fuentte
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 2,534
- 7,122
Mkuu natamani sana kujua kiundani zaidi kuhusu uwekezaji wa namna hii.Kwa jinsi mambo yalivyotokea kipindi cha nyuma kidogo uwekezaji wa aina hii ulipungua kiasi chake, ni wazi kunahitajika sera bora zenye manufaa na kuhakikishiwa usalama kwa wawekezaji nchini, wote wawekezaji wa ndani na hata wa nje. Benki kuu kimsingi imejitahidi mno katika kutoa viwango vizuri vya riba katika hizi treasury bills na bonds.
Walau katika kipindi cha Mama yetu sera za uwekezaji zinaeleweka. Wawekezaji wanahitaji uwekezaji wenye uhakika hivyo naamini kwa mambo yalivyo huenda interest cap ikazidi kupanda kila watakapo toa coupon rates mpya. Mimi ninawekeza katika vipindi vya miaka 7 tu na interest cap yake inanipa manufaa zaidi kuliko bonds za miaka 25. Hasa ukizingatia inflation pamoja na mabadiliko ya kisera.
Ni uwekezaji muhimu kwani ni less risky lakini faida yake haijengwi na Leo. Ila ni salama mno kuliko ununuzi wa hisa hasa kama huna financial knowledge ya soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE).
Tafadhali naomba unipe dondoo namna ya kuanza na ABCs nyingine muhimu,
Shukrani.