Trafiki wa Kateshi, utaratibu wenu wa usimamizi ukoje?

Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,499
1,582
Nimesafiri kwa kuendesha gari toka Mwanza to Arusha kupitia Singida.

Nilipofika Kateshi pembeni ya kituo cha polisi, askari wa usalama barabarani akanisimamisha na kutoa simu yake na kuonyesha picha ya gari nyeupe ambayo haionyeshi namba na haionekani vizuri na kuniambia nimeover speed eneo Gehandu.

Nikamuuliza mbona sikuwaona hao walionipiga torch, akasema alikuwa amevaa kiraia.

Je una uthibitisho gani kuwa hapo nilipopita ni kwenye speed limit? akawa kimya na kuniambia niendelee na safari.

Je polisi mnautaribu wa kumuweka mtu njiani kazi yake kupiga picha magari na kuzituma whatsapp?
 
Ndiyo shida ya kuwapa kiwango cha ukusanyaji faini kama wako mahakamani na wasipofikisha kiwango hawana kazi...Unadhani watafanyaje sasa?
 
Polisi wajiangalie sana. Mimi juzi walinipiga fine eti kisa sijafunga mkanda. Hilo nalo ni kosa jamani?
 
Siku hizi Hawa traffic wamehamia kwenye torch,ndio sehemu iliyobaki ya kipato mjini siku hizi 98% watu wameelimika documents zote zipo kamili mkanda umefunga leseni Ipo,insurance, fire extinguisher, n.k, kwa hiyo mjini hakuna hela kilichobaki ni torch tu wanakubambikizia kwa sababu Una haraka na upo safarini unaona ni heri kulipa kuliko kupoteza muda na kujibishana.
 
Halafu polisi wa Manyara wanafurahisha sana, kuanzia wa pale Dareda, Endasaki, Maeneo ya Tumaini Hospital na pale kituoni Katesh. Hawa wanaenda na viti kabisa kwenye post zao, Gari iko speed anasimama ghafla na kuisimamisha.

Ni majipu. Tochi za uongo ni Ukipita Maisaka kuelekea Magugu na pale Minjingu hatari sana.
 
Ni kosa ndio, ila kufunga mkanda ni kwa usalama wako zaidi dada nahs haukwenda driving school
 
Halafu polisi wa Manyara wanafurahisha sana, kuanzia wa pale Dareda, Endasaki, Maeneo ya Tumaini Hospital na pale kituoni Katesh. Hawa wanaenda na viti kabisa kwenye post zao, Gari iko speed anasimama ghafla na kuisimamisha.

Ni majipu. Tochi za uongo ni Ukipita Maisaka kuelekea Magugu na pale Minjingu hatari sana.

Hakuna eneo lina traffic wengi kama kutoka babati mpaka makuyuni! Hiyo barabara mchana inakera
 
Back
Top Bottom