Transfer Window updates 2013/2014 season - Europe

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Kocha mzoefu wa Uholanzi Van Gaal (62) ameikacha Tottenham, sasa yupo kwenye mazungumzo na Manchester United.
Van Gaal ameshawahi kuzifundisha Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar na Bayern Munich kwa mafanikio
makubwa na ameahidi kuinogesha zaidi EPL.
======================================
DONE DEALS (BIG NAME TRANSFERS):

REAL MADRID
- Gareth Bale (24) ametua Real Madrid kwa uhamisho wa £85.3m (REKODI YA DUNIA) kwa mkataba wa miaka 6. Atalipwa mshahara wa £300,000 kwa wiki. Kumbuka Christiano Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la £80m.

ARSENAL

- Kiungo mchezeshaji anayeteleza Mesut Ozil (24) ametua Arsenal kwa mkatabawa miaka 5, kwa dau la £42.4m na mshahara wa £150,000 kwa wiki.
- Kipa Emiliano Viviano (27) ametua Arsenal kwa mkopo kutoka Palermo. Viviano anadakia pia timu ya taifa ya Italia.
- Kiungo Mathieu Flamini (29) amerejea Arsenal kutoka AC Milan kwa uhamisho huru. Flamini aliichezea Arsenal mwaka 2004 - 2008.
- Mshambuliaji Gervinho (26) ameuzwa AS Roma ya Italia kwa bei ya £8m.

CHELSEA
- Mshambuliaji kinda Romelu Lukaku (20) ameondoka tena, amehamia Everton kwa mkopo.
- Mshambuliaji Samuel Eto'o (32) ametua Chelsea kwa uhamisho huru kutoka Anzhi Makhachkala, kwa mkataba wa mwaka 1.
- Kiungo mshambuliaji Willian (25) ametua kwa uhamisho wa £30m kutoka Anzhi Makhachkala ya Urusi. Mkataba miaka 5.
- Kiungo Florent Malouda (33) ameondoka Chelsea kwenda Trabzonspor ya Uturuki kwa mkataba wa miaka 2.
- Mshambuliaji André Schürrle (22) kutoka Bayer Leverkusen ametua kwa dau £18m.
- Kiungo kinda Marco van Ginkel (20) ametua kutoka Vitesse Arnhem kwa dau la £8m.

LIVERPOOL
- Mshambuliaji wa Chelsea Victor Moses (22) amehamia Liverpool kwa mkopo wa msimu mmoja.
- Beki wa kati na kushoto Mamadou Sakho (23) ametua Liverpool kwa dau la £18m kutoka PSG.
- Beki wa kati Tiago Ilori (20) ametua Liverpool kutoka Sporting Lisbon kwa dau la £7m.
- mshambuliaji Iago Aspas (26) ametua kutoka Celta Vigo kwa dau la £7m.
- Golikipa Simon Mignolet (25) ametua kutoka Sunderland kwa dau la £9m.
- Beki Kolo Toure (32) ametua Liverpool kutoka ManCity.
- Kipa Pepe Reina (31) ameondoka Liverpool na kutua Napoli kwa mkopo. Anaungana tena na kocha Rafa Benitez.
- Mshambuliaji kinda Jonjo Shelvey (21) ameondoka Liverpool kwenda Swansea kwa dau la £5m.
- Mshambulaji Andy Carroll (24) amehamia West Ham kwa dau la £15.5m
- Mshambuliaji Fabio Borini (22) amehamia Sunderland kwa mkopo.

MANCHESTER CITY
- Beki Martin Demichelis (32) ametua ManCity kwa dau la £3.5m kutoka Atletico Madrid.
- Mshambuliaji Stevan Jovetic (23) ametua kwa dau la £22m kutoka Fiorentina.
- Mshambuliaji Alvaro Negredo (27) ametua kutoka Sevilla kwa dau £20m.
- Beki Maicon Douglas Sisenando (31) ameondoka ManCity kwenda AS Roma, baada ya kucheza mechi 13 tu tangu ajiunge na City.
- Kiungo mkabaji Fernandinho Luiz Roza (26) ametua kutoka Shakhtar Donetsk kwa dau la £30m.
- Kiungo Jesús Navas (27) ametua kutoka Sevilla kwa dau la £16m.

MANCHESTER UNITED
- Kiungo mshambuliaji Marouane Fellaini (25) ametua ManUtd kutoka Everton kwa dau la £27.5m.
 

Attachments

  • Ozil.jpg
    Ozil.jpg
    16 KB · Views: 296
Gareth Bale hana mpango wa kuondoka Tottenham hata kama hawatacheza Champions League msimu ujao.
 
- ManUtd wanataka kumchukua kocha wa Borrusia Dortmund kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson.
- Gonzalo Higuain anauzwa. Tottenham, Chelsea, Arsenal kutupa karata.
- Thamani ya Christian Benteke ni zaidi ya £30m. zaidi ya mara 4 ya bei aliyonunuliwa.
- Fabregas anafikiria wazo la kurudi Arsenal.
- Arsene Wenger hana mpango wa kwenda PSG wala popote. Arsene ndio Arsenal.
- Barcelona inamwania golikipa wa ManUtd David de Gea, ana miaka 22 tu.
- Xabi Alonso huenda akatua Chelsea simu ujao.

Aseeeee!
 
Fabregas hatumtaki tena Arsenal aliondoka kwa mbwembwe sana!!

Tunataka Alexander Song arudi tena
 
Beki Kolo Toure (32) ametua Liverpool kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Jamie Carragher kustaafu.
Kolo.jpg
 
Roberto Mancini OUT! kwa kushindwa kufikia malengo ya klabu.
 
Gareth Bale kubakia Tottenham msimu ujao kwa mshahara wa £170,000 kwa wiki.
 
Jose Mourinho anaondoka Real Madrid. Carlo Ancelotti anatafutwa kuja Real Madrid, lakini mmiliki wa PSG amesema HATOKI MTU.
 
Fabregas anawindwa na Manchester United kwa dau la £25m.
 
Arsenal wanajipanga kumchukua kipa Simon Mignolet kutoka Sunderland kwa dau la £10m.
 
Jose Mourinho sasa ndio kocha mpya wa Chelsea kwa mkataba MNONO wa miaka 4, kwa dau la £8.5m kwa mwaka. Mourinho atakuwa kocha ghali kuliko wote katika historia ya EPL.
...THE SPECIAL ONE!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom