Transition period......

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,982
2,000
Baada ya Kikwete kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi (Ijumaa) kesho yake (Jumamosi) akaapishwa. Mwenzeni nilibaki na maswali kadhaa.

Hivi katiba yetu inasemaje kuhusu kuapishwa kwa raisi mpya? Maana nilijiuliza kama ingekuwa ndiyo Dkt. Slaa kashinda na kutangazwa mshindi Ijumaa hiyo na kesho yake kuapishwa, kungekuwa na smooth transition of power kweli?

Je, hili nalo ni moja ya mapungufu ya katiba yetu? Manake ni kama wanaharakisha tu kumwapisha huyo raisi mpya......
 
Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
195
Huu ndio udikteta na ubinafsi wa wengi viongozi wetu wa kiafrika, kwangu ushindi wa Kikwete,Kibaki,Mugabe n.k makes no difference
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,982
2,000
Huu ndio udikteta na ubinafsi wa wengi viongozi wetu wa kiafrika, kwangu ushindi wa Kikwete,Kibaki,Mugabe n.k makes no difference

Yaani inashangaza kweli. Mtu anatangazwa mshindi leo halafu kesho anaapishwa. Na wageni waalikwa wanakuja kutoka za nje kama vile walikuwa wameshatonywa kuwa kaeni mkao wa kula Jumamosi tunamwapisha Mkwere.....huo mwaliko ulitumwa lini kama mshindi alitangazwa jana yake tu? Gademu!!!
 
Baba Mtu

JF-Expert Member
Aug 28, 2008
871
225

Ratiba ya kuapishwa iko wazi, yaani inaeleweka ni lini rais mpya ataapishwa. Wageni waalikwa wanapewa taarifa kuwa ni lini rais wa tanzania ataapishwa iwe mkwere kikwete kama ilivyokuwa au kama angekuwa mchaga slaa au mnyamwezi lipumba, kwa hiyo wao wageni wanakaa mkao wa kula
 
Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Jun 18, 2008
241
0
Baada ya Kikwete kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi (Ijumaa) kesho yake (Jumamosi) akaapishwa. Mwenzeni nilibaki na maswali kadhaa.

Hivi katiba yetu inasemaje kuhusu kuapishwa kwa raisi mpya? Maana nilijiuliza kama ingekuwa ndiyo Dkt. Slaa kashinda na kutangazwa mshindi Ijumaa hiyo na kesho yake kuapishwa, kungekuwa na smooth transition of power kweli?

Je, hili nalo ni moja ya mapungufu ya katiba yetu? Manake ni kama wanaharakisha tu kumwapisha huyo raisi mpya......

Wasiwasi wako tu. Hapakuwa na kosa lolote. Kwanza kumbuka kwamba rais akishatangazwa hakuna mamlaka yoyote ya kutengua matokeo yake. Kuapishwa kesho yake au baada ya mwezi ni mipangilio tu na wala hapana dosari yoyote. Wewe ulitaka aapishwe lini na kwa sababu zipi ?? Hivi Dr. Slaa angeshinda kungekuwa na haya yote??? Ana wabunge wangapi na mwenzake ana wangapi??? Halafu (Slaa) anataka kudanganya umma kuwa alishinda!!!! Padri kusema uongo ni jambo baya zaidi kuliko asiye na dini.
 
Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,519
0
Ratiba ya kuapishwa iko wazi, yaani inaeleweka ni lini rais mpya ataapishwa. Wageni waalikwa wanapewa taarifa kuwa ni lini rais wa tanzania ataapishwa iwe mkwere kikwete kama ilivyokuwa au kama angekuwa mchaga slaa au mnyamwezi lipumba, kwa hiyo wao wageni wanakaa mkao wa kula
We unayejiita baba mtu, slaa sio mchaga ni mbulu.
 
TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,616
2,000
Ratiba ya kuapishwa iko wazi, yaani inaeleweka ni lini rais mpya ataapishwa. Wageni waalikwa wanapewa taarifa kuwa ni lini rais wa tanzania ataapishwa iwe mkwere kikwete kama ilivyokuwa au kama angekuwa mchaga slaa au mnyamwezi lipumba, kwa hiyo wao wageni wanakaa mkao wa kula

Wewe baba fisi, kwa jinsi ulivyomkabila unawataja kwa ukabila wao na kumbe Slaa ni Mbulu ndugu, wewe ulijua mchaga maana mnasema Chadema ni ya Wachaga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom