Trend Reading: Rais Magufuli amebadilika, he is changing for the better, ameonyesha uwezo, anaweza!. Mei Mosi ya leo atapandisha mishahara!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,

Hili ni bandiko kuhusu Trend reading, Trend Reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo jambo lililofanyika bali bali unaliangalia kwa kujiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika ni nini? na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa jambo hili ni nini?, ndipo unakuja na conclusion kama hii.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli na Awamu yake ya tano, hajawahi kupandisha mishahara ya watumishi kwa kipindi chote cha miaka yake mitatu madarakani, na sio tuu hajawahi kupandisha mishahara, bali hata zile annual salary increments zime freez, ziko at stand still zikipiga mark time.

Kuna mengi makubwa mazuri Rais Magufuli amekuwa akiyesema na kuyafanya kuhusu Taifa letu Hili la Tanzania, lakini pia kuna madogo machache mabaya yamekuwa yakifanyika chini ya utawala wake ambayo sio ya kawaida, sio ya kisheria, sio ya kiutaratibu na sio ya kikanuni na kunyamaziwa.

Moja miongoni mwa madogo mabaya haya ni kutopandishwa kwa mishahara ya watumishi wa serikali haswa ile annual salary increment.

Kuna watu wanadhani mshahara ni favour of president, yaani hisani ya mwajiri. No, mshahara sio hisani, mshahara ni haki ya mtumishi au mwajiriwa yoyote kama haki nyingine zozote, na kupandishwa kwa mishahara sio favour au hisani, bali ni haki kama haki nyingine zote, zile annual salary increment sio favour ni right ni haki za wafanyakazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, hivyo there is no excuse to justify that for whatever reasons there might be.

Lakini kwa kusoma trends za mabandiko positive kwa rais wetu Magufuli ambaye each passing day, he is changing for the better, something is telling me that today, leo, rais Magufuli atapandisha mishahara ya watumishi wa serikali, hata kama sio nyongeza kubwa, lakini naamini kabisa angalau zile annual salary increments and a little bit more, zitatolewa.

Let just wait attentively kusubiria nyongeza hiyo, ikiisha tangazwa rasmi na rais wetu Magufuli, ndipo nami nitarejea na kuwapa trends zenyewe za positive changes kwa Rais Magufuli, ili nisije nikazitaja hapa kabla, ikatokea rais Magufuli ameingia JF asubuhi hii, na kwa vile aliisha sema yeye hapangiwi, asije kusoma humu na kukasirika na kuamua kughairi kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma leo Mei Mosi ya mwaka huu kwa kisingizio kuwa amepangiwa, asinge pangiwa angeongeza mishahara, hivyo soma bandiko hili kimya kimya kimya tukisubiria nyongeza hiyo mishahara.

Japo katika bajeti ya re current expenditure sikuona fungu la kuongeza wagebill, lakini kitu kizuri kuhusu rais Magufuli, hata bila kuidhinishwa Bunge, "anaweza". Kama kwenye kununua ndege, ameweza bila bajeti hiyo kuidhinishwa na Bunge, atashindwa nini kuongeza mishahara ya watumishi wa umma. Kama ameweza kwenye flyover, ameweza kwenye SGR, ameweza kwenye Stigler Gorge, atashindwaje kwenye hili la nyongeza ya mishahara?. Rais Magufuli namuaminia, akiamua anaweza.

Hivyo Watanzania, lets be very hopeful na very positive kwa rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuwa, at least this time around, he will do the right thing and God will bless him and bless Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais wetu Magufuli,
Mungu Wabariki Wafanyakazi wa Tanzania kwa uvumilivu mkubwa ulio wajaalia wa kuvumilia yote.

Nawatakia Mapumziko Mema ya Sikuu ya Wafanyakazi na mishahara juu.

Paskali.
Trend Reading: Rais Magufuli amebadilika, he is changing for the ...
Trend Reading: Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri Yananukia ...
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 ...
Trends Reading: Tetemeko Bukoba, Walinyamaza, Ajali ya Kivuko ...
Trend Setting: Mapendekezo ya JF kwa mabadiliko ya Baraza la ...
Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba ...
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 ...
Trend Reading: Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri Yananukia ...

Update.
Rais Magufuli amemaliza bila kuongeza mshahara hata senti moja, ila kama nimemsikia akisema ile annual salary increment italipwa.
Kiukweli Wasukuma tuko Wasukuma wa aina nyingi!, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, nimemvulia kofia kwa kuusema ukweli wake macho makavu bila hata kupepesa macho, hajaongeza hata senti tano!.

Naombeni mnisamehe bure kuwapa matumaini hewa. Mimi nilipoona rais Magufuli anatembelea na mabulungutu ya fedha taslim cash money na kuzigawa kwa wahitaji mbalimbali katika ziara zake, basi nikajua, sasa Magufuli amekuwa na roho njema na roho safi ya moyo wa kutoa ili watu wapate, nikajua na mishahara atatoa, na haswa kuzingatia kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa, basi mimi nikategemea mishahara lazima itaongezwa kwa ajili ya kura, kumbe nimekosea.

Hata hivyo, kwa vile hili ni bandiko la trends, sometimes trends zinakwenda ndivyo sivyo, ila kwa vile ameahidi kupandisha mishahara kabla mwisho wa madaraka yake, na kwa vile mwisho wake wa madaraka ni mwakani, hivyo sasa for sure, Mei Mosi ya mwaka ujao ndio mishahara itaongezwa, haswa kwa kuzingatia mwakani ni mwaka wa uchaguzi mkuu, then, nyongeza hiyo itakuwa na maana kubwa zaidi kuliko angeongeza mwaka huu.

Kiukweli hapa nilipo, sura imenishuka, nimekuwa mdogo kama sisimizi au piriton.
Wafanyakazi poleni sana.
Life goes on.
Paskali
 
Frustration hutokea pale ambapo tunatarajia makubwa na kupata madogo au kutopata kabisa.

Kama ataongeza mishahara ilo lipo wazi ili kutuliza hali ya hewa kwa ajili ya uchaguzi baadae mwaka huu na mwakani. Na hasipoongeza hilo lipo wazi tu kutokana na trend yake tokea alipoingia madalakani hadi sasa hivyo hakutokuwa na jipya.

Jambo la msingi hapa ni kuwa mshahara na ongezeko la mshahara ni haki ya mwajiriwa na ipo kwenye mikataba ya kazi hivyo kama ameamua ku breach mikataba na kuwa yeye ndio katiba, that is well and good.

Sioni sababu ya kuwafanya watumishi, "They know nothing" na ni watu wa kupigia magoti haki zao ndo wazipate.
 
Pigeni Kaz bhana, mnachopata hakiwatoshi? Kuna mtanzania Yuko ubwindeni huko, hana kituo Cha afya, barabara mbovu, maji badala ahangaike na hizo changamoto, mnataka awaongezee nyie mnaofanyia Kaz kwenye viyoyozi, acheni utani,

Mwacheni Rais wetu apambane na vitu vya msingi Kwanza, miradi na uchungu alionao na nchi n mku wa, tumuunge mkono, tumwombee na tumtie nguvu
 
Atapandisha mishahara kwa kiasi gani?
Ukizingatia ni muda mrefu mishahara haijapandishwa ikiongezwa elfu kumi,ishirini,thelathini bado ni maumivu
 
Ewe mtumishi mwenzangu kama unasoma huu uzi, achana kabisa na kuwaza nyongeza ya salary!!

Jiongeze, piga kazi piga dili kipato kiongezeke!! Ikishindikana kabisa jilipe mwenyewe huko kazini kwako!!

Hata akisema ataongeza utapigishwa mark time mpaka uchoke... Wataanza uhakiki, mara uhakiki wa madaraja... Kuja kizinduka mwaka umeisha!!
 
Back
Top Bottom