TRC: Picha zinazosambaa ni za Mabehewa ya safari ndefu, mengine yatafika Juni 2023

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,062
10,247
.
JamiiForums-1018205869.jpg
 
Binadamu Mtakatifu

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
2,103
4,106
Hahahahahaha.

Wakumbuke tu hii dunia ya sasa sio ile ya Mwalimu Nyerere ambayo watu hawako well informed, dunia ya sasa upatikanaji wa information na uelewa wa watu ni mkubwa sana, unapotoa taarifa yeyote au hata kama unataka kudanganya unapaswa kutumia akili nyingi saana vinginevyo utaona raia wako wakorofi sana.

Tofauti ya mabehewa ya safari ndefu na fupi ni nini?.... kilichoonekana na wananchi bandarini na kuanza kupiga kelelel ni muonekano wa nje wa mabehewa ndio unaonyesha its old ages, repaired used etc.

Behewa la safari ndefu na fupi utofauti wake ni kwenye technicality ambazo mtu wa kawaida hawawezi kuziona labda technical oriented personnaly.

tofauti la behewa la safari ndefu na fupi lipo kwenye engineering design hasa tires and rims, brakes system, rollers, suspensions and spring etc, SIO KWENYE MUONEKANO WA NJE, TUACHE USANII WA KIZAMANI DUNIA IMEBADIRIKA KIDOGO.
Kumbe treni ina tairi na rim ahsant kwa taarifa
 
Gfav

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
234
355
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema mabehewa yote yaliyoainishwa kuletwa kwa ajili ya treni ya Reli ya Kisasa (SGR) yatakuja na kwamba yaliyoanza kuingia nchini ni ya safari ndefu.
View attachment 2426194

Wiki hii katika mitandao ya jamii kumekuwa na picha zikionyesha mabehewa yaliyoletwa sio yale yaliyoahidiwa kuletwa nchini kutokana na tofauti ya muonekano wake.

Leo Alhamis Novemba 24, 2022, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amezungumza hayo wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea ujenzi wa SGR katika eneo la Kikuyu jijini hapa.

“Tayari tumeanza kupokea mabehewa 14 ya abiria kwa ajili ya uendeshaji wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro,”amesema.

Amesema picha zinazosambaa katika mitandao ya jamii zinaonyesha mabehewa hayo ambayo yatapokelewa rasmi kesho Ijumaa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Kadogosa amesema picha ya mchongoko zinazoonyeshwa katika mitandao hiyo ni za treni ambazo zitatumika kwenye safari za mda mfupi na kwamba treni hizo zitawasili Juni 2023.

Amesema safari za treni ya SGR kati ya Dar es Salaam hadi Morogoro zitaanza Februari 2023.

Aidha, Kadogosa amesema taarifa kuwa kuna mabehewa yatapigwa mnada sio za kweli na kwamba TRC haihusiki na hilo.

Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita imelenga kuimarisha sekta ya usafirishaji ili kupanua uchumi wa mtu mmoja na Taifa kwa kuwezesha watu wanaofanya shughuli zozote za kiuchumi kupata usafiri.

“Hapa Dodoma kutajengwa bandari kavu kubwa sana, eneo la kuweka mizigo kutoka bandarini litakuwa hapo…nataka niwahakikishie usimamizi huu wenye maelekezo ya mkuu wa nchi, sisi tuliopewa dhamana ni kufikia malengo,” alisema.

Ya safari fupi ya naenda wapi?
 
Marashi

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
2,656
3,910
Kadogosa anabugi,, watu wanataka yale ya high speed train,, yale yako kama ndege,bora asiwape matumaini, halafu yasije,, high speed train huwa ina operate kwenye njia yake special,, sidhani hiyo reli itamudu kupitishq high speed train
Wanavojichanganya unaoata feeling kuwa mwenye project yake alishatangulia mbele ya haki wamekuja wapigaji.

Unajenga reli ya standard gauge unaleta vichwa na behewa za "ngongongo"
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
45,257
52,767
Hahahahahaha.

Wakumbuke tu hii dunia ya sasa sio ile ya Mwalimu Nyerere ambayo watu hawako well informed, dunia ya sasa upatikanaji wa information na uelewa wa watu ni mkubwa sana, unapotoa taarifa yeyote au hata kama unataka kudanganya unapaswa kutumia akili nyingi saana vinginevyo utaona raia wako wakorofi sana.

Tofauti ya mabehewa ya safari ndefu na fupi ni nini?.... kilichoonekana na wananchi bandarini na kuanza kupiga kelelel ni muonekano wa nje wa mabehewa ndio unaonyesha its old ages, repaired used etc.

Behewa la safari ndefu na fupi utofauti wake ni kwenye technicality ambazo mtu wa kawaida hawawezi kuziona labda technical oriented personnaly.

tofauti la behewa la safari ndefu na fupi lipo kwenye engineering design hasa tires and rims, brakes system, rollers, suspensions and spring etc, SIO KWENYE MUONEKANO WA NJE, TUACHE USANII WA KIZAMANI DUNIA IMEBADIRIKA KIDOGO.

Kabisa kwa mfano Gerson Msigwa kautangazia umma kwamba Ruvu imejaa pomoni kutokana na mvua kunyesha sana morogoro na kweli wakafungulia maji ya kisima ya kigamboni kuanzia jumamosi ili watu waamini kwamba ni kweli tatizo lilikuwa mvua.......Ruvu bado empty na mvua morogoro ni ya kawaida sana tena sehemu chache tu.

Ila usipokuwa makini utawaamini na progaganda zao.
 
12 Reactions
Reply
Top Bottom