Travelling Partners Part two (2)

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,962
22,330
Kama mada inavyojieleza hapo juu, uzi huu ni mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia wale ambao wanataka kusafiri kwa ajili ya utalii lakini hawajui ABCs za kusafiri kama watalii.

Ninatambua kwamba kuna watu na makampuni kadhaa ambayo sasa yamekuwa yakitangazia watu safari za sehemu mbali mbali huku wakiwa na maneno mazuri na ahadi kadhaa wa kadhaa kuhusu safari hizo za kitalii. Sitaki kuzungumzia juu ya hayo maana hayanihusu na mara kadhaa humu Smart911 anatuambia "mambo yao tuwaachie wenyewe".

Kuna wadau wengi sana ambao wanatamani kusafiri lakini kuna vikwazo kadhaa vinawafanya wasisafiri. Vikwazo vichache ni kama ifuatavyo
(i) Uwezo wa kifedha- si Watanzania wengi ambao wana uwezo wa kutoa $ 1000- 1500 kwa mkupuo kwa ajili ya safari ya kitalii ya siku 7 mpaka 10
(ii) Elimu ya maeneo ya kutembelea- Hii inahusisha zaidi watu kutojua ni nchi ipi nafuu kutembelea na rafiki kutembelea
(iii) Kukosa drive ya kutimiza malengo- Hili linachangiwa na hali ya mtu kukata/ kukatishwa tamaa na mambo flani flani likiwemo kutotimiza malengo ya kipesa ndani ya muda aliojipangia kuandaa safari.

Binafsi nimeanza kusafiri kama mtalii miaka michache iliyopita na mpaka sasa nimefanikiwa kusafiri jumla ya nchi kumi na mbili zikiwemo South Africa, Kenya, Singapore, Malaysia, Cambodia, Thailand, U.A.E, Saudi Arabia, Turkey na Egypt. Nimepata uzoefu wa kutosha wa kusafiri kama mtalii huku nikitumia budget ya kawaida tu kila mara ninapo safiri.

Ili kuwafundisha na kuwafanya wengine waone kwamba inawezekana kusafiri na kwenda kutalii, nimeamua kuandaa safari ya Kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kutalii kule. Hii ni mahsusi kwa beginners kwa sababu hata gharama hazipo juu kabisa na pia hii ni nchi nzuri kutalii kwa beginners. Safari hii itafanyika kama ifuatavyo

(a) Wakati wa safari- June 2022
(b) Siku za kukaa Afrika ya kusini- siku saba (7)
(c) Gharama za safari - Dollar za kimarekani 1,000/= na gharama hizi zitahusisha yafuatayo:-
- Ticket ya ndege kwenda na kurudi (Dar - Johannesburg- Capetown- Dar).
- Accommodation ( siku 3 Johannesburg na siku 4 Capetown). Hotel zenye hadhi ya nyota 3 na kuendelea.
- Ticket ya ndege kutoka Johannesburg kwenda Capetown.
- Vipimo vya COVID- 19 (Tanzania na Afrika ya kusini).
- Chakula cha asubuhi na jioni kwa siku zote saba.
- Usafiri wa kwenda na kurudi airport/ hotelini ndani ya Afrika ya kusini.

Kwa kuwa hii ni safari ninayotaka kusafiri na kundi la watu, basi idadi haitozidi watu kumi (10).

Kwa wote ambao wapo interested basi waje inbox, tutabadilishana namba za simu na kuunda kundi la WhatsApp ambalo tutendelea na mipango yetu.

Utakapoona unaweza kujumuika nasi basi utahitajika kulipia $250 (dola mia mbili na hamsini au laki tano) , baada ya malipo hayo utakabidhiwa ticket yako na itakuwa mguu mmoja tayari upo safarini. Hii $250 au laki tano itakuwa ni non- refundable isipokuwa tu katika mazingira ambayo inastahili kufanya refund ambayo tutayajadili kundini.

Kwa kutambua changamoto ile niliyoitaja kwamba si watu wengi wenye kuweza kutoa pesa zote $1000 kwa mpigo, binafsi nitazikata ticket za ndege zote za washiriki kwa kutoa pesa yangu mfukoni na wao watakuwa wakilipia safari kidogo kidogo ambapo May 25th itakuwa ni deadline ya kukamilisha malipo yote.

Naamini watu watakuwa na maswali mengi sana, nakaribisha maswali hayo na nitayajibu kwa kadri ya uwezo wangu.

ANGALIZO: Tafadhalini aje inbox yule ambae yupo serious na anajiona anataka kutimiza ndoto yake au zake za kusafiri.
 
I love travelling...

But most of time with my Dadii or solo.

Wish you all the enjoyment in your coming trip.
Good! This time you can also tell your daddy or opt to go solo.

I know kwa baadhi ya watu SA wanaweza wakaona pa nini huko?? Ila kwa beginners hii ni best opportunity.

Thanks for the wish though, kasie matata
 
Good! This time you can also tell your daddy or opt to go solo.

I know kwa baadhi ya watu SA wanaweza wakaona pa nini huko?? Ila kwa beginners hii ni best opportunity.

Thanks for the wish though, kasie matata

Okay thanks for the invitation, not promising...

Naweza nikawa solo ila nikawa nawajoin kwenye tour sites kwa pembeni like hi and bye tukiwa huko after that nakuwa kivyangu vyangu...

Mazoea mabaya..😉.

Idea yako ni nzuri, wataojoin watafurahia sana.
 
Okay thanks for the invitation, not promising...

Naweza nikawa solo ila nikawa nawajoin kwenye tour sites kwa pembeni like hi and bye tukiwa huko after that nakuwa kivyangu vyangu...

Mazoea mabaya..😉.

Idea yako ni nzuri, wataojoin watafurahia sana.
Karibu sana kasie,

Ntafurahi ukijiunga nasi.

Na kwa vile wewe ni mzoefu hatutoogopa sana hata ukiwa kivyakovyako kule.

Looking forward to it
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom