Transparency International: Tanzania inafanya vizuri Kupambana na Rushwa na Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Transparency International: Tanzania inafanya vizuri Kupambana na Rushwa na Ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Dec 4, 2011.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wakati vyama vya Upinzani, hasa CHADEMA haitambui kazi wafanyayo Serikali ya Kikwete, taasisi kubwa ya kimataifa 'Transparency International' imethibitisha kutambua juhudi za serikali kupambana na rushwa kuzaa matunda. Haya yamesemwa na uongozi wa Taasisi hiyo, ilipotoa Ripoti yake ya Rushwa hivi karibuni ya 2011 kwa nchi zote duniani.

  Katika taarifa hiyo Tanzania ina index 3 na kushika nafasi ya 100 kati ya nchi 182 duniani. Ukilinganisha na mwaka jana Tanzania ilikuwa na index 2.7 na ilikuwa katika nafasi ya 116 duniani. Hii inamaanisha kuwa Tanzania imezipita nchi 16 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Nchi zinazoshika mkia ni pamoja na Somalia, Afghanistan na Korea Kusini. Wakati New zealand, Danmak na Finland zikiongoza kwa kufanya vizuri.

  Kinachonishangaza mimi ni kutosikia pongezi toka kwa wapinzani ambao wamekuwa mstali wa mbele sana katika kukemea rushwa. Sijaelewa kama maana ya demokrasia ya vyama vingi, maana yake ni kwa vyama pinzani kusema mabaya tu na kutotaja hata zuri moja lililofanywa na chama tawala. Kama hivyo ndivyo, ni nini maana ya kuwa na vyama pinzani ambavyo kila siku vinasubiri Serkali kufanya makosa ndipo vipaze sauti KWELI UPINZAni Tanzania umekufa na hata kama upo si kwa faida ya watanzania.

  Angalia ripoti nzima hapa: Corruption Perceptions Index: Transparency International
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Hao TI sijui wanakusanya vipi hizo takwimu zao zinazoonyesha kwamba kuna mafanikio katika kupambana na rushwa. Juzi juzi tu tumeona jinsi Jairo alivyohusika na kukusanya shilingi milioni 50 katika taasisi mbali mbali zilizo chini ya Madini na Nishati ili kutoa rushwa kwa Wabunge wapitishe bajeti ya Wizara hiyo.

  Wahusika akina Ngeleja, Malima na Jairo wamechukuliwa hatua gani hadi hii leo? Washiriki wa ufisadi wa rada wamechukuliwa hatua gani hadi hii leo? wahusika wa Meremeta, Kagoda n.k. wamechukuliwa hatua gani hadi hii leo?

  Huwezi kupambana na rushwa/ufisadi wakati wahusika hawachukuliwi hatua zozote zile kufuatana na sheria za nchi. Ni usanii kusema kwamba Serikali ya Kikwete imepata mafanikio yoyote katika kupambana na rushwa. Hao TI lazima wawe very careful katika tafiti zao vinginevyo katika nchi nyingi watapoteza credibility yao (kama bado ipo).
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  kwa kweli JK kajitahidi:

  1. EPA walirudisha pesa yetu
  2. Jairo kapewa likizo ya malipo
  3. Hosea alipewa onyo kali kwa kutetea Richmond
  4. CCM imejivua ngamba...

  Kama si uchakachuaji wa TI tungekuwa hata wa '2' nyuma ya New Zealand, wapinzani hamuoni haya
   
 4. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wakati wa Mkapa na Marais wengine hata hayo matukio kama ya akina Jairo, EPA n.k ilikuwa ni taboo kufasikika kwa wanyonge kama sisi. Unapotaka kupambana na tatizo ni lazima kwanza kukubali kuwa lipo. La pili ni kuviruhusu vyombo vya habari vipate habari za taasisi au watu hao wala rushwa au mafisadi. Hivi hatukuviona katika serikali zilizopita.

  Nyerere alikuwa anawahamisha watu kama akina Jairo toka idara moja hadi nyingine, halikadhalika wakuu wa mikoa, mabalozi na wakurugenzi. Mwinyi alikuwa anawaogopa na mkapa alikula nao sahani moja.

  Jingine la kufahamu ni kuwa INDEX ina kipimo toka 10 mpaka 0, ikiwa No 10 ndio nchi safi sana na 0 ni zile zilizokithiri kwa rushwa. Kwa maneno mengine bado rushwa ipo na ni kubwa kuangalia hiyo skala. Ninachosema ni kuwa juhudi zifanywazo na serikali zinaleta matunda. Kuna nchi kadhaa za Afrika tunazipita, angalia mwenyewe katika tovuti hiyo. Hata Kenya na Uganda zipo hoi kwetu.
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Hao jamaa wako bize sana. Kufanya tafiti katika inji 182 si mchezo ati?
  Kwa hiyo kutoa matokeo ya kulipua si jambo la ajabu!
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Kitu unachotakiwa kukumbuka na kuwa muwazi na mwenye uelewa mpana ni vipi Jairo na wizara nzima imelipuriwa, nna uhakika Shelukindo ni mmoja wa watu waliotumiwa na intelijensia yetu kuripuwa bomu, haiwezekani kuwa kayajuwa tu hivihivi na ki "note" kakiokota tu njiani.

  Ilikuwa atumiwe mmoja wa wana intelijensia aliopo bungeni kupitia upinzani lakini ikaonekana itazidi kutia dosari CCM. Amini usiamini, juhudi za dhati zinafanyika kupigana na rushwa lakini we have a long way to go ikiwa adhabu kali hazitatolewa.

  Mimi napendekeza "top secret elimination squad". Ambayo itafanya kazi zake kwa siri kubwa, itachaguwa magwiji wa rushwa na wale waliojilimbikizia mali kwa njia za haramu, ikipata ushahidi japo circumstantial, inawa eliminate na siku ya pili yanatolewa makosa yao kwenye vyombo vya habari, hakuna kupelekwa Mahakamani hakuna kupoteza wakati, nnakuhakikishia wakifika watano tu, hata umpe millioni trafik hachukuwi na faini anakulamba. Bila hivyo, tutahangaika miaka nenda miaka rudi, tutalipunguza tu kwa kiasi fulani hili tatizo.
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  KUTOKA 116 MPAKA 100 NDIO UNAITA MAFANIKIO.
  mafanikio dhidi ya rushwa yanapimwa kwa watu wangapi waliochukuliwa hatua kwa kwenda jela kwa ajili ya kula rushwa. tangu aingie ikulu mwaka 2005 mpaka leo hakuna kigogo hata mmoja aliyekula rushwa ndani ya grand corruption hata mmoja aliyekwenda jela mawaziri wa Tanzania wanaongoza kwa kula rushwa lakini wanaokamatwa kila siku ni waalimu na wauza maandazi.
  EPA
  RICHMOND
  GREEN
  RADAR
  KAGODA.

  SANASANA NCHI TUMESHUHUDIA RAIS MZIMA ANAWAPA WEZI PAYMENT PLAN. AIBU KUBWA.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280

  Sidhani kama sheria za utawala bora ndio zinasema hivyo, kwamba unapotaka kupambana na rushwa basi kwanza ni kukubali kwamba Tanzania kuna rushwa (iliyokithiri) halafu uruhusu vyombo vya habari vipate habari za taasisi au watu wala rushwa au mafisadi halafu hapo ndio uwe mwisho wa kupambana na rushwa.

  Viko wape vyombo vya dola (Takukuru, polisi na mahakama) ili viwachunguze wahusika wa kutoa na kupokea rushwa huku wakiwa mahabusu na kama ukipatikana ushahidi wa kutosha (ambao upo katika kila ufisadi) basi watuhumiwa wapandishwe kizimbani na kufunguliwa mashtaka na kama watapatikana na hatia basi wahukumiwe bila uoga wowote ule, lakini tunachokiona ni usanii tu halafu hao TI wanasema eti tumepiga hatua katika kupambana na rushwa!!!! Hivi unadhani Kikwete angekuwa makini kupambana na rushwa Jairo angethubutu kukusanya bilioni moja ili kuzitoa kama rushwa kwa Wabunge ili wapitishe bajeti ya Madini na Nishati kinyemela!?

  Tuwe wakweli wa nafsi zetu badala ya kupigia makofi vitu ambavyo havistahili kabisa kupigiwa makofi. Rushwa na ufisadi bado vimeshamiri sana ndani ya magamba na Serikali ya magamba na sioni dalili ya kupambana navyo zaidi ya usanii tu. Wakati wa Mwalimu hakukuwa na ufisadi kama huu tunaouona sasa wa watu kukwapua mabilioni katika taasisi zetu mbali mbali (EPA, Kagoda, Meremeta, Rada, Ununuzi wa ndege ya rais, magari na helikopta za jeshi, mikataba ya madini, mikataba ya BoT ambapo Mkono kachota bilioni chungu nzima) . Rushwa ilikuwepo lakini haikufikia kabisa kiwango cha sasa.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Kwanini FF asiwe anashusha points kama hivi kila siku!? Hapo kwenye rangi sikubalini nawe. Sijaona juhudi zozote za kupambana na rushwa. Kikwete kulikuwa na matukio mengi ambayo kama angeamua kutumia ujemadari wake na kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa angejizolea sifa nyingi sana toka kwa Watanzania wote na hata mataifa mengine, lakini labda kwa woga wa jinsi alivyoingia Ikulu na hivyo kuogopa kuwagusa waliofanikisha safari yake ya kwenda Ikulu, ametuangusha sana Watanzania na cha kusikitisha zaidi ni kwamba bado ana miaka minne mingine ya kuendelea kuwepo madarakani. Kwa maoni yangu ataiacha nchi yetu ikiwa katika hali mbaya sana.
   
 10. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naomba huitake radhi korea ya kusini.ni korea ya kaskazini..
   
 11. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Zawadi ngoda,FF,rejao,na nyote nyie watetea ujinga na waleta upupu hapa Jf hebu mwambieni sharobaro wenu kuwa mshahara hatujapata. So kesho kesho j3 tutaanza na wiki ya kuchukua rushwa maofsini ili tuishi. Hawa TI credibility yao hovyo sana, kwanza ni uzandiki kudai s.korea au n.korea ni vinara wa rushwa,simply kwa kuwa makampuni yao yanachota tu hapa tz hivyo lazma watoe sifa za kipuuzi kwa serkali ili iendelee kulala.
   
 12. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jokers! Watu mpaka leo hatujalipwa mshahara kwa sababu za wazi kabisa, ufisadi na rushwa halafu mnaleta ripoti za kujipendekeza! Au kuna mmoja wao anataka kuwekeza kwenye kanchi ketu?
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio Kikwete, tatizo sio kuogopa, tatizo ni mfumo alioukuta Kikwete, kaukuta mfumo ambao upo na ni wa kulindana lakini licha ya huo mfumo Kikwete kaonesha mfano mzuri sana wa kupambana na Rushwa. Kikwete si mtu wa kukurupuka hata kidogo.

  Hayo madudu yote ya EPA, Kagoda sijui nini sijui nini, kayakuta na kayashughulikia na anaendelea kuyashughulikia, juzi tumeliona la Jairo na kimya kimya tunaona la Mataka, nani alijuwa kuwa la Mataka linashughulikiwa? TAKUKURU ingawa kuna mapungufu yake makubwa, lakini kuna nyooshwa na nnakuhakikishia wana shutuma nyingi sana wanazishughulikia, sema wanakwenda kimya kimya.

  Kuna uozo mkubwa sana alioukuta Kikwete Tanzania lakini ukijidai kufanya kama alivyofanya Sokoine, ujuwe unaiangusha hii nchi kiuchumi vibaya sana. Huwezi kwa dunia ya leo ukatmia Uamiri Jeshi kuendesha nchi. Ita "collapse". Kuna mengi ya kupoteza kuliko ku gain. Bora ya hivi, mambo mazuri hayataki haraka.
   
 14. m

  mbwago2007 Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kawaida taasisi nyingi za kimataifa kiisifia Tz kuwa inafanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu uchumi nk, wakati watanganyika tunaona kila kitu kinarudi nyuma licha ya kuwa nafasi ya tatu ya omba omba wa kimataifa. Nchi ambayo inakopa fedha kutoka kwenye mabenk ya kibiashara kwa ajili ya kulipana mishahara, posho na sherehe (rejea shrehe za miaka 50 ya Uhuru) wakati hospitali hazina dawa, shule hazina vifaa, upatikanaji wa umeme na maji usiokuwa wa uhakika. Kwa kifupi international organisation zina sera za "UKILA NA KIPOFU USIMGUSE MKONO" Rejea enzi za Ben Mkapa alitushangaa watanganyika kwa kuto kumsifia kwa vile alikuwa anasifiwa nje. Wale wa nje walikiwa na haki ya kumsifu kwa vile walijipatia mali zeu bure, kumbuka NBC, Meremeta Tangold n.k
   
 15. m

  mbwago2007 Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatujawahi kuwa na serikali nyingine tangu Tanganyika ipate uhuru zaidi ya serikali ya ccm, serikali hii ndiyo iliyoua uchumi na ndiyo iliyotufikisha nafasi ya 116 mwaka jana katika rushwa. Na usisahau kuwa sasa hivi tumeipiku Kenya kwa rushwa ambayo ilikuwa ikiongoza kwa muda mrefu katika enei la Afrika mashariki. Naomba ukumbuke kuwa hiyo serikali yako haikuwekwa madarakani ili kuendelezwa rushwa, bali iliwekwa ili kutokemeza rushwa ambayo imekuzwa na kupaliliwa na serikali hiyi hiyo. Kwa hali hiyo ni haki yetu kukosoa pale tunapoona haifanyi vizuri. Kwa nini unataka kupongezwa kuwa kazi yako ya msingi?
   
 16. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "mficha maradhi kifo humuumbua"
  mie nnatangaza mgogoro wa unafiki na wewe.Kwa muda mwingi umekua ukimtetea JK kuwa sio kosa lake.Katika ahadi zake kuelekea IKULU alituahidi kupambana na rushwa.matokeo yake leo hii amekua kinara wa haya matakataka yao,halafu unatuambia tatizo si yeye.Amepewa Rungu kama jemedali mkuu anakua muoga na wakati uko vitani.unataka tuone tatizo ni wengine?Vitani ukiwa mstari wa mbele halafu ukarudi nyuma bila amri lazima tukutie risasi ya makalio kwa kuasi.(hivyo kama ndivyo unavyomtetea JK ni muasi wa raia wa nchi hii)Pili tukikuambia mfumo uliopo wa CCM ndio unaolea hao mafisadi kwani ukiingalia CCM si jembe na Nyundo bali inaogozwa na mafisadi unaitetea,sasa unataka tukueleweje kama wewe sio mnafiki?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nilitaka kuuliza swali hili hili lakini umeshauliza. Thank you sir/madam
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kama hayo si mafanikio, sasa ungeyaitaje matokeo ya taarifa hiyo kama tungetoka nafasi ya 116 mpaka 150 au 182.
   
 19. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mambo ya kupambana na rushwa ni Mengi na si tu kutuma polisi na kuwapeleka watu mahakamani, bali vile viloe kuongeza kipato cha wafanyakazi, elimu na hata kuondoa upungufu au uhaba wa huduma husika.

  Kifupi hayo niliyoyataja nin mwanzo tu wa habari nzima, kwani kama hukujitambua kuwa unakasoro au wewe ni mgonjwa, Daktari hawezi kufanya lolote.
   
 20. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Sijakuelewa uliposema tumeipiku Kenya katika Rushwa, una maana kuwa sisi ni zaidi au.... Kifupi ni hivi Katika nchi tatu yaani Tanzania, Uganda na Kenya, Tanzania inaongoza kwa usafi kuliko Uganda na Kenya. Wakati Tanzania ina Index ya 3, Uganda ina 2.4 na Kenya ina 2.2. Napenda kukukumbusha tu kuwa katika skala hiyo ambayo ina namba 10 hadi 1. Namba 10 ndio wasafi sana (best) na Namba 1 ni wachafu sana au mabingwa wa Rushwa.

  Kutokana na Namba hizo ni dhahiri kuwa Kenya na Uganda Rushwa imeshamili zaidi kuliko Tanzania. Na si Uganda na Kenya tu tulizozipita bali ni nchi 72 kwa dunia nzima. Ni kweli bado kipande cha kumalizia ni kirefu, lakini angalau tunaweza kupiga makofi hata mara moja. Na haya ndio matunda ya uhuru ya miaka 50.

  Tukiwa wa wazi ni vyema kukiri kuwa serikali hii ya Kikwete imejitahidi sana kupambana na gonjwa lililokuwa sugu. Kwa mfano, japo hapa Jf na watanzania kwa ujumla tulimpigia kelele sana Sumaye akiwa waziri mkuu katika awamu ya Tatu ya urais, lakini Mkapa akiwa Raisi si tu alishindwa kumuondoa toka nafasi hiyo bali vilevile alimuandaa na kumpigia debe kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. FIKIRIA NCHI HII INGEKUAJE KUWA NA RAIS FISADI KAMA SUMAYE. Kama si juhudi za Kikwete na Membe leo hii tungekuwa na Rais mla rushwa na fisadi Namba wani. Na hii ingeendelea kizazi baada YA KIZAZI kwa mafisadi kuachiana urais huku wanyonge tusingekuwa na uchaguzi mwingine.

  Si huyo tu bali hata Lowasa naye leo kama asingetimuliwa, angekuwa na nafasi namba moja katika kinyanganyiro cha Urais mwaka 2015. Hata kama magazeti yanajaribu kumsafisha, lakini ni muhimu kusikiliza wakunga. Kama Mwl yerere alimtoa nje kwa tuhuma kuwa si msafi, na hii mara ya pili kutupwa nje kwa tuhuma hizo hizo kwanini tukazanie kuwa Lowasa ni msafi. Binafsi naamini kuwa nafasi zake za kuiongoza Tanzania zimekwisha, na ni muhimu awaachie wengine wapate nafasi hiyo kwani hatuna imani naye tena.

  Haya balali kafa kwa kihoro kutokana na kofi la Kikwete, na Jairo ndio maji shingoni hata bado sijamtaja Mungai. Huyo Mkapa amesakamwa kama mtoto mdogo ni kwa sababu hana akili nzuri, angekuwa na akili angeshakufa au kujinyonga kutokana na karaha ya wananchi japo hakufikishwa mahakamani.

  Hao ni wachache tui kuwataja, lakini msururu unaojiharishie kutokana na ukali wa Kikwete ni wengi nao hawamuoni Kikwete kama umuonavyo wewe. Kikwete ni Raisi mwenye staili yake ya uongozi, utacheka naye lakini inapofika kwenye kuwajibika hana simile.

  Hakuna aliyejua kuwa Makamba angeng'olewa katika nafasi yake ya ukatibu mkuu, au Rostam Aziz angeachie nafasi zake zote hata ubunge.

  Kubalini msikubali yaliyotokea wakati wa Kikwete kwa kuwatupa nje viongozi wasiowajibika ni mengi pamoja na kwamba hakuwatupa jela. Safari ni ndefu lakini tutafika tu.
   
Loading...