Tetesi: Trafiki Kituo cha Makumbusho, Dar: RTO hajui mfanyalo, IGP anajua

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
13,975
20,250
Kituo kikubwa cha kubadilisha magari na abiria cha MAKUMBUSHO kilichopo Kijitonyama kwa sasa ni kama mtoto yatima.

Kituo hiki kilijengwa baada ya kile cha Mwenge kuvunjwa. Kituo hiki kina njia nyingi za kuingilia na kutoka na ni kizuri kwa miundombinu japo kimekuwa kero kuliko kona kwakuwa wafanyabiashara wameruhusiwa na Rais wafanye hata mlango wa chooni, Politics!

MA-TRAFIC wamekuwa wakikaa pale kituoni, yaani kwa gari zote zinazotokea barabara ya Tegeta /Mwenge/Sinza/ Tandale kuingia Makumbuho wanazisimamisha UKIWA NDANI YA GARI UTAONA KONDAKTA HARAKA ANACHUKUA TIKETI, ANACHUKUA KITU MFUKONI MWAKE ANAVIRINGISHA KWENYE TICKETI anamwachia yule polisi trafiki na baada ya muda yule kondakta anakuja kwenye gari: Hili jambo si kwamba gari linasimama kukaguliwa ama Dereva kukaguliwa leseni ama ubovu wa siti za gari, hapana, kondakta anashuka anampa ticketi na hicho kitu kilichofungwa na ni kwa gari zote.

Mchezo huo huo gari ikitoka Makumbusho wakakuta trafiki maeneo ya Hongera Baa, wanasimamishwa na kuwapa trafiki ticketi, wanaondoka, wakifika Sinza Kijiweni habari hiyo hiyo, wakifika pale Kariakoo Lumumba wanakuta wengine na pale Kariakoo Big Bon, the same story.

Swali kwa RTO, unafahamu hili ama tumjuze mheshimiwa raisi atuletee mtu atayetaka kujua na wewe upelekwe Katavi ukaishi na Gambosh?

IGP, unajua haya mambo yafanywayo na trafiki wako, na mkuu wa usalama barabarani amelala tu kukesha kwenye kurasa za Kigogo2014 kila uchao?

MHESHIMIWA MAGUFULI, unafahamu vizuri kwamba IGP ameshindwa kusimamia wateule wake? MAPOLISI vyeo vya chini wekeni CV zenu mezani, soon watu wanang'olewa.

NOTE: Pale Kinondoni Manyanya kua trafiki wawili wamekaa kuanzia jana, wanavizia magari yanayotoka Kinondoni Studio, yakipita tu kwenye taa wanayakamata, zile taa pale zimewekwa kimakosa na TEMESA na haieleweki gari ipi ina haki na ipi haina haki, isipokuwa zinazotoka Msasani na zinazokwenda Morroco, sasa polisi elimisheni TEMESA waweke taa vyema, na alama si kuvizia watu, mtakufa midomo wazi.

DALADALA: Baada ya agizo la level seat, sasa MAGARI WALITOA ZILE SEAT ZA KATIKATI, badala ya kurudishia za chuma kwa kuchomea, wameweka vigoda, hakuna pa kuegamia, ni mambao, abiria wanalazimishwa kukaa na ukikataa unatukanwa huna kondakta mmoja huku abiria 26 wakikuangalia bila kusema neno, huu ni upuuzi na kinyume cha sheria za usalama ambazo ziantaka kla garinliwe na mkanda, RTO nipo chini ya miguu yako japo nakupita umri na cheo, na hela pia, fanya ukaguzi wa kushtukiza.

LART/SUMATRA fanyeni kaguzi msiwaachie polisi, kule wao wameshafanya ni shamba la bibi na wanafahamiana na wamiliki wote wa magari, kuweni serious, ama mnasuburi mpaka TUMJUZE MPENDWA MAGUFULI?
 
Mifumo ya haki hapa nchini huwezi kuielewa imekaa hovyphovyo badala ya kutoa elimu wao wanataka rushwa.
hebu angalia traffic anakula mshahara kila mwisho wa mwezi anataka rushwa kwa konda ambae hawezi hata kununua kiatu kipya, kwa hali hii jamii itapata ustawi kweli?
 
Back
Top Bottom