Mtamba wa Panya
JF-Expert Member
- Aug 6, 2017
- 695
- 1,712
Hati fungani ni biashara "kichaa" na watu pekee ambao wanawekeza kwenye hii biashara ni wale waoga wakupoteza thamani ya mitaji ya pesa zao. Mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya mafao pamoja na mashirika mengine bila shaka hutumia njia hii ya uwekezaji ili kutunza mitaji yao pengine ni kutokana na ukubwa wa mitaji ambao ni vigumu kuwekezwa kwenye sekta zenye "Higher Risk but greater return".
Tukichukulia mfano wa Hati fungani za miaka 20 za serikali zinazotoa riba ya 15.49% p.a: Angalia mtiririko ufuatao;
Tuchukulie umewekeza kiasi cha Tsh x kwa muda wa miaka hiyo 20, jumla kuu ya malipo utakayopata baada ya miaka 20 ni Tsh;
lakini kumbuka kuna kitu kimoja ambacho huzikumba FIAT Currency zote duniani, nacho ni Inflation au Mfumuko wa bei . Tukichukulia wastani wa 3.7% p.a (kwa mujibu wa takwimu za NBS [1], hapa naomba tusifikirie suala la "kupikwa" takwimu na naomba tuunge mkono juhudi) kwa muda wa miaka 20 hiyo ya uwekezaji wako. Then mtaji wako wa Tsh x baada ya miaka hiyo 20 utakuwa na thamani ya Tsh;
Hii inamaanisha faida ya uwekezaji wako kwa muda wa miaka 20 ni Tsh;
ambayo ni faida ya asilimia 100 kwa muda wa miaka 20; ambayo yenyewe kiuhalisia ni Tsh;
yaani kwa mahesabu ya "pesa yako ya kweli" ya miaka 20 iliyopita, faida yako ni asilimia 48.4 tu.
Hebu tuangalie mfano mwingine, iwapo mtu atawekeza kiasi kilekile cha Tsh x kwa muda wa miaka 20. Tukichukulia wastani wa faida ya asilimia 10 kwa mwaka, then baada ya miaka 20 mtaji wake utakuwa ni Tsh;
ambapo faida yako itakuwa ni Tsh;
yaani mara 4.659 ya mtaji wako wa awali, ambayo kiuhalisia ni faida ya Tsh;
yaani asilimia 225.3 kwa mahesabu halisi ya miaka 20 iliyopita.
sasa unaweza kuona kwamba kwa wastani wa faida ya asilimia 10 tu kwenye biashara yako kwa miaka 20 faida unapata asilimia 225.3 wakati kama utakuwa umewekeza kwenye hati fungani utakuwa umepata faida asilimia 48.4 tu japo utakuwa kwenye "risk free investment".
Je, kama utafanikiwa kupata faida ya wastani wa asilimia 20 kwa muda wa miaka 20 unaweza kupiga hesabu ni kwamba utapata faida kubwa zaidi. Yaani;
Baada ya miaka 20 mapato yatakuwa ni Tsh;
kumaanisha faida yako itakuwa ni Tsh;
ambayo kiuhalisia ni Tsh;
yaani faida ni mara 17.538 ya mtaji ulioanza nao "miaka 20 iliyopita"
Sasa unaweza kuona kwa faida ya kufanya biashara ukapata wastani wa 20% profit kwa miaka ishirini ni 1753.8% wakani hati fungani ni 48.4%.
Hakuna mfanyabiashara anayeelewa biashara akawekeza kwenye hati fungani labda kama hakuna namna na yeye anataka kulinda mtaji wake usishuke thamani.
Ahsanteni.