Tragical Errors and Miscalulation of CCJ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tragical Errors and Miscalulation of CCJ!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jun 11, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwanakijiji,

  Kama kuna kituko cha Kisiasa na Uchanga (ndio natumia herufi kubwa kama msisitizo) ambacho kimetokea Tanzania na mchakato wa Siasa, ni vuguvugu la kuanzishwa kwa CCJ na matokeo yaliyotokea sasa hivi ambapo wamekosa usajili na kila Chama cha Upinzani unawaangukia na kuwaomba wajiunge kwao.

  Kwangu mimi nasema hivi, ilikuwa ni kosa kubwa sana kwa CCJ kukimbilia kutaka kusajiliwa ili kishiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutokana na sababu kuu moja: CCJ kuwa chama kimbilio kwa wale ambao wanatarajia kutemwa na CCM na ambao wanaona aibu kuingia vyama vingine au kula matapishi yao ya kudharau haki za msingi za Uraia kama vile kuundwa kwa katiba mpya au kukemea uchafu ulioko ndani ya CCM.

  CCJ walikuja kwa kujiamini sana, lakini kasi yao ilinitia shaka hasa kung'angania kusajiliwa ili kishiriki Uchaguzi Mkuu. Inawezekana kina Itikadi ambayo ni ya mkono wa kushoto wa siasa kali, lakini badala ya kukijenga chama (kama vile Mchungaji anavyotaka kuanzisha PPPT) kuanzia vijijini na kusambaza moto wa CCJ unaoambatana na Itikadi na Sera ambazo ni tofauti na CCM, CCJ waliingia kichwa kichwa mtego ule ule wa kukimbilia kutaka kuing'oa CCM kupitia Uchaguzi Mkuu na kuitikisa Tanzania hasa ukizingatia kuwa atokeo ya uchaguzi wa Wagombea wa CCM, ungezaa mateka wengi ambao wangehamia CCJ (haya ni maoni na mtazamo wangu) baada ya kutema na CCM.

  Utaona wazi Mpendazoe alikuwa Bangusilo la wale ambao wako ndani ya CCM ambao wanasubiri kikao hiki cha Bajeti kiishe wapate mshiko wao wa nguvu, ndipo waamue kuutangazia umma Uzalendo wao uko wapi.

  Rafiki yangu Mzee Mwanakijiji, umefanya kazi kubwa sana kuwatangaza CCJ, lakini pamoja na utaalamu wako, bado ulisahau kuwa CCM ina mbinu chafu na kuwa si CCM pekee ambao wangetishika kuundwa na kukubalika kwa Chama hiki hususan wakati huu wa Uchaguzi bali hata vyama vingine vya upinzani.

  Tatizo ni kila mmoja anataka kuchukua madaraka kutoka CCM, lakini hawataki kutumia muda na mbinu nzuri kukibomoa CCM.

  CHADEMA wamejaribu na vita vya ufisadi, lakini mafanikio ni madogo sana zaidi ya msisimko mdogo na mazingaombwe yaliyosababisha Lowassa kujivua Uwaziri Mkuu. CUF walijaribu miaka ile, lakini wameamua kuwa ngamia na kuingiza kichwa kwenye hema na yaelekea wanaweza ingiza nundu nzima lakini ni kwenye lile hema dogo la kuhifadhia kuni na si kwenye hema kuu.

  Sasa nikirudi kwa CCJ, sidhani kama Ajenda ya Change itafanikiwa ikiwa CCJ watakazania kusema kuwa ni lazima kwanza waingie Ikulu, ndipo tuanze kuona Cheche zao.

  CCJ inabidi irudi kambini na kujipanga upya na si kwa lengo la kusubiri wagombea huru, bali ni kutumia hizo ajenda za Change na Cheche zake kukiangusha CCM bila wao kushiriki Uchaguzi Mkuu!

  Kikubwa na hili nawapa CCJ changamoto ni wao kuja na Itikadi na Sera ambazo zitaonyesha wazi kuwa wao ni tofauti na kila mtu na kwamba hata kama hawashiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu, bado watakachokihubiri kwa Watanzania, kitaleta mabadiliko siku ya kupiga kura.

  Labda ni kutokana na kutofahamika huku kwa Itikadi yao, ndiyo maana leo hii Viongozi wa Vyama vingine vya Upinzani wanatoa mialiko na kutandika mazulia mekundu kwa CCJ wajiunge nao. Sasa sijui kujiunga huku ni kuachana na CCJ au ni ushirikiani wa kukichambua CCM ili kiangushwe.

  Cha msingi ni CCJ kuonyesha na kuegemea kwenye jambo moja kuu kama nguzo yao kuu ya kuondoa adha zinazowakera Watanzania nalo ni ujenzi wa mfumo bora wa kiuchumi ambao utainua viwango vya maisha ya Watanzania.

  Sasa hivi suala si Mkapa na Kiwira, Lowassa na Richmond au Rostam na Dowans! Sasa hivi ni kuhusu vipi Tanzania itapunguza deni na kuanza kujitegemea kiuchumi! Sasa hivi ni kushambulia uamuzi wa Serikali kukopa kwenye mabenki huku ikiongeza matumizi badala ya kupunguza matumizi na kupunguza ukubwa wa Serikali ili fedha zitumike kwa mambo ya maendeleo na maslahi ya Mwananchi.

  Uchaguzi huu ni kuhusu mishahara ya wafanyakazi, bei za mazao ya wakulima, kuneemeka kwa afya za Watanzania, elimu ya watoto wetu, Utunzaji wa Rasilimali zetu na kuwepo kwa miundombinu imara ya kuimarisha uchumi ambao utampunguzia Mtanzania kejeli za Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  Itakuwa ni makosa makubwa sana, kama CCJ wakiendelea kung'ang'ania wapewe usajili ili wachukue fomu za uchaguzi! Waachane na Uchaguzi, waanze kuwa kushambulia CCM na sera zake na kufungulia mbwa! Matunda ya kazi yao yasiwe kwa ajili ya CCJ pekee, bali yawe kwa Watanzania wote.

  Kama CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, DP na hata wanaojiita Wapiganaji ndani ya CCM ni waoga wa kuparuana na kuchafuana na CCM na Serikali yao kisa ni Ruzuku na nguvu ya Dola, basi CCJ ndio wawe attack dogs wa Watanzania kwa kuwaambia wazi kuwa Maisha Bora kwa Mtanzania yanawezekana na tuna uwezo kwa nguvu na mtaji wetu wenyewe kufanikisha hili na hatuhitaji Wawekezaji.

  Narudia tena, hili la kudai vita vya Ufisadi si tija tena, maana Watanzani wameridhika na Ufisadi na ni mfumo ulioshamiri, hivyo kutaja majina na fedha zilizoibiwa hakuleti mabadiliko yoyote zaidi ya mapovu ya hapa na pale.

  Natofautiana nawe rafiki yangu katika vita hivi vya kuing'oa CCM, nawe unalielewa hilo.

  Natamka wazi kutaka kuleta hitimisho kwa madhambi yaliyotufikisha hapa si kigezo bora cha kushinda uchaguzi, kutoa ahadi kuwa tutawafunga au kufilisi si kigezo au mali kwa Watanzania. Si kwamba haya yasifanyike, bali Watanzania hawako tayari kupiga kura ili yatimilike na ushahidi uko wazi katika Chaguzi ndogo zote na uchaguzi wa TAMISEMI mwaka jana.

  Hivyo basi kishindo cha CCJ, kimezimwa kutokana na woga wa vyama vingine ya kisiasa na zaidi ni makosa ya kujianda kivita na kimapambano kulikofanywa na CCJ ambako kumefanya leo Tendwa awapige mpira na kuwafanya waonekane ni watoto na wasiojua wanalokifanya. Yawezekana ni pupa. ashiki au midadi ya kuamini kuwa wakipata usajili, basi CCM itaanguka! Kazi hiyo si rahisi, waulizeni CUF kule Zanzibar au kina CHADEMA, NCCR na wengine.

  Ningekuwa mimi CCJ, ningejiandaa vizuri na kujijenga ili nishiriki vizuri Uchaguzi Mkuu 2015. Ningejenga nguzo imara, kutangaza Itikadi na Sera huku nikiichambua CCM na Itikadi zake na Sera na kuonyesha ni vipi hazina manufaa tena kwa Watanzania.

  It is not too late to join the fight, I extend my welcome to CCJ to join the battle, but they need to be good listeners and keep a distance from ghalasa kutoka CCM ambao wameshindwa kusimama kidete na kumtetea Mtanzania ndani ya CCM na sasa wanatafuta namna ya kuendeleza mlo na kutia samli vitumbua vyao.

  Mzee Mwanakijiji, usikate tamaa, bado ujumbe wako wa Change utafanikiwa. Subira yavuta heri na haraka haraka haina baraka! Njoo bwana tumalize kukijenga PPPT tutafanikiwa!

  Wako katika mapambano ya kuleta Mapinduzi na Mabadiliko ya Fikra,
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Asante Rev, baada ya kusoma hii, umenikumbusha, vipi kile chama chetu? or was it a joke?.
   
 3. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama kuna mahali unaniacha hoi Rev ni hapo kwenye kutangaza Itikadi na Sera kwa watu maskini wa nchi hii.... mkuu watz kwa sasa hawahitaji sana ma-itikadi wanataka mtu anayeweza kuwatoa kwenye huu umaskin hayo ma-itikadi ni yenu wasomi....aghrrrrrrrrrr
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Hii thread ni nzuri sana.....
  I need to know a lot about ccj kabla sijazungumza lolote.
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu hicho ulicho kisema ndio sawa kabisa wa TZ hawana muda wa kutaka kujua saana maitikadi wala hata katiba yani siku tukifika hatua ya kubadili katiba kuatkuwa na shughuri kweli kweli. ukichunguza sana kwa mfano tu hapo jana Mkulo akiswa akisoma Badget yake ya fedha huku watu wanakodolea macho runinga na kusikia Radio wakitaka kusikia tu mshahara umepanda? vinyaji je vimepanda na mfumuko wa bei utakuwaje na maisha yatakuwaje basi hakuan kingine wa TZ wanachotaka kusiki ni serikali kutekeleza na wakishindwa wa TZ ni kulaumu tuuuu.

   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Rev. Heshima mbele mkuu.

  Asante kwa bandiko zuri, unachokiongea mimi nakiafiki haswa pale unapoongelea maswala ya timing, timing ya CCJ ilikuwa mbaya walisubiri sana, na vile vile kama ulivyogusia kwamba huenda kuna wabunge ambao walikuwa wanataka kuliacha basi la CCm na kupanda la CCJ lakini walikuwa na woga, hawakuweza kuliacha wakiwa porini ili wapande la CCJ, wamesubiri mpaka watakapofika kituoni, kwa kuwa waliogopa wasingepewa refund ya ticket zao, hizi ni siasa za umimi kwanza.

  Kuhusu maswala ya sera na katiba za vyama nitatofautiana na wewe kidogo, niko nyumbani kipindi hiki na najaribu kuongea na watu wengi ili niweze kupata upeo wao na mawazo yao juu ya siasa za hapa nyumbani, mambo yamebadilika, sasa hivi watu hawajali tena sera za vyama, na wala hawajali mgombea anatoka chama gani haswa katika viti ya udiwani na ubunge, wanachagua/watachagua watu na siyo sera za vyama, tuombe mungu tufike salama baada ya uchaguzi wa october naamini tutaona mabadiliko makubwa sana katika sura ya siasa ya nchi yetu.

  Mwenzenu.

  MJ
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Pasco, it was never a joke. It is not an easy thing to start a party simply by saying tunataka uing'oa CCM. Chama ni lazima kiwe na taswira ya namna yake ambayo itakitofautisha na na wengine wote.

  Wengi hapa wanakimbilia kusema kuwa na Itikadi na Sera si za msingi, wanasahau kuwa bila kuwa na utambulisho na imani ya kinachoeleweka, si rahisi kujenga political base kwa Tanzania. Ama kila mtu analenga kwenye short term goals, kuing'oa CCM, lakini hawafikirii beyond kuing'oa CCM na kitakachotokea baada ya kuing'oa CCM!

  Kama miaka 20 ya Upinzani haijatupa funzo la kujifunza na kuelewa kuwa bila kuwa na Itikadi na Sera zinazoeleweka, kamwe huwezi kuwa na mvuto au uwezo wa kuleta mshikamano wa kuiondoa CCM.

  Leo hii kila mwaka wa uchaguzi, vyama viliyoko vinapigana vikumbo kugombania nani ana mgombea maarufu zaidi ili kuchukua jimbo au urais. Wamekaa chini mara kadhaa kutaka kujenga ushirika, lakini wameuvunja na kununiana.

  Turudi pale ilipoanzishwa NCCR, kila mtu alikuwa huko, lakini kutokana na kila mtu kuwa na fikra na mtazamo wake na badala ya kujenga mfumo, itikadi, sera na taswira moja na wote kushikamana, chama kika sambaratika!

  Leo hii hatuwezi kuing'oa CCM ambayo inajiita Chama cha Kijamaa na kukimbilia kuingia madarakani kumfunga Mkapa, Rostam, Lowassa au mafisadi, kisa wananchi tumechoka kunyanyaswa na kuonewa.

  Hatuwezi kuwa na uimara ilhali CCM bado ni chama kilichojijenga kisera na kiitikadi ndani ya Watanzania na ni rahisi sana kwa CCM kurudi madarakani katika muda mfupi sana na kuwafanya Wapinzani waonekane wajinga machoni pa Watanzania.

  Kuiangusha CCM, si watu wawili ambao wanaisumbua nchi, inapaswa kuingia na nguvu za kuhakikisha CCM inashindwa kihoja, kisera na kiitikadi. Leo tukishawafunga kina Lowassa je tutakifuta CCM usajili au kudai tukitaifishie mali zake kukivunja nguvu? Kama kuna mawazo kama hayo ni dhahiri basi sisi hatuna tofauti na CCM.

  Wanapodai CCM inawenyewe, ingawa kwa dhihaka tunawatukana kuwa ni mafisadi, lakini wenye CCM bado ni wananchi na kuna kundi kubwa sana la wafuasi wa CCM ambao ni safi na ni rahisi kwa wao kujipukut mavumbi baada ya kuanguka na kujijenga upya na kuwa Chama mbadala!

  Tusikimbilie kuing'oa CCM au kukimbilia Ikulu kisa eti tutaondoa onyonge wa Mtanzania kwa siku mmoja! Tusisahau kuwa iwehe vile, katika miaka 25 ijayo, CCM inauwezo wa kuwa na asilimia 45-70 ya viti vya Bunge, na hiki ni chama kimoja tu, tofauti na vyama vingine ambavyo vitapaswa kujikusanya viti viwili vitatu ili vipate umoja wenye nguvu huku kati yao hawaaminiani!

  Kule kwenye hoja ya Mtei, Shalom kanipa majibu kuwa mwaka huu, kati ya viti karibu 400 vya ubunge, CHADEMA inatarajia kupata viti 70, ambayo ni asilimia 17, CUF nao labda watapata idadi hiyo hiyo hivyo kuwafanya jumla yao kua kiwango kidogo sana juu ya theluthi moja.

  HIvyo miswaada yote ikija Bungeni, bado CCM itaipitisha na kuiburuza, na tusisahau kuwa CCM imeshaanza kujianda kujisuka upya na kujijenga kwa uchaguzi wa 2015 na si huu wa mwaka huu tena.

  Wakati nimeandika PPPT, nilitamka wazi lengo si kukimbilia uchaguzi mkuu au kuwa na malengo ya muda mfupi ambayo hayana matunda ya kudumu bali ni kujenga chama imara ambacho kitaanzia kwenye vijijiji, na kuishi na Watanzania katika kila ngazi na kadri matunda ya mahusiano yetu yatakavyokuwa yakiongezeka, ndivyo basi uimara utakapoongezeka na kutufikisha kwenye lengo la kuomba dhamana ya kuwaongoza Watanzania.

  CCM inayoogopa CCJ, si Chama bali ni kundi la watu wachafu waliokichafua Chama kwa matakwa binafsi na kukitumia Chama na dhamana ya kuongoza nchi kwa maslahi binafsi na hivyo kuendekeza Uhujumu na utawala mbovu.

  Sisi tunapaswa kuwaogopa wale CCM makini ambao wanajijenga kimywa kimya kuchukua hatamu za Chama chao, hawa ni wale vijana kati ya miaka 18-45, ambao wamesha kula yamini ya Ujamaa na Kujitegemea na si hawa wa miaka 50-80 ambao wameshaloea utamu wa madaraka na wameshindwa kumkomboa Mtanzania kutoka Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  It is all about strategy na hili ni wazi kama watu kam CHADEMA wakiwaachia kina Mnyika na Zitto ambao ni vijana wakawa Sauti kuu na nguvu ya Chama, itakuwa ni rahisi sana kwa CHADEMA na hata CUF kuweza kupata nguvu kubwa na ufuasi wa kweli kwenye sanduku la kura.
   
 8. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said Rev.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev.Kishoka,
  Mkuu wangu umeandika kitu cha kisawasawa... Pongezi sana kwani Umewaeleza wazi CCJ mahala wanapotakiwa ili kuwagusa wananchi.. Mkuu sera ni muhimu sana na nadhani kila chama kinazo na karibu vyama vyote wanafanana isipokuwa wanatofautiana vipaumbele..Lakini hili la Itikadi mimi bado sijalinunua kabisa... sijui...
  Ukitazama vizuri utagundua kwamba mtindo wa Itikadi wa Ulaya hauwezi kutumika kwetu - Haiwezekani kwa sababu sisi tupo chini ya bahari nikiwa na maana tupo minus 10 ya ktk bar. Wenzetu wanazungumzia plus wakiwa juu ya bahari hivyo kwa kila mrengo unaotumika Ulaya kwetu itakuwa ni vichekesho tu.

  Nimetumia mfano wa Plus na Minus kwa sababu sisi maskini kama maskini tukiwa tumezama inatubidi tupige mbizi za juu wakati wenzetu wanajaribu kupaa.. Kwa kila ongezeko la GDP kwetu sisi ni hatua ya kutoka -10 kwenda -6 ndio ponya, while wenzetu kwa kila Plus wao wanaongea namba ikiwa 2 itakuwa 6..na hakika mbinu za kuogelea za mfa maji haziwezi kuwa sawa na yule anayeogelea kwa raha zake.

  So why waste our time kufundisha Itikadi ikiwa haina ponya...Mkuu sisi ni maskini tunachotaka ni shibe kwanza kabla ya mahubiri. Tukiwa chini ya bahari kila pumzi ni uhai wa mtu..Ukinitupia gogo sintajali kama wewe ni mrengo gani, dini gani au rangi gani ndicho wananchi wanacholilia.. Trust me on that, na naweza weka hela yangu juu! Sisi hatuna utamaduni wa Itikadi isipokuwa kutoka ktk Umaskini,Ujinga na maradhi ndio maana tunapokea misaada toka Amerika, China, Iraq, acha mbali hizo NGO.. yaani hapa mkuu wangu hatuna dini hata nguruwe ikibidi tutamtafuna tena kwa kumsifia.

  Hivyo nadhani tuwe makini na matumizi ya hizi itkadi kwani Mzee Mwanakijiji anapodai kuwa CCJ ni Conservative hali mambo mengi wanayotaka kuyafanya ni ya Kijamaa...Hii mtawachanganya sana wananchi na hata wasomi ambao kwao piga ua Ujamaa ni KUSHOTO. Ndivyo tulivyofundishwa na sii rahisi kuyaondoa madarasa hayo kwa dealectical method - Mtakesha.

  Hata Wazungu na Waarabu walipokuja na dini zao hawakubeba Biblia au Kuran basi tukafuata mafundisho yao. Laa hasha ukweli ni kwamba waliweza pia kutuonyesha jinsi gani tunaweza kuondokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi na hadi leo tunazidi kuwasifia kwa mikopo na misaada ya NGO zao zinavyosaidia, huku wananchi wakipigwa na msasa na sura za Biblia/Kuran..Kwetu tunatafsiri misaada hiyo kwa ujazo wa kuokolewa kimwili (physical), tena tunawashukuru sana kama sii wao pengine tungesha kufa lakini wao wanahesabu kuwa neno la Mungu limefika Kiroho...Ndivyo tulivyo mkuu wangu.

  Hakuna mtu aliyepinga chama kuundwa na sera zake ambazo ni tofauti na vyama vingine, lakini hizi sera ni lazima ziwaguse maskini zaidi ya ahadi.Wajisikie kama wao ni sehemu ya sera hizo kama mafundisho ya dini. Binafsi nangana na maelezo ya Mwanakijiji hasa pale alipogusia UFISADI, rushwa ni sehemu kubwa ya maisha ya wananchi lakini ni KERO kubwa sana kwa Watazania walio wengi..Binafsi bado naamini kabisa kwamba Ufisadi bado unauzika sana tu. Mrema mwaka 1995 na Mtikila walipata sifa kubwa ya Upinzani kwakutumia siasa nyepesi kama hizi. Siasa ambazo zinaeleweka na wengi (Watu na Mazingira) kiasi kwamba wananchi walishachoka kuona Wahindi wakichuma kupitia migongo yao.

  Halafu hata Mkapa, unajua kwamba alipata sifa awamu ya kwanza kwa sababu alitupiga changa la macho kwa kufanya mengi ambayo akina Mrema na Mtikila waliyapigia siasa! - Mkapa lijaribu kuwabana sana Matajiri na Wahindi wasiolipa kodi, akaweza kuwatia ndani watu kibao kwa kuepa kodi Na akarudisha Uhusiano mkubwa na IMF jambo ambalo wasomi wengi walitaka kuona kwa sababu moyo wetu wa Uchumi ulisha simama kabisa. Kila Mdanganyika alimkubali Mkapa panoja na kwamba kulikuwa na makosa mengi ya Kiuchumi..Hizi ndizo siasa za Bongo, You gut to feel them..

  Tatizo kubwa naloliona ktk swala la Ufisadi ni pale tunaposhindwa kuelewa kwamba hili sii angamizo la baadhi ya watu bali ni angamizo la chama kizima cha CCM..Hapa mkuu wangu CCM hawatalala, naweza kusema vita hii haiwezekani na wapo radhi kumaliza wananchi wote kabla wao hawajafikishwa mahakamani..Sijui kama wenzangu mmeshafikiria hilo. kwa hiyo vita hii sii rahisi wala mchezo wa kuigiza wataondoka watu...Ebu Pitieni (google) Hutuba ya mwisho ya JFK kuhusiana na - The Secret Society... Jamani vitu hivi vipo na kwa udogo wake vinaweza kuwa Tanzania pia.

  Sisi tulipokuwa tukipigania Uhuru kama tungeonyesha dalili ya kuwafikisha mahakamani Waingereza yaani kitu chochote kinachohusiana na kuua iwe kwa haki ya makhakama au vyovyote vile ni sawa na kutangaza vita. Uhuru tusingeupata Waingereza wangepigana hadi mwisho.. Kina Mandela na Mugabe ilibidi wakubali kuwasamehe Makaburu ndipo Uhuru ulipowezekana kinyume cha hapo ilikuwa haiwezekani. CCM watapigana hadi damu ya mwisho kuhakikiha hawafikishwi mahakamani. Tofauti na kinaMandela, kina Che na Wanamapinduzi wengineo wote wa silaha ilifikia vile kwa sababu suluhisho la dialogue au mahakama ilishindikana. Sasa sidhani kama tutaweza kuweka dialogue na viongozi wa CCM wakubali kufikishwa mahakamani!.

  Nikirudi kwa Chadema, Hawa jamaa zetu wamejaribu sana tu ndani ya bunge, ktk vyombo vya habari na hata majukwaani kwani ndiko Mbowe alipopata Umaarufu wake, lakini wameshindwa kuleta matunda ambayo wananchi waliyategemea kwa sababu hawana support ya wananchi wenye njaa. Chadema walimlazimu JK kusema tumwache mzee wa watu astaafu, tukakaa kimyaaa - tumekubali. Pinda akasema yupo tayari kusulubiwa yeye kuliko kukisambaratisha chama - Tukazidi kupooza..Kina Sitta, Malecela, Msekwa, Makamba wote hawa wamekuja na maneno mazito dhidi ya kukiadhibu chama kutokana na Ufisadi wa baadhi ya viongozi ambao hata kuwaondoa ndani ya chama imeshindikana. This is what we are facing!

  Na ajabu ya Mungu, hao Chadema waliosimamia issue nyingi bungeni na hapa JF hata shukrani toka kwa wananchi hawakupata, ila imekuwa kama vile wali wahabarishwa wananchi ktk mchezo wa kuigiza na Kibonde wa Clouds...Kwa nini Chadema walishindwa! sidhani kama wengi tumejiuliza hilo isipokuwa kulaumu ugonvi uliotokea ndani ya chama ambao binafsi naamini ulipangwa kukisambaratishachama.. Na wengi wetu tuliununua kwa gharama kubwa..na sasa tunachuma tulichopanda. CCM ni chama Kubwa, ina kila mbinu ambazo hata siku moja Msije wa underestimate.

  Nitaendele kusisitiza kama wapo kweli wapiganaji na wenye nia ya kuing'oa CCM, the ONLY way ni kuunganisha nguvu zetu - WATU. Hata ikibidi vyama vya Upinzani vivunjike vyenyewe muanze Upya ifanyike, lakini msikae mkisubiri CCM kusambaratika - Haiwezekani, watasambaratika watu na sio chama CCM. Wakati huo huo naiona Light at the end of the tunnel, INAWEZEKANA kabisa kukishinda chama hiki ktk Uchaguzi mkuu.
  Kazi ilobakia ni kwenu Wanasiasa.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  kusema kweli, kuanzishwa kwa CCJ kulinihuzunisha sana! na hasa baada ya kugundua kwamba kilitaka kugombea uchaguzi mwaka huu. Hivi kuna mtu ana kumbukumbu yoyote katika Bara la Afrika (au labda pengine popote duniani) chama kipya kabisa kinaanzishwa, kinasajiliwa na baada ya miezi sita kinaingia kwenye uchaguzi na kushinda? Mwaka 2002 NARC ya Kenya ilifanya hivyo, lakini huo ulikuwa ni muungano wa vyama kadha vilivyokuwapo tayari.

  Huzuni yangu ya kuanzishwa CCj ni kwamba kilikuwa kinaongeza tu utitiri wa vyama, kitu ambacho serikali ya CCM yenyewe ilikuwa inapendelea na pengine yenyewe huvianzisha vingine. Kuna baadhi ya vyama sasa ndiyo navisikia kama vipo kwamba vilikwisha kuandikishwa ingawa sikusikia kabisa masakata yao ya kuhakikiwa na Msajili. Hata hivyo kukataliwa kuandikishwa CCj kunatokana na CCj wao wenyewe kutokuwa makini.

  Watu walioanzisha CCJ angalau wangetumia busara, uwezo, na nyadhifa zao kuunganisha vyama vilivyopo na siyo kuanzisha kingine! Vyama vingi vinazidi kuwavuruga wapenda mageuzi wa kikweli kweli na kuviona kama dhihaka kubwa!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Rev nakubaliana na wewe kwa asilimia zote..Kwa kweli hawakujipanga vya kutosha kama hawataweza kujoin forces na chama chochote kingine cha upinzani basi wajipangea vizuri ili wapate usajili ili 2014 na 2015 washiriki kwenye chaguzi otherwise tunawakaribisha sana CHADEMA mlango uko wazi tena mkubwa huo!
   
 12. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Swali la pembeni mchungaji.Hivi kuna mwana CCM under 45 ambaye sio opportunist?kwa nini kijana wa miaka 18 aipende CCM?maana huyu amezaliwa wakati Mwinyi raisi,ameenda shule wakati mkapa raisi,probably anajiandaa kuingia chuo kipindi cha kikwete.
  Kijana huyu kama ni mtanzania wa kawaida ana sababu gani ya kuipenda CCM?kwa kuwa ilimlipa babu yake mafao East africa?kwa kuwa mzazi wake mshahara unatosha kulipa mahitaji ya familia?!
  Kijana huyu aipende CCM kwa sababu CCM hii imefanikiwa kumtoa kwenye lindi la umasikini?
  Sioni sababu ya Kijana wa Kitanzania kuipenda CCM kama haimfaidishi kwa njia moja au nyingine.CCM imeoza beyond repairement.hata kabla ya ufisadi CCM ilisimamia sera zilizotuijaza umasikini na Status quo za kipuuzi.
  i guess ndio maana jamaa wa JF tunaitwa outsiders,we are too smart for CCM.
  regarding CCJ,hawa jamaa wamejitahidi,maana Chadema wali-ride na issue ya ufisadi hadi ikaanza kuloose touch na maana halisi,CCJ wanasaidia kuchangamsha siasa za nyumbani.Nia yao haiko clear.Lakini nitawapa benefit of doubt.
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  CCJ ni KINA NANI?
   
 14. b

  buckreef JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lugha za fundamentalists wa kisiasa, kama CCM hawajafanya chochote mbona mnashindwa kuwang'oa? CCM kama chama hakina ubaya wowote na malengo yake ni mazuri sawa tu na alivyokuwepo Nyerere.

  Kuna wilaya na halmashauri ambazo zinaongozwa na CHADEMA, mbona hatuoni mabadiliko yoyote huko?

  Kuna kundi la vijana ambalo linataka kuichukua CCM kutoka kwa viongozi waliokumbatia ufisadi na kuirudisha kwa wananchi walio wengi. Wewe unaweza kubeza lakini bado hutoi jibu maana hata huko uliko nako kunanuka, it doesn't matter ni kinyesi cha nguruwe au punda, vyote ni vinyesi tu.
   
 15. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  M.M.Mwanakijiji heshima mbele!

  Hututendei haki hata kidogo, naona unaingia unasoma mabandiko unagonga thanks (za kweli na za kukebehi) baada ya hapo unaingia mitini, mzee tueleze, what is CCJ, why now nini matarajio yao, nani mgombea uraisi...na zaidi ya hapo CCJ ni kina nani?..

  Rudi utueleze.

  Mwenzenu

  MJ
   
 16. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  0.02...well said kamanda.
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kimweri,

  Kuna struggle ya generations Tanzania ambayo ni kati ya Traditionalist na kwa kiasi fulani nusu ya baby boomers dhidi ya nusu ya baby boomers, Generetion X and Y na mpaka hawa wa sasa wa Y2K. Ndiyo kuna waliosoma enzi za Nyerere, kuna waliamka tangu Mwiny na hadi sasa Mkapa.

  Wanaotuhujumu ni wazee, ambao badala ya kufurahia legacy yao ya kuwa walipigania uhuru, wao wanataka kuwa ndio matajiri wa kwanza wa kiafrika wenye kumiliki kila kitu na kufanya maamuzi ya kila kitu. Upeo wao ni ule wa kupigania uhuru na mkoloni na si wa sisi vijana na hata watoto wetu ambao wamekuwa na kuyaona ya ulimwengu mpya.

  Mfano, pamoja na kuanguka kwa Ukomunisti wa Urusi, Ujerumani Mashariki na hata kuanza kwa Ukomunisi endelevu ulioko Cuba na China ambao umezifanya nchi hizo kujipima tena kiitikadi na kuziingiza nchi zao kwenye ushindani wa kiuchumi, sisi bado tunang'angania mfumo uliotuletea Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1971 na unatumika kwa nguvu kukandamiza Wananchi na kutishia watu.

  Shalom kanijibu na kusema yaliyowatokea kina Lamwai, hayo ni matokeo ya mgongano wa kifikra na generation. Leo hii naamini ukiwaachia kina Nape, January na vijana wengine wa CCM, kama Kibunango, watakiendesha CCM kwa ufanisi zaidi na hawatatumia woga wa Baba na Babu zao wa kutumia nguvu ya dola.

  Nikirudi kumjibu Mkandara hapa kwa maswali yake ya Itikadi, Tanzania ya leo si Tanzania ya mwaka 1970. Tuko katika ulimwengu wa luninga, utandawazi, uwekezaji na soko huria. Tuko mahali ambapo mipaka ni michoro isiyo na maana tena, kutokana na jamii yetu kuingiliana na jamii nyingine na mapokeo mengine ya nje. Nasema hivi nikiwa najenga msingi mzima wa kusema ni kwa nini kuna ulazima wa vyama si kukimbilia kutamka Sera (policy) lakini pia ni lazima vijijenge ki-Itikadi (ideology) na ni kwa ajili ya mshikamano na mafanikio ya Chama kama kikundi na ndipo waweze kujioanisha na jamii na kupokelewa na jamii.

  Turudi nyuma mwaka 1966, tulikuwa na kina Mtemvu, Kambona, Babu, Kasanga Tumbo, Nyerere na wale wengine wote ambao walikuwa ndani ya TANU. TANU kilianza kama chama cha kupigania UHURU na kumn'goa mkoloni. Ilipofika mwaka 1967, TANU ikabadilisha mkondo na kutangaza wazi kuwa wao ni Wajamaa na kuanza kuuza ujamaa kwa kuwafundisha Watanzania maana ya ujamaa na unavyoendana na maisha ya kijamaa.

  KIna Mtemvu na Kambona ambao walikuwa mabepari au makabaila na kukumbatia Itikadi tofauti na Ujamaa wa Nyerere, badala ya kujijenga na kuleta upinzani wa kihoja, wakaishia kutimuliwa kama Wahaini na TANU ikaamua kuwa dikteta na kuunda mfumo wa chama kimoja na kuifanya Tanzania iwe nchi ya kijamaa. Ndio kulikuwa na ulazima wa kufanya hilo enzi zile, ingawa kuna mengine yaliyofanyika hayakustahili.

  Leo hii jamii yetu imebadilika, kwa mujibu wa CIA, zaidi ya nusu ya Watanzania wako chini ya umri wa miaka 18, iwe wako mijini au vijijini, upeo wao pamoja na hali halisi za maisha ni tofauti sana na wazazi wetu.
  https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html

  Wao leo hii wako tayari kupokea mafundisho iwe ni ya kijamaa, ukomunisti, ubepari, ukabaila kwa namna nyingine tofauti na Wazazi na Mababu zetu kwa kuwa dunia yetu inasonga mbele na sasa hizi kinachopiganiwa ni uwezo wa nchi kujijenga kiuchumi na si kisiasa.

  James Carville wakati anamsaidia Bill Clinton kugombea alisema uchaguzi ule ulikuwa ni "economy stupid" lakini ilikuwa ni kwa mkao mwingine wa Kibepari lakini kupitia Chama cha Democrat na si Ubepari wa Republican
  It's the economy, stupid - Wikipedia, the free encyclopedia

  Leo hii, vyama vya siasa Tanzania vinashindwa kujenga hoja na sera za msingi za kisiasa ambazo zinalenga kwenye kuujenga yuchumi zinakimbilia kusema wao kazi ya kwanza ni kuing'oa CCM< lakini hawatamki wazi kuwa wakiingia madarakani watawezaje kuendesha nchi, uchumi na mfumo wake utakuwa ni wa namna gani na utaleta manufaa gani kwa wananchi na Taifa zima.

  Alichofanya Nyerere mwaka 1967 ni kuuza Ujamaa na kuufananisha na mfumo wa maisha ya kiafrika, nasi tukaafiki. MKandara umeuliza mahali iweje mbona Wachagga wako endelevu? mimi nitaongeza na Wapemba na katika kukujibu, nitasema je tumetafakari ni mfumo gani wa kisiasa (ukweli ni kuwa mfumo wa siasa hutegemea mfumo wa kiuchumi na vice versa) na kiuchumi ambao unaweza kuwafaa Wachagga na Wapemba ili wakatuongoza katika uzalishaji?


  Kwa Mchagga na Mpemba, Ujamaa wa mwaka 1967 ni ukandamizaji, leo hii wakimsikiliza Mapesa Cheyo na sera za Utajirisho, hawawezi kumuelewa watatajirika vipi kama hakuna Itikadi inayojiuza na kusema katika Ubepari, Tanzania itajiondoa katika Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  Kama tuliweza kujeng itikadi ya Ujamaa wa Kiafrika au zaidi wa Kitanzania, tutashindwa nini kujenga Itikadi iwe ni ya Kibepari au Kikabaila na kuifanya ya Kitanzania na si ya Marekani au Urusi na kuifanya itufanyie kazi kama vile Ujamaa ulivyotufanyia kazi?

  Itikadi ni imani, Wakristo tunaamini katika utatu mtakatifu na kukiri imani, Waislamu itikadi yao kuu ni zile nguzo tano za uislamu. Lakini katika dini zote, kuna amri (sera) zinazosema usiibe, usiue, usizini, na kadhalika.

  Watanzania wanapaswa kufundishwa Imani za hivi vyama na si sera pekee. Lengo ni kuhakikisha kuwa waelewe katika dunia ya leo na mfumo wa kisasa wa kiuchumi, hakuna lisilowezekana.

  CCM wanang'ang'ania Ujamaa, kwa maana hakuna Mjamaa mwingine aliyekuja na kuonyesha Ujamaa au Ubepari ni bora kuliko CCM. CCM wanasera za maisha bora kwa Mtanzania, CUF wamesema hilo hilo, na CHADEMA wanasema hilohilo, swali ni hili, je Maisha bora haya yatapatikana katika mfumo gani wa kiuchumi na itikadi gani za kisiasa ambazo Mtanzania ataweza kujitambulisha nazo?

  Na kwa kumalizia, Itikadi ni taswira halisi ya Chama, bila kuwa na Itikadi inayoeleweka na kukubalika kwa wote wanaojiunga, matokeo yake ni hili la utitiri wa vyama kutokana na kila mtu kuwa na mfumo wake au sera zake lakini hakuna msingi wa Kiitikadi ambao ndio uti wa mgongo wa Chama.

  PPPT, kitakapokuja, kitakuwa ni chama cha Kijamaa endelevu, si Ujamaa wa TANU, Democrats au KGB, itakuwa ni Ujamaa wa ki-PPPT ambao utashabihiana na Mtanzania wa leo na Mazingira ya leo. Mkandara hupenda kuniambia Watu na Mazingira, basi sisi tunaunda chama na Itikadi ambayo itakuwa ndani ya Watu na Mazingira.

  Mwisho, naomba nimnukuu Omar Ilyas kwenye makala yake kwa kitu ambacho hata Mwalimu Nyerere aliking'amua kuhusu Itikadi.
  omarilyas
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev.Kishoka,
  Mkuu shukran tena na tena. Hakika mawazo yako yametulia sana tu..Ila nakuomba unielewe kwamba nachozungumzia mimi siii maswala ya kesho..Mimi natazama uchaguzi wa October na kuwatazama Watanzania hali zao zilivyo. Umemsoma Zitto akitoa taarifa ya CIA ikisema ni zaidi ya asilimia 83 ya Watanzania leo wako ktk Umaskini na kati yake zaidi ya asilimia therethini wako chini kabisa ya pato la dollar moja kwa siku..
  Mkuu hawa watu ni wafa maji yaani tumekwisha kunywa vikombe na tunazama..

  Watu kama hawa hakuna muda wa kuwa preach Itikadi, meaning mtu anayezama na kufa maji hukuna muda wala sababu ya kuwambia jinsi ya kuelea kwa kuogelea kichura, sijui how to save energy and breathing ili kuogelea ili afike nchi kavu...Mbinu hizi zote na zaidi ni nzuri sana kwa mtu aliye salama lakini sii kwa mfa maji.

  Anachotaka kuona huyu mfamaji ni support ya mkono wako, kamba, mti au chochote cha kumwokoa..Nguvu kubwa ya maamuzi unayo wewe.. Hii ndio position yetu, sikatai kabisa vyama vyetu kuwa na mrengo wa Itikadi ambao unaendana na WATU na MAZINGIRA yetu. Hili ni muhimu sana lakini baada ya kukolewa.

  Na hapa ndipo mimi siku zote huona makosa ya bajeti yetu na mikakati yote ya kiuchumi tunapojaribu kuweka sera za maendeleo bi,a kujali hali tuliyokuwa nayo..Maadam Taifa ni maskini na linaendelea kuzama kinachotakiwa ni sera za kuokoa maisha ya wananchi kwanza.Hizi habari za Ujamaa na Ubepari tuziweke kando tufanye vitu vinavyoweza kutuondoa katika hali hii kisha tukiwa safe ndipo itikadi zinaweza kufanya kazi kwani mara zote Itikadi ni tofauti ya Ibada na vipaumbele..

  Trust me again, mtu akiwa anazama maji (kazidiwa) hatajali ni nani aliyekuja kumwokoa iwe Bepari au Mjamaa.. akisha okoka ndipo mwambie huyo mtu kaokoka kwa nguvu za nani..Right now, hakuna siasa ila nani ataweza kumwokoa Mtanzania... na ndio maana tuna grab anything on site hata iwe ujani kiasi kwamba wasomi kama nyie mnashindwa kuelewa na kuuona Ujinga wa Mtanzania.

  What I hate more ni pale wanasiasa na hasa vyama vinapokaa kama yule mzungu aliyekuwa akichukua picha ya mtoto wa Kiithiopia akiliwa na scavenger - Vulture....ili kuonyesha Unyama wa Haile Selassie (Bepari). Na alipokuja Mingistu Haile Mariam Mjamaa ndio akawamaliza kabisa (he made it worse) na itikadi zake ambazo hazikushabihiana na WATu au mazingira walikuwepo..
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bob Mkandara,

  Ya Oktoba 2010, si wengine tulianza kuandika na kuwaomba Upinzani waanze kujijenga tangu sijui 2007? Mkuu umesahau ile thread ya Focus 2010 au ya CHADEMA must reform? Tumelia wee, tumetoa maoni, tumekosoa tumejenga hoja, mpaka na kujitolea lakini kama sikio la kufa vile, yakaingia sikio moja, wengine tukajibiwa kwa dhihaka na sasa Oktoba 2010 iko ndani ya kumi na nane, leo watu wanagutuka na kusema tujikusanye! Laiti wangetusikiliza miaka mitatu iliyopita na hata wengine tulipoandika Waraka wa Mchungaji, na kama wangeufanyia kazi na si kujiona kuwa wao ni wajuzi, leo hii wengine tusingeaza kuongelea 2015, tungeongelea jinsi ushindi utakavyonoga Novemba 2010.

  Umeona jinsi Robert Green wa Uingereza alivyofungwa kijinga leo hii na Clint Dempsey? Basi ndio hivyo hivyo Upinzani wa Tanzania umeshafungwa na CCM!

  Hivi kuna mtu ambaye ameshakaa chini na kujiuliza ni wehu gani uliomwingia Mzee Mwanakijiji akaachana na watu wengine wote iwe ni CHADEMA au Wapiganaji wa CCM na kukimbilia CCJ? Jibu lake ni rahisi sana, "tumepuuzwa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha, sasa kilichobakia ni kutafuta wengine wapya tufanye nao kazi ambayo waliokuwa na uwezo wa kuifanyia kazi, juhudi za maarfia yetu na Uzalendo wetu, wakaamua kutupuuza si wasikivu na wataendelea kukwama mpaka siku watakapoamua kuwa wasikivu"!

  Hili la Oktoba Bob Mkandara, si tulianza kulijengea hoja tangu Disemba 21 2005? Au umesahau yale ya S C R E W Muungwana, Ajizi ya kibuge, Paukwa Pakawa, Meremeta, Nami nikawaona Wapanda farasi wanne?

  Kama mwaka 2008 tulikuwa tunawabembeleza Upinzani wajiandae kuchuka viti vya TAMISEMI 2009 kama njia ya kuhakikisha kuwa wana uwakilishi wa kutosha kudhibiti masanduku ya kura na hata kuwa na upper hand kwenye kuhakikisha daftari la kupiga kura ni sahihi na si CCM pekee wenye kuwa na uwakilishi mzima na wao Upinzani (especially CHADEMA) wakadai wao lengo lao ni Ikulu na Bunge ambalo kwa utabiri wa Shalom watapata sana sana viti 70, je unatarajia ni vipi leo watakuwa tayari kumsaidia huyu masikini?

  Mikakati ya kuwasaidia washinde imetolewa, wao wanaipuuzia, kwa nini basi tupoteze muda kudhani Oktoba 2010 kutatokea miujiza?

  Hata huko CCM kwenyewe ambako tulikuwa tunaombea kuwe na mapinduzi baridi, kila mtu kageuka na kukumbatia chama, si Wapiganaji au babu yao, wote wanatetea ulua na si kumtetea Mtanzania.

  Wengine tumelonga mpaka kuanza kuwindwa, ni sisi attack dogs ambao hatutegemei ruzuku ya chama au Serikali, lakini tuko tayari kuuza Itikadi na Sera na kutoa mbinu za medani kushinda vita. Sasa kama tunaendelea kupuuzwa halafu leo tunang'amua kuwa juhudi za kutaka kazi ambayo ingeanza kufanyika miaka mitano iliyopita ndio leo tunakurupuka na kudai tujizatiti? Ndio maana namwambia Mzee Mwanakijiji CCJ nao wanapotea maboya kwa kung'ang'ania kukimbilia uchaguzi mkuu huu wa mwaka huu.

  Ikitokea Upinzani ukapata japo theluthi ya viti vya bunge, hiyo itakuwa Alhamdulilahi, lakini tuwe tayari na kuwa wepesi wa kuanza kujiandaa kwa 2015.

  Leo Kikwete katamka kuwa sehemu kubwa za ahadi za uchaguzi 2005, zimetimia kama vile kujenga barabara, shule na vituo vya afya na bado atawaambieni kuhusu Kilimo Kwanza!

  Sijakata tamaa ya kuwaondoa CCM chafu, bali ni lazima niwe realistic, kuwa kazi hiyo kwa mwaka huu ni ngumu kwa kuwa tumechelewa kufanyia kazi na kujijenga ipaswavyo.
   
 20. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na hapa pa kutothamini itikadi ndio kunapowamaliza watanzania. Itikadi ni muhimu katika maisha/mfumo wa kisiasa kama ilivyo imani/dini kwa maisha ya kijamii ya binadamu. Kutothamini itikadi ni kutoa nafasi kwa siasa za longolongo/siasa za matumbo/populism.....Itikadi ni muhimu lakini lazima iwe ni itikadi ya dhati na sio ya kuvutia watu tu kama ambavyo CCJ walitaka kufanya na Ujamaa na kujitegemea. Na hapo ndipo ugomvi wangu na CCJ unapoanzia. Itikadi ka ya Ujamaa na Kujitegema na jina la Baba wa Taifa ndio misingi ya Utanzania wetu na ni HARAMU kwa mtu yeyote kutumia kama mtaji wa kulinda maslahi yake ama ya kundi fulani....

  omarilyas
   
Loading...