Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Wakati nikiwa katika mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa nilikutana na kisa hiki ‘laivu’ katika maeneo ya kituo kimoja cha polisi.
Askari mmoja wa kike (WP) alikuwa akilia na wenzake wakijitahidi kumbembeleza, lakini nilipowauliza baadaye wenzake wakasema: “Analia kwa sababu ameondolewa kwenye kitengo.”
Awali sikuelewa, lakini wakanielewesha kwamba, askari huyo alikuwa wa usalama barabarani na sasa ameondolewa na kurejeshwa kwenye dawati la kawaida (General Desk au GD), ambako aliona kama ‘ametupwa’.
Ilinishangaza kuona askari, ambaye wakati anaajiriwa hakuomba kupangiwa kitengo chochote, leo analalamika na kumwaga machozi kwa kuhamishwa kitengo cha trafiki ambacho alipangiwa kutokana na utaratibu wa kazi.
“Wanapata fedha nyingi sana, siyo sisi ambao tuko hapa kwenye madawati…” alisema mmoja wa askari hao wa kike baada ya mwenzao kuondoka.
Mwingine akadakika: “Yule mwenzetu ... ISOME ZAIDI NDANI