Trafiki kuchukua funguo halafu afuatwe kwenye gari yake, Afande Mpinga ndio sheria inavyotaka ama?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,584
Hii nchi ya aibu sana! Traffic kakamata gari Kimara Bucha ziko zaidi ya kumi anakwenda kuchomoa funguo zao alafu wamfuate.

Ajabu ana mashine ya EFD kwanini asiwapige faini kama wamekosea? mnatengeneza mazingira ambayo hata asie na akili anawaza rushwa rushwa.

Njoo hapa Kimara Bucha Service Road wamepanga gari zaidi ya kumi alafu hamuwaandikii wala kuwapa risiti za EFD.

Ulipiga marufuku hili la dreva kutoka kwenye gari kumfuata traffic, leo mnatengeneza mazingira wenyewe.

Tubadilike sana ma traffic hasa wa Dar.
 
T202 DBL MOJA YA GARI ILIOKAMATWA DEREVA ANARUDI ANAONDOKA ZAKE ..N SHIDA MNASAFARINNDEFU TWENDEN RWANDA TUKASOME NYAKATI
 
HII NCHI YA AIBU SANA TRAFFIC KAKAMATA GARI KMR BUCHA ZIKO ZAIDI YA KUMI ANAKWENDA KUCHOMOA FUNGUO ZAO ALAFU WAMFWATE

AJABU ANA MASHINE YA EFD KWANINI ASIWAPIGE FAINI KAMA WAMEKOSEA MNATENGENEZA MAZINGIRA AMBAYO HATA ASIE NA AKILO ANAWAZA RUSHWA RUSHWA...

NJOO HAPA KMR BUCHA SERV ROAD WAMEPANGA GARI ZAIDIYAKUMI ALAFU AMUWAANDIKII WALA KUWAPA RESIT ZA EFD ..ULIPIGA MARUFUKU HILI DREVA KUTOKA KWENYE GARI KUMFWATA TRAFFIC LEO MNATENGENEZA MAZINGIRA WENYEWE

TUNADILIKE SANA MA TRAFFIC HASA WA DAR
Mi nadhani haya mazingira wanayotengeneza mtu ukiwa na haraka zako lazma rushwa ikutoke, au hata ukilipia faini inawezekana kabisa hiyo pesa isisfike kuliko. Nadhani wangetoa namba flani ambayo dereva ukiwa na mashaka na unavyohudumiwa na trafik unaweza kuwapigia kupata maelezo ya kina.
 
Wewe unalalamika funguo waliambiwa hadi tairi watoe shukuru wamechukua funguo maana kwenye tairi waliambiwa kuwa ukiwauliza wakujibu lilikuwa hivyo hivyo
 
Mpinga alisema dreva asishuke kwenye sasa wanachukua funguo ili uwafuate wakakutoe upepo jombaaa
 
Hivi hamjui hawa ndg zetu wanafanya kazi kubwa sna kuamka asubuhi na kusimama road masaa kibao kwa uyo mshahara usioweza nunua pampaz hata za wiki wasichukue chochote alafu wakistaafu mnawatukana ohh ulikuwa traffic hata kibanda huna wabongo bwana. Nashauri hao jamaa wapewe mda wao kuanzia saa 5 asubuhi waanze kukusanya za kwao
 
Sidhani kama hiyo number itasaidia,juzi juzi nimepandia basi toka tabora kuja dar basi linaendeshwa kasi napiga ile no ya Sumatra hawapokei,trafiki wanalisimamisha basi na kuliachia bila faini yaani ni shida tupu.
 
Mpwaaa rushwa kuisha n lazima tuwe NA rohongumu kama za rwanda
 
Hivi hamjui hawa ndg zetu wanafanya kazi kubwa sna kuamka asubuhi na kusimama road masaa kibao kwa uyo mshahara usioweza nunua pampaz hata za wiki wasichukue chochote alafu wakistaafu mnawatukana ohh ulikuwa traffic hata kibanda huna wabongo bwana. Nashauri hao jamaa wapewe mda wao kuanzia saa 5 asubuhi waanze kukusanya za kwao
kweli upumbavu ni mzigo,
 
Back
Top Bottom