Narudia kusema Tanzania ya leo ukilala njaa nisiri yako,usishangae mambo unayosema sii ya lazima kwakuwa tunayo makubwa na ya muhimu zaidi ya hayo yanayo hitaji gharama.Hii ajali ya majuzi, treni kuacha njia baada ya mvua kubwa, limeniacha na maswali ambayo lazima yajibiwe.
Baada ya ajali mbaya ya train na MV Bukoba zilizotokea miaka ya My Mkapa, Awamu ya pili, nilitegemea tutakuwa kumetengenezwa Stand at Operating Procedures kwa kuendesha hivi vifaa vyetu cha mass transport.
Haingii akilini kuwa reli haikaguliwi KILA KABLA YA SAFARI.
Na haingii akilini kuwa ma Station Master kati ya vituo vikubwa viwili vya karibu hawakuwasiliana.
Na haingii akilini kuwa dereva wa train hakuwa na weather reports, na hali ya mito mbele ya safari yake.
Haingii akilini vile vile kwamba kusafiri kwa reli za TRC is a question of chance, kufika safari yako ni majaliwa.
Hata yote, TRC inapaswa kuyajibu.