TRC kuna jipya mwaka huu? Itapendeza kama mtanijibu

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Kwa mara ya kwanza nilisafiri na treni ya Deluxe mwaka huu mwezi wa kwanza. Niliinjoy sana kutokana na huduma na mambo niliyojionea huko
Uzi huu 👇👇

Katikati ya mwaka huu nilisafiri kwenda Moshi msibani ila nisafiri na msafara wa coster (za msiba) zilikua 8 na gari za kawaida kama 5 pamoja na ila ya special kwa maiti 1.

Wakati wa kurudi sababu tulirudi na hizo gari nikagusia usafiri wa treni na jinsi ulivyo mzuri. Jambo kusikitisha nilikutana na wasafiri wa treni wakisema hawatapanda tena treni kwani walitoka Moshi jioni ya saa 10 na kufika Dar saa 5 asubuhi (11:00 am).
Walilalamika kuwa ilikua inasimama sana na pia mwendo ulikua mdogo tofauti na ilivyozinduliwa.

Sasa mimi naipenda hii treni na nimeitangaza sana hata niliona ushauri ambao niliotoa mwanzo kwenye uzi juu hapo ulitekelezwa. Sasa https://www.jamiiforums.com/members/tanzania-railways-corp.481608/ kuna mabadiliko au bado mmekariri biashara? Mwaka huu mnakuja na kivutio gani cha kushawishi watu wapande treni? Vipi swala la muda mmerekebisha au bado ni saa 5 kuwasili?

My take:
Ili kuweza kumudu changamoto hizi za kuchekewa bora kuwe na vichwa vya kubali ili kuepusha zile service baada ya kuwasili na kugeuza. Kila trip na kichwa chake,kikitfika hiki kinageza kingine ambacho kimeshapoa na kuchekiwa na kiko tayari kwa safari.
 
Deluxe hii hii ya Kigoma??

TRC ilikuwa 80s 90s. Nilipanda ya Mwanza 1st Class December, niliapa sitorudia maishani. Yale mabox yaliyolowana nafikiri ndiyo behewa za scandal ya enzi ya Mwakyembe.

Tutapanda milele Allys, Nyehunge, Kisesa, DarLux kwa status ile ya mabehewa aissseeee!

Kwenye basi traffic wanadhibiti kusimamisha abiria, treni wanakatia watu kusimama Dar Kigoma, Dar Mwanza..inashangaza sana!

Everyday is Saturday :cool:
 
Deluxe hii hii ya Kigoma?

Everyday is Saturday:cool:
Basi hii ni tofauti na ya Moshi.
 
Basi hii ni tofauti na ya Moshi.
Aisee nilijutia nafsi yangu, nilijidai nataka kuwaonyesha watoto na familia jinsi tulivyosafiri na treni na mbwembwe!
Nilijilaumu SANA kuitesa familia vile!

Treni ilikuwa na 1st na third tu! Hao waliokuwa 3rd class sijui walikuwa na hali gani!

Ya Moshi ni level siti afu pia ni safi kwa sasa labda kwenye kuwahi ndio kuna tatizo
 
Screenshot_20201219_231129.jpg
hongereni naona treni mpaka 23 imeshajaa tayari
 
Back
Top Bottom