Trafiki waanza rasmi kukamata magari yote yenye taa za urembo, Sports Light

Sheria za mdomoni kazi sana... na pia kumbe walishapanga hadi fine ni 30,000/= ?duh
 
Sheria za mdomoni kazi sana... na pia kumbe walishapanga hadi fine ni 30,000/= ?duh
Uwekaji wa taa hizo ni kinyume cha Sheria ya Usalama Barabarani Kifungu cha 39 Sura ya 168, ambacho kinaeleza matumizi ya taa. iyo sheria ipo toka kitambo haijatungwa jana mkuu hayo ma taa yanaumiza sana..
 
Mbona Mwendo kasi ni Sheria ila misafara ya Raisi na wengineo spidi yao ni hatari... pia askari ndio wanavunja sheria kila siku huwa nashuhudia sana natamani niwe nawapiga picha ikitokea nimeruhusiwa na kizawadi kama kitakuwepo..

Hizo taa kama zinazingua mtu akiwasha fumba macho tu hahaha Nachojua Tinted ya mngao kama wa kioo na Ngao kubwa kwenye magari yamekatazwa kisheria... nadhani na zile horn za Tarumbeta za kuimba kama ile ya ''Fungua geti fungua geti msela anapita'' au ile ya ''Honi ya kwanza ya pili nipo Morogoro''
 
Kweli wakamate tu. Yaani ukiwa masafa marefu unakutana na madereva malimbukeni wanakupiga taa mpaka unapoteza uelekeo. Nilikuwa nashuka Sekenke nikitokea Singida, jamaa akawa anapandisha akitokea Shelui. Kila nikimpa ishara apunguze mwanga haelewi. Nikajua ni gari kubwa na labda jamaa ana matatizo. Nikasimama, kinanipita, kumbe kiverosa! Nilichukia sana. Naangalia niliposimama, bado kidogo ningegonga jiwe kubwa.
 
04487e57449eda6996d07b0a4ec25387.jpg
 
Leo nimeamini. Kila member JF ana gariiiii
Wee,thubutu,kwenye mitandao ya kijamii kila MTU ana akili,ni tajiri,msomi,anaelewa sana,ana familia bora,anatoka familia ya kishua,anaishi maeneo yenye hadhi kubwa,ana marafiki matajiri/wasomi/wana siasa maarufu,anaenda supermarket kununua mahitaji ya kila siku ya chakula,sio kariakoo,anamiliki simu latest version kabisa nk.Wana jf na alike sio watu wa mchezo mchezo ati,ukibahatika kumfahamu anavyochangia kwenye social media hizi na real life analoishi utachoka kabisa.Bora sisi tunaoishi vijijini baiskeli ndio mpango mzima.
Polisi/Trafiki kazeni buti,shughulikieni hawa wenye taa za maudhi barabarani bila kujali vikelele vichache vya humu,kwani wachangiaji wengi humu wanaafiki mnachotekeleza.
 
Kweli wakamate tu. Yaani ukiwa masafa marefu unakutana na madereva malimbukeni wanakupiga taa mpaka unapoteza uelekeo. Nilikuwa nashuka Sekenke nikitokea Singida, jamaa akawa anapandisha akitokea Shelui. Kila nikimpa ishara apunguze mwanga haelewi. Nikajua ni gari kubwa na labda jamaa ana matatizo. Nikasimama, kinanipita, kumbe kiverosa! Nilichukia sana. Naangalia niliposimama, bado kidogo ningegonga jiwe kubwa.
Hizi taa watu wengi hawajui namna na mahali pa kuzitumia.. mie naona sawa tena sawa sana.. eti wanaota "Jua" akili ndogo kabisa.. mjini mtu anawasha sport lights za nini sasa..
 
HAPANA, SIO HATARI.

UNAFAHAMU KUWA, MFANO SAFARINI AU KIPINDI CHA MVUA, ZILE HUSAIDIA SANA.?

KWA MTU ANAESAFIRI MARA KWA MARA HIZI ZINAMFAA MNO!
Wenzio wanawasha hizo anatoka Segerea anaenda Buguruni, barabara yenyewe nyembamba......na wengine humu wanazo na wanafurahia kusumbua madereva wengine. Inabidi baada ya kipimo cha ulevi tupimwe na akili pia.
 
zipigwe tu marufuku. make kuwa watu wengine awajui kuzitumia taa za kutumia porini wanazitumia town zinatuumiza bhn
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom