Alwaz
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,055
- 10,723
Kaitka miaka hii michache nyuma maendeleo ya teknolojia yamepelekea kutengenezwa taa za vimuli vimuli kwenye magari ambazo nionavyo mimi ni hatari kwa maisha yetu.
Nazungumzia zile taa za kuashiria kupinda au kusimama kwa vyombo vya moto. Taa hizi sasa zimekuwa zikitumika ovyo kiasi kwamba ishara zote zilizoziklitumika mwanzo hazina maana. Watumiaji wake huwa wanaona ni mapambo lakini zinaingiliana sana na ishara halisi za matumizi ya vyombo hivyo.
Unaweza ukawa nyuma ya chombo cha mwenzako na usijue kipi amekusudia ni kupinda kulia au kushoto au ni kusimama..
Nimewahi kushuhudia ajali iliyotokana na vimulimuli hivyo. Nionavyo mimi bila utaalamu wa usalama barabarani
Taa za kuashiria kupinda kulia na kushoto ziwe ni njano. Taa za kusimama ziwake maeneo hayo hayo lakini nyekundu.
Honi nzito sana iwe ni za malori makubwa, ukisikia bila kugeuka unajua semi linakuja hilo upishe mbali.
Honi za dala dala ziwe nyepesi kidogo
Honi za mabasi ya abiria ziwe nzito lakini nyembamba. Ukisikia hata gari haijajitokeza unajua basi la mikoani hilo linakuja na kadhalika.