TRC yaendeleza kampeni ya uelewa kuhusu usalama na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli ndani ya treni za mijini katika Jiji la Dar es salaam

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
Shirika la Reli Tanzania – TRC linaendelea na kampeni ya uelewa kuzuia ajali na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli kwa kutoa elimu kuhusu mambo ya kuzingatia katika maeneo ya miundombinu ya reli kwa abiria wa treni za mijini Dar es Salaam iliyofanyika katika treni inayoelekea Ubungo na Pugu Februari 7, 2020.

Kampeni hiyo endelevu inayofanywa na TRC ambapo lengo ni kutoa elimu ya uelewa juu ya mambo yanayohusu kuzuia ajali na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli ikiwemo matumizi sahihi ya alama za reli, kuhimiza utunzaji wa miundombinu ya reli, mfumo wa kushughulikia maoni, malalamiko na taarifa zinazoripotiwa kuhusu hujuma ya miundombinu ya reli.

Zoezi hilo limeendeshwa na timu ya mawasiliano kutoka Idara ya Usalama wa njia ya reli na Kitengo cha Habari na Uhusiano kutoka TRC kwa kuzungumza na abiria wa kawaida pamoja na wanafunzi wanaotumia usafiri wa treni kuelekea Ubungo na Pugu katika nyakati za asubuhi na jioni ambapo maafisa hao walitumia mfumo wa matangazo uliopo katika treni na kupitia mazungumzo ya ana kwa ana kutoa elimu ya uelewa.

Afisa usalama wa miundombinu ya reli Bwana Edward Chezari amewaasa wananchi wawe makini wawapo karibu na miundombinu ya reli kwa kuepuka kukaa, kufanya biashara katika maeneo ya reli na kuacha kutumia spika za masikioni wanapokuwa karibu na reli kwa kuwa zinahatarisha usalama wa maisha eneo la kivuko kwa watu kushindwa kusikia honi ya treni pindi inapopita.

”Ukifika kwenye eneo la makutano ya barabara na reli inapaswa kutulia na kuangalia pande zote kwa umakini kabla ya kuvuka ,na kwa wanao tumia vyombo vya moto wawe makini pindi wanaposikia treni inakuja”, alisema ndugu Chezari.

Pia wananchi wameipokea kampeni hiyo na kuitaka serikali iwachukulie hatua madhubuti kwa wale wote wanaokiuka sheria na kuhujumu miundominu ya reli ili iwe mfano kwa wengine kuacha kuhujumu miundombinu hiyo na kuweza kuitunza na kuilinda.

Hata hivyo abiria wamelipongeza Shirika la reli Tanzania kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya reli na kutoa elimu ya uelewa kuhusu ulinzi wa miundombinu ya reli pamoja na alama zinazowaongoza madereva, abiria na watembea kwa miguu katika njia za reli.

Kwa upande wake abiria Amosi Rehani amefurahishwa na usafiri wa treni za mjini kwani umesaidia kuokoa muda kwa wakazi wa mjini kwa kupata usafiri wa uhakika na salama ambao hauna foleni ukilinganisha na usafiri wa magari katika njia za kawaida.

IMG_20200208_104635_205.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom