Trafiki mataa Karume acheni uonevu

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,764
Naomba kamanda kuwachunguza hawa matraffic mataa ya Karume hasa wakina dada matraffic anakutoa kwenye foleni anakupeleka kibandani hujui kosa lako anakupeleka kwa wakubwa wao yeye anaondoka unabaki kujiuliza nimefanya nini hutoki hapo mpaka uache kitu.

Anae bisha aenda akasimame pale kwenye vibanda vya mabegi Karume ajionee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na zile taa pale hazionekanagi vzuri..unaweza jikuta umepita kumbe siyo kijani
 
Dunia nzima hakuna watu dhulumati kama hawa jamaa. Siku ya mwiso nikimkuta mmoja peponi nitasangaa sana
 
Kuna yule mama nadhani ni mhaya kuna siku naelekea buguruni nimekaa upande wa kuelekea kulia kama naenda kigogo nailia timing taa iwake kijani ile imewaka tu nikaingia kushoto ninyooshe nilekee buguruni akaniwahi weka gari pembeni nikaipeleka principle ya kwanza sishushi kioo hadi uje ugonge kushusha kioo ananiuliza "kwanini nimehama mstari?" Nikamwambia nimebadili mawazo naenda buguruni, "ooh pale hauruhusiwi" nikamuuliza siruhusiwi kivipi? Wakati nilikua nyuma ya mstari wa dotted lines yaani sijaingia kwenye straight line( ule mstari ulionyooka) mama akaanza kuniambia wewe umevuka kwenye straight line nikamwambia sijakuvukia hapo na kama wewe uliniona kwanini usingenisimamisha hapo hapo wakati nina hama? Yani umeshaondoa ushahidi halafu unaniambiaje nithibitishe? "Ooh hii kesi itaenda mahakamani nikamwambia sawa ila maswala ya mahakamani yanapoteza muda gharama za kupoteza muda sina..mara karukia ooh utalipwa fidia nikamwambia hakuna fidia kwenye kesi ya traffic maana hadi kesi ya traffic iishe nifungue kesi ya madai ndo nilipwe fidia akaona daah kumbe sheria unaijua embu lete leseni nikampa makaratasi kuonesha leseni imezuiwa kuna kesi mahakamani lete gari hapa niikague nikamwambie fresh gari hio kagua mzee ingawa gari ina shida zake za kutosha ila alishaona huyu atanichosha tuu alanirudishia makaratasi yangu..hakusema kitu..mzee nikapiga gia mafuta...hahahaha maza hana hamu na mimi tena...
 
Dunia nzima hakuna watu dhulumati kama hawa jamaa. Siku ya mwiso nikimkuta mmoja peponi nitasangaa sana
Trafiki wa Tanzania huwezi wanafanya kazi vizuri ukilinganisha na wa nchi Jirani isipokuwa Rwanda peke yake.
Tatizo ni sharia kuwa nyingi sana zinazoadhibiwa kwa faini tu yenye kiwango sawa. Sheria inatushawishi tutoe Rushwa mana hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutoa elfu 30 badala ya kutoa 4000 akaondoka zake na kosa amelifanya yeye mwenyewe.
Mimi nalaumu Sheria zinazowapa mamlaka ya kuadhibu makosa wanayoyaona bila kuweka uzito wa kosa. Na kipimo cha kazi kuwa ni kuadhibu badala ya kuelimisha.
Siku zote sheria ni ngumu sana kutokana na wingi wake kwa binadamu; ndio maana Wakristo wanaamina kuwa Mungu aliondoa Sheria kupitia Kifo cha Yesu ili watu wahesabiwe haki kwa Neema.
Hakuna binadamu atakayefika Mbinguni kwa juhudi zake mwenyewe.
Hivyo tusiwahukumu wengine mana huenda tunayoyafanya gizani niabaya kuliko.

Tujiulize je ,mishahara wanayolipwa inaendana na kazi wanazofanya na wale wanaokutana nao muda wote ili wasidhulumu?
Je, kuna mifumo ya kuwafanya waishi kwa kusimamia haki na kutoa adhabu stahiki bila kushawishika na Rushwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kamanda kuwachunguza hawa matraffic mataa ya karume hasa wakina dada matraffic anakutoa kwenye foleni anakupeleka kibandani hujui kosa lako anakupeleka kwa wakubwa wao yeye anaondoka unabaki kujiuliza nimefanya nini hutoki hapo mpaka uache kitu.anae bisha aenda akasimame pale kwenye vibanda vya mabegi karume ajionee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na rushwa yao hawataki 5000

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo linalowakumba hao jamaa ni kazi yao kuwa hadharani sana.
Ingekua kazi zote zinafanyika hadharani basi nafikiri tungebaini ufisadi mkubwa sana kwenye maofisi ya watumishi wa umma .

Buku tano ni za brashi tu japo wengine wanakera sana kutokana na kauli zao. Ila Kiukweli watumishi wa Tanzania wana hali mgumu zinazopelekea kushawishika kuomba au kupokea rushwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom