwa na ufisadi ni CCM, Watanzania wakihamasishwa kwa kuelimishwa jinsi CCM ilivyo lilidimiza taifa hili na kuonyeshwa mifano ya nchi tulizopata nazo uhuru huku zikiwa nchi hizo zikiwa hazina kitu kabisa kulinganisha na sisi tuliokuwa na kila kitu, tukaonyeshwa nchi hizo sasa hivi ziko wapi, halafu ukilinganisha na sisi Tanzania tulipo licha ya rasilimali lukuki tulizo nazo, Watanzania katika umoja wetu tukihamasika kusema, enough is enough, amini usiamini, CCM, inakwenda!

Ila Tanzania tuna tatizo jingine kubwa, hata tukihamasika kuipiga chini CCM ikaanguka, then tunaichagua nini au nani?. Kiukweli kabisa kwa siasa zetu hapa tulipo, bado CCM haina mbadala, hivyo hata Watanzania tukiamua kusema no na kudhamiria kuipiga chini CCM, mazingira ya kutokuwepo mbadaka, kunaturudisha kule kule kwenye CCM ni zimwi likujualo. Ni hapo tuu!

The central message hapa ni sisi Watanzania wote tukidhamiria kwa dhati na tukiamua kwa pamoja collectively ku wish kushinda tunashinda!

Hongereni Watanzania ku I will Taifa Star ishinde ikashinda, tusiishie kwenye michezo, twende kwenye uchumi, social services na kumalizia kwenye siasa

Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Update:
Tukio hili, limethibitishwa kutokea leo saa kuanzia saa 4:00, Timu ya Taifa Stars na Kamati ya uhamasishaji, wamealikwa lunch ikulu, tukio hili litatangazwa mubashara na TBC1 na TBC Taifa.
P.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la Siasa za michezo,

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu kuipongeza Timu yetu ya Taifa, Taifa Stars kututoa kimasomaso, hongereni sana.

Najua kupitia kitu kinachoitwa Trend Reading, Timu yetu ya Taifa Stars, soon Itaaalikwa Ikulu ili Kupongezwa na rais kwa . Ushindi Huu. Hii ni Dalili Njema ya kungaa kwa nyota ya Rais Magufuli, kuirudisha ramani ya Tanzania katika medani za michezo kimataifa, na katika pongezi hizo, ushindi huo utawianishwa na mafanikio ya utekelezaji sera ya michezo kama ilivyo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM, rais Magufuli apongezwe kwa mafanikio haya kama ilivyo ada all credits zienda kwa Baba kwa jinsi ile ile ya mkubwa ni jalala, lakini nawaomba Sana, Don't Politicise it. Tusipoliticise kila kitu for political mileage, Tuanze utamaduni wa utaifa, kwenye maslahi ya taifa, tuweke pembeni siasa na tofauti zetu zote Tutangulize utaifa wetu, umoja wetu na Utanzania wetu

Somo la Ushindi
Siri ya ushindi wa leo the powers of will ya ushindi collectively toka kwa Watanzania wote kutokana na kuhamasishwa, hivyo ikajenga a strong momentum na kutuketea ushindi.

Upendo, amani, umoja na maendeleo pia yakihanashishwa hivi tukaweka a collective will powers za kuleta maendeleo, tutaendelea .

Ukitokea ni kweli Vyama Vingi winatuletea migogoro na kuchelewesha maendeleo, Watanzania tukihamashishwa kuvikataa na kuichagua CCM pekee, vinakufa.

Lakini pia kama chanzo
Unajaribu kufananisha Ushindi wa Starz na MUUNGANO na mshikamano wa Taifa Hili?

Ukitoka huko DCA kwenye free/½ of charge nadhani utajuta kuandika huu utumbo.

Kuna tofauti kubwa Kati ya
Mpira na SIASA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Please don’t politicise and then ushindi huu ni dalili njema kwa kichaa!? Kwanini usiandike ushindi huu ni dalili njema kwa Tanzania katika sekta ya michezo?

Umoja wa Kitaifa ni pale Taifa Stars inaposhinda tu?

Kwanini tusiwe na umoja wa kitaifa kwenye kila issue ikiwemo wizi, ufisadi, uminyaji wa demokrasi nchini, kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge, kudharau katiba, mahakama na sheria za nchi? 😳

Wanabodi,
Hili ni bandiko la Siasa za michezo,

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu kuipongeza Timu yetu ya Taifa, Taifa Stars kututoa kimasomaso, hongereni sana.

Najua kupitia kitu kinachoitwa Trend Reading, Timu yetu ya Taifa Stars, soon Itaaalikwa Ikulu ili Kupongezwa na rais kwa . Ushindi Huu. Hii ni Dalili Njema ya kungaa kwa nyota ya Rais Magufuli, kuirudisha ramani ya Tanzania katika medani za michezo kimataifa, na katika pongezi hizo, ushindi huo utawianishwa na mafanikio ya utekelezaji sera ya michezo kama ilivyo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM, rais Magufuli apongezwe kwa mafanikio haya kama ilivyo ada all credits zienda kwa Baba kwa jinsi ile ile ya mkubwa ni jalala, lakini nawaomba Sana, Don't Politicise it. Tusipoliticise kila kitu for political mileage, Tuanze utamaduni wa utaifa, kwenye maslahi ya taifa, tuweke pembeni siasa na tofauti zetu zote Tutangulize utaifa wetu, umoja wetu na Utanzania wetu

Somo la Ushindi
Siri ya ushindi wa leo the powers of will ya ushindi collectively toka kwa Watanzania wote kutokana na kuhamasishwa, hivyo ikajenga a strong momentum na kutuketea ushindi.

Upendo, amani, umoja na maendeleo pia yakihanashishwa hivi tukaweka a collective will powers za kuleta maendeleo, tutaendelea .

Ukitokea ni kweli Vyama Vingi winatuletea migogoro na kuchelewesha maendeleo, Watanzania tukihamashishwa kuvikataa na kuichagua CCM pekee, vinakufa.

Lakini pia kama chanzo
 
Please don’t politicise and then ushindi huu ni dalili njema kwa kichaa!? Kwanini usiandike ushindi huu ni dalili njema kwa Tanzania katika sekta ya michezo?

Umoja wa Kitaifa ni pale Taifa Stars inaposhinda tu?

Kwanini tusiwe na umoja wa kitaifa kwenye kila issue ikiwemo wizi, ufisadi, uminyaji wa demokrasi nchini, kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge, kudharau katiba, mahakama na sheria za nchi? 😳
Hivi mkuu BAK viongozi wakuu wa serikali ya Tanzania kuanzia enzi za Nyerere walikufanyia nini?

Maana huwa unawa bull shit kila Mara mkuu, lakin ni haki yako kikatiba, saw a lakin hata ushindi wetu wa Taifa Stars ujafurahia?
 
Please don’t politicise and then ushindi huu ni dalili njema kwa kichaa!? Kwanini usiandike ushindi huu ni dalili njema kwa Tanzania katika sekta ya michezo?

Umoja wa Kitaifa ni pale Taifa Stars inaposhinda tu?

Kwanini tusiwe na umoja wa kitaifa kwenye kila issue ikiwemo wizi, ufisadi, uminyaji wa demokrasi nchini, kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge, kudharau katiba, mahakama na sheria za nchi?
Humu jamii forum nimegundua kitu kimoja yaani kuna watu muda wote wanataka uandike masuala ya kuitukana Serikali bila sababu ndo furaha yao na utapongezwa sana,Lakini unapoandika upande wa pili kwa yale mazuri na ya msingi basi utaoga matusi sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli kwenye mabaya na mazuri na ndiyo sababu katiba ya nchi ina kipengele cha kuwapa raia haki na uhuru wa kuikosoa Serikali na watendaji wake wakati wowote ule. Miaka 58 ya uhuru nchi yenye utajiri mkubwa sana wa rasilimali lakini hatuna kimoja cha kujivunia ni wizi, ufisadi na kusaini mikataba mibovu huku wakikingiana vifua sheria isichukue mkondo wake. Tia akili kichwani.

Humu jamii forum nimegundua kitu kimoja yaani kuna watu muda wote wanataka uandike masuala ya kuitukana Serikali bila sababu ndo furaha yao na utapongezwa sana,Lakini unapoandika upande wa pili kwa yale mazuri na ya msingi basi utaoga matusi sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni katika hali hii hii ya nusu bei ninapojiuliza Mr. Makonda amekuwa ha pesa nyingi kiasi hiki lili? kwa biashara gani? manake milioni kumi kumi ni total ya milioni 220 when did Makonda make all these money and how?? ni sawa tu linalotokana na nusu bei
 
Utakuwa mjinga wa mwisho kufikiri eti, star's wameshinda kwa juhudi za awamu ya tano.
Hivi P. ulikuwa na miaka mingapi mara ya mwisho stars iposhiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza?. Mbona wazee wetu hawasemi zilikuwa ni juhudi za Mwl. Nyerere?
Mwinyi alianzisha hii safari, Mkapa akafanya mabadiliko kimtizamo wake, lakini safari ilikuwa inaendelea na naamini Kikwete aliongeza speed ya michezo Tz, hadi kuwa na unafuu kwenye kodi za vifaa vya michezo kuingizwa Nchini, na kuandaa vipaji ambavyo ni stars ya leo. Hadi real Madrid tuliwaona Bongo, na star's walipewa heshima ya kuitembelea Bunge na Ikulu pia kipindi cha Kikwete si ndo walipewa na nyumba kabisa....
Maraisi wote waliotangulia walianzisha hii safari na waliwekeza kwenye michezo. Sasa hii ya JPM na taifa star's vipi?
Itakuwa ni miujiza miaka mitatu unawazidi walitengeneza njia zaidi ya miaka 35.!

Nimalizie kwa kusema, ni ujinga kuiombea star's ishindwe, kisa kamati ya Bashite Wema sijui nani. Lakini pia ni ulimbukeni uliopitiliza kushawishiwa na watu kama hawa ili star's ishinde. Mmoja, madawa mwingine vyeti, hawana si good rolle model kwenye jamii inayojadiri maadili kila siku.

Kama Mtanzania unayejitambua, huhitaji kuhamasishwa, bali jihamasishe mwenye kwa ushindi wa Nchi yako, mafanikio ya Nchi yako, fundisha upendo wa Nchi yako kwa utakaowaacha walio chini yako.
 
Please don’t politicise and then ushindi huu ni dalili njema kwa kichaa!? Kwanini usiandike ushindi huu ni dalili njema kwa Tanzania katika sekta ya michezo?

Umoja wa Kitaifa ni pale Taifa Stars inaposhinda tu?

Kwanini tusiwe na umoja wa kitaifa kwenye kila issue ikiwemo wizi, ufisadi, uminyaji wa demokrasi nchini, kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge, kudharau katiba, mahakama na sheria za nchi? 😳
Kwanini usiandike ushindi huu ni dalili njema kwa Tanzania katika sekta ya michezo? Add........Chini ya Raisi Magufuli
 
Bashite au Wema hawana maadili katika jamii hivyo hawezi hamasisha MTU mwenye akili timamu. Ushindi huu ni coincidence tu. Na mipango ya nje ya uwanja.

Hakuna awamu hii ilipowdkeza kwenye ushindi huu, kama mnababisha tutaona huko mbele,

furaha ya pombe za Bure isiwatoe akili
 
Back
Top Bottom