Trend Reading: Salum Mwalimu, Mb. Mtarajiwa, Kinondoni!. Hata Wana CCM Wasioendekeza Ujinga, Watamchagua!. | Page 25 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trend Reading: Salum Mwalimu, Mb. Mtarajiwa, Kinondoni!. Hata Wana CCM Wasioendekeza Ujinga, Watamchagua!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Jan 19, 2018.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,643
  Likes Received: 23,839
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Declaration of Interest
  Naomba nianze kwanza kwa kudeclare interest, kuwa mimi Pascal Mayalla ni mkaazi wa Wilaya wa Kinondoni, kama mwananchi wa kawaida, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, na hili bandiko, sio la kumpigia debe mgombea yeyote, bali as good citizen of this nation, ukiona mtu yoyote au chama chochote, kinatuleta ujinga Watanzania, sisi Watanzania wenzenu ambao sio wajinga, na tumejaaliwa kauwezo hata kadogo tuu cha kuubaini ujinga tunaotaka kuletewa, then we have a duty of care, (tuna wajibu) wa kuwasaidia wenzetu wengine ambao ni less fortunate, kuwaelimisha kuhusu ujinga huo, na tuna jukumu la kuwahamasisha wenzetu, wasikubali kufanywa wajinga kwa kuletewa ujinga na bado wakachagua ujinga huo.

  Tanzania Tuna Mapungufu Makubwa Katika Uelimishaji Elimu ya Uraia, Hivyo Kila Tunafanywa Wajinga kwa Kuletewa Ujinga na Kuchagua Ujinga!.
  Watanzania wazalendo wa kweli, ni wale wenye moyo wa dhati wa kuwasaidia wenzao kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha, wasikubali kufanywa wajinga, kwa kuukataa ujinga!. Wewe ukiwa ni mzalendo, ukaona chama fulani kinataka kuwaletea wananchi ujinga, hupaswi kunyamazia kimya ujinga huu, bali una wajibu wa kuwaelimisha wengine kuwa hiki mnacholetewa na chama fulani, ni ujinga, hivyo kuwaelimisha na kuwahamasisha, wasikubali kufanywa wajinga kwa kuletewa ujinga na chama chochote cha siasa, na wao kuukubali ujinga huo, kuukumbatia na kuchagua chaguo la ujinga huo.

  Wanaoletwa Ujinga na Kuchagua Ujinga Huo Bila Kujua Wanachagua Ujinga, ni Watu wa Kuhurumiwa na Kuelimishwa.
  Watu wenye kauli ya mwisho, wamchague nani katika uchaguzi wowote, ni wananchi wa eneo husika, ikitokea wananchi wa eneo fulani, wameletewa ujinga bila wao kujua walicholetewa ni ujinga, hivyo kujikuta wamechagua ujinga!. Watu wa aina hii, wanaoletewa ujinga na kuuchagua ujinga huo bila kujua kuwa wanachagua ujinga, ni watu wa kuhurumiwa na wanachohitaji ni kusaidiwa kwa kuelimishwa ili wasiendelee kufanywa wajinga, kwa kuletewa ujinga na kuuchagua ujinga huo!.

  Wanaoletewa Ujinga, Na Kuelimishwa Wameletewa Ujinga, Lakini Bado Wakachagua Ujinga, Ni Wajinga Kuliko Waliowaletea Ujinga!. Jee Wanakinondoni ni Wajinga Kuliko?.
  Ukiletewa ujinga, na ukapatiwa fursa ya kuelimishwa kuwa hiki ulicholetewa ni ujinga, lakini bado ukawa radhi kuuchagua huo ujinga kwa ridhaa yako mwenyewe, utakuwa umefanya informed decision kwa kuukubali ujinga huo, hivyo watu wa aina hii, watakuwa ni watu wajinga kuliko hata aliyewaletea ujinga|!. Swali linabaki kwa Wana Kinondoni, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga?, Wanaweza kuletewa ujinga na wakauchagua huo ujinga?.
  Hivyo hili ni bandiko elimishi, kuwaelimisha wana Kinondoni, ujinga wanaoletewa na CCM, ili mwisho wa siku, hata kama wataamua kuchagua ujinga, tutakuwa tunawajua ni watu wa aina gani kwa sababu angalau, walipata fursa ya kuelimishwa kabla!.

  Jee Watanzania ni Mazuzu?. Tunaweza Kuletewa Ujinga na Kuuchagua Tuu Ujinga Huo Kama Mazuzu?.
  Bandiko hili ni bandiko elimishi la muendelezo wa ile hoja yangu kuwa Watanzania kwa muda mrefu tumekuwa tukifanywa mazuzu na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kwa kutuletea ujinga, na wanasiasa wajinga, just to take us for granted kuwa kwa vile ni chama kikubwa, kinapesa sana, kinapendwa sana, na kinakubalika sana, hata kikileta ujinga wa aina gani, ujinga huo utapita hivyo, hivyo kujiaminisha, hata wakisimamisa jiwe, jiwe litachaguliwa!.

  Ujinga huu ndio Chama cha Mapinduzi, CCM kimewafanyia wana Kinondoni kwa kuwaletea mgombea aliyewafanyia ujinga fulani Kinondoni, licha ya ujinga huo, CCM kimewaletea tena mjinga huyo huyo na kuwataraji wana Kinondoni, watamchagua!.

  Jee Ujinga wa CCM Kinondoni ni Upi?, Jee ni Ujinga Kweli?, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga Kuchagua Ujinga?.
  Ili kuielewa hoja yangu hii kwa kina, inakubidi ujipe muda kupitia kwanza bandiko hili
  Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.
  CCM na Ujinga Uliopitiliza, Jee wana Kinondini ni Wajinga?. Ni Mazuzu?. Wanafanyiwa Ujinga, Jee Wataukubali Ujinga Huu?.
  Kiukweli kitendo kilichofanywa na CCM kuwasimamisha wabunge wale wale waliotufanyia ujinga wa kujiuzulu, na kutuingiza gharama za uchaguzi wa marudio kwa sababu za kijinga, ni ujinga uliopitiliza!.

  Hii inaamisha CCM inawaona wana Kinondoni na wana Siha kuwa ni wajinga!, yaani mtu aliyeaminiwa na wananchi, na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wao, halafu anajiuzulu kwa sababu za kijinga, kisha kugombea tena kupitia chama kingine, akitaraji atachaguliwa tena!, ikitokea ni kweli akachaguliwa, wananchi wa maeneo hayo, watakuwa ni wajinga wa kutupwa, kwa kufanywa wajinga na kuukubali ujinga huo!. Kwa sasa siwezi kuwasemea wananchi wa Siha, ila kwa vile mimi ni mkazi wa Kinondoni, na ni mpiga kura wa Kinondoni, kamwe siwezi kuukubali ujinga huu, hivyo nitawahamasisha wana Kinondoni, wanaojielewa ma kujitambua, wasiukubali ujinga huu wa CCM inaotuletea, kutaka kutufanya mazuzu!, hivyo kutoa wito kwa wana Kinondoni wote, wakiwemo wana CCM, kuutumia uchaguzi huu wa marudio, kutuma ujumbe mzito kwa Chama cha Mapinduzi, kuwa Wana Kinondoni, we might be ignorants kwa kutokujua, but we are not stupid!, nikimaanisha tunaweza kuwa tulikuwa wajinga kwa kumchagua kiongizi mjinga kwa mara ya kwanza, bila kuujua ujinga wake, lakini sisi sio mazuzu, Chama cha Mapinduzi, kututeulia mjinga huyu, halafu tuje tumchague kwa mara ya pili, tutakuwa ni ma stupid!. Ili Kinondoni kuonyesha kuwa we not stupid na hatukubali kuletewa ujinga, nahamasisha wana Kinondoni, kumchagua mgombea yoyote, kutoka chama kingine chochote but not CCM!.

  Namfahamu Mgombea wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu!, Ni Jembe la Ukweli!.
  Licha ya kukiri kuwa sina chama, lakini kunapotokea fursa ya kumbaini mtu fulani anaweza kuwa kiongozi mzuri, nami ninajukumu la kuwaelimisha wengine, uzuri wa mtu huyo, na huwa nafanya hivi hata kwa wagombea wowote wazuri wa vyama vyovyote.
  Mfano katika mchakato wa CCM, hata kabla wengi hawajajua kuwa mgombea wa CCM atakuwa ni John Pombe Magufuli, mwaka mmoja kabla Magufuli hajateuliwa na CCM, niliweka angalizo hili
  Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

  Na miongoni mwa wagombea urais wa CCM waliogombea na Magufuli, mimi pendekezo langu lilikuwa
  Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!
  na hata sasa rais wetu ni Dr. John Pombe Magufuli, hata tawala milele, muda wake utafika, naye ataondoka na watakuja wengine, hivyo baada ya kuuona utendaji wa rais Magufuli, nimetoa ushauri huu, Watanzania tusiendelee kusubiria tuu kumpata rais kwa bahati, bali tuanze mtindo wa grooming, tukimuona mtu fulani ana uwezo, tusisubiri hadi Magufuli aondoke, ndipo watu waanze kupigana vikumbo kuusaka urais, bali tumgroom
  Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?
  Huu ni uthibitisho kuwa mimi sina chama hivyo mtu akiwa ni mzuri, haijalishi ni wa chama gani, tutamuunga mkono, ndani ya CCM kuna watu wazuri, tuwaunge mkono, na pia kuna watu wa hovyo, tusiwaunge mkono, na kwenye upinzani pia kuna watu wazuri, tuwaunge mkono, na watu wa hovyo, tuwakatae!. Hivyo hata kama ningekuwa mwana CCM, hala chama change cha CCM kikatuletea mtu wa hovyo, kama huu ujinga wa Kinondoni na Siha, halafu Wapinzani wakatuletea mtu safi!, tutamchagua mgombea wa upinzani, na hiki ndicho hata Mwalimu Nyerere alichofanya Butiama ile 1995 kumsuport mgombea wa upinzani!.

  Hivyo baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naomba kwanza kukiri, mimi Pascal Mayalla, namfahamu Kijana huyu kwa karibu, alikuwa ni Mwandishi wa Habari na Mwenzangu wa Channel Ten, alipoajiriwa Channel Ten, alinikuta na nilimpokea, ni mchapa kazi hodari, hivyo kwa ujinga ambao CCM imewafanyia wana Kinondoni, naamini kabisa, hata wana CCM wanaojitambua, na wasiokubali ujinga, wakiujua wasifu wa Salum Mwalimu, watamchagua Salum Mwalimu!.

  Kinondoni, Msikubali, Kuwachagua Mala.. wa Kisiasa, Wanaohongwa Kuhama Vyama Vyao, ni Mala.. tuu kama Wale Wanawake Mala.. Wengine Wote!.
  Kitendo cha mwanasiasa kukubali kuhama chama kwa kurubuniwa, au kuahidiwa chochote, maana yake ni kukubali kuhongwa, na kuhongwa, kuko kwa aina nyingi, sio lazima kuhongwa pesa!, kuna waliohongwa ajira, kuna waliohongwa kugombea tena, kuhongwa ni kuhongwa tuu, na kitendo cha mtu yoyote kuhongwa chochote na kukubali hongo hiyo, huu ni umala.. wa kisiasa, hivyo kuna wanasiasa, wanaohama vyama vyao na kuhamia vingine, kwa ridhaa zao wenyewe, hawa hawana kosa lolote kwa sababu hii ndio demokrasia yenyewe.

  Lakini wanaohama vyama kwa kuhongwa ahadi au kushawishiwa kwa namna yoyote, na kuukubali ushawishi huo, hawa ni wanasiasa mala.. wa kisiasa!. Na kuhongwa sio lazima pesa tuu, hata kuitwa Ikulu na kuombwa kuhama chama chako. huku ni kutongozwa, ukibali ni hongo!. Thank God, Mwamba wa Kaskazini, uliitwa Ikulu na kutongozwa ahame, kwa vile yeye sio mala. wa kisiasa, mwamba huu uligoma, ila ndio uliotufungua macho kuwa kumbe kuna hongo, watu wanatongozwa, na kuhongwa, uthibitisho wa kuhongwa huku ni kupokea hongo hizo wazi wazi na kila mwenye macho, anaziona!.

  Kwa kufuata kanuni ya aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, huu ni uthibitisho jinsi viongozi wetu wenye dhamana, wanavyofanya mambo ya kujinga ya kutongoza wanasiasa na kuwahonga!.
  Kama Hiki Ndicho Lowassa Alichoitiwa Ikulu!, Then Tuna Rais wa Ajabu!, Kama ni Uongo, Lowassa Ashitakiwe Kwa Uchochezi!.
  Kwa vile tuhuma hii haijakanushwa!, then huu ndio uthibitisho wa baadhi ya wanaohama vyama, wamehongwa!.

  Jee Mtulia wa CUF Kinondoni, na Moleli wa Chadema Siha, Wamehongwa?. Hivyo ni Mala.. wa Kisiasa!.
  Jibu ni yes!, hawa wote wawili, wametongozwa!, wakahongwa na kuhongeka!, hivyo wote wawili ni mala.. wa kisiasa!. Uthibitisho kuwa wamehongwa na kuhongeka, ni kitendo cha kujitoa vyama vyao, kuwasaliti wananchi waliowachagua na kujiunga CCM, na hapo hapo kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM. Ugombea wa CCM, unapitia mchakato fulani, kitendo cha wajiuzulu hawa kujiunga CCM leo, na kuteuliwa bila mchakato rasmi wa ki CCM kufanyika, zikiwemo kura za maoni, ni uthibitisho tosha, walikubali kujiengua vyama vyao kwa ahadi za kuteuliwa tena!. Hii ni hongo na huu ni umala.. wa kisiasa!. Wana Kinondoni na Wana Siha, wasiukubali ujinga huu!.

  Paskali
   
 2. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #481
  Mar 6, 2018
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,653
  Trophy Points: 280
  Prediction algorithm kati ya 2005 mpaka 2015 kwenye chaguzi za hapa nchini ilikuwa na variables nyingi sana na loop kibao...hivyo kuwa ngumu kutumika kwa urahisi. Lakini kuanzia sasa na kuendelea. Variable zimepungua sana na loop ni chache kutokana na baadhi ya kugundulika kwa baadhi ya variables kutokuwa reliable na kukosa thamani hivyo kupelekea kuziondoa. Hii ilisaidia sana algorithm hii kuwa na loops moja tu hivyo kurahisisha matumizi yake hauhitaji kuwa na 'processor' kubwa na 'space' ku'run' aligorithm hii. Una click tu ndani ya 30ms unapata majibu. Ya mwaka 2020, majibu yake yatapatikana mapema sana yaani 2019 (mwakani).
   
 3. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #482
  Mar 6, 2018
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,653
  Trophy Points: 280
  Hakuna demokrasia isiyo na gharama. Tuheshimu uhuru wa kuamua na kufanya kwa misingi ya demokrasia. Mbunge wa zamani wa CUF alitumia demokrasia hiyo hiyo inayopigiwa kelele na 'wanaharakati' kufanya uamuzi aliouna sahihi na CCM kwa demokrasia waliyonayo ndani ya chama na mikakati ya kuendelea kuongoza nchi kwa maslahi ya watanzania wote safi wakamuunga mkono. Sasa ni mbunge wa Kinondoni. Hii ndiyo gharama za demokrasia, ni wajibu wa kila chama cha siasa kutumia furusa zilizoko kwenye demokrasia kukamilisha mipango yao yenye nia njema kabisa kwa wananchi. Tusinung'unikie gharama ya demokrasia...demokrasia tuliitaka na bado tunasisitizwa kujiendeshe kidemokrasia.

  Asante P. Mayalla kwa uzi!
   
 4. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #483
  Mar 14, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 12,231
  Likes Received: 6,893
  Trophy Points: 280
  Pascal Mayalla wakati mwingine vijipropaganda vyako huwa havieleweki.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...