Trafiki Dar wakusanya bilioni 1.9 mwezi February kwa makosa ya barabarani pekee

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,015
2,191
Kikosi cha usalama barabarani Kanda maalumu ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi BILIONI MOJA NUKTA TISA 1.9 kutokana na faini za ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia siku ya kwanza ya February 2016 mpaka tarehe 22 February 2016.

Taarifa yao imekuja siku moja baada ya Wizara ya fedha kutangaza jana kukusanya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya TRILIONI MOJA kwa mwezi February 2016 pekee ambao bado haujamalizika kikiwa ni kiwango tofauti na mwaka uliopita ambapo walikua wakikusanya kwenye BILIONI 800 n.k.
 
Nimekutana nao leo kinondoni kona ya mwananyamala.. ni shidaaaaaah wamekusanya magari kibao,,,,
 
Sifa kwa trafiki ingepaswa kuonesha jinsi makosa yalivyopungua kwa madereva kuelimika na ajali zilivyopungua. Hii ya wingi wa makosa na wingi wa pesa za adhabu je yastahili kuwa pongezi kwao?

Point.

Na kwa maombi yao ni kwamba watu waendelee tu kufanya makosa ili hela iendelee kuongezeka, tena wanawekewa target kabisa ya fine badala wangewekewa target ya kuhakikisha ajali zinapungua.

Magari mabovu yanakamatwa yanatozwa fine yanaachwa yaendelee kuwa barabarani ili kesho yakamatwe tena.
 
Kikosi cha usalama barabarani Kanda maalumu ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi BILIONI MOJA NUKTA TISA 1.9 kutokana na faini za ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia siku ya kwanza ya February 2016 mpaka tarehe 22 February 2016.

Taarifa yao imekuja siku moja baada ya Wizara ya fedha kutangaza jana kukusanya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya TRILIONI MOJA kwa mwezi February 2016 pekee ambao bado haujamalizika kikiwa ni kiwango tofauti na mwaka uliopita ambapo walikua wakikusanya kwenye Milioni 800 n.k.
Lazima vitambi ya rushwa viishe
 
Hapo ujumbe ni kuwa traffic Dar walikuwa wanagawana bilioni kwa mwezi kupitia vitabu feki na hela ya rushwa. Sasa kazi tu, endeleeni kutanua nyie watu wa Dar ili sisi huku Igwamanoni, Mwabaluhi, Isungang'olo hadi Tegeruka tuanze kupatiwa dawa mahospitalini
 
Juzii.nilikua safari..nimeona hata bidii ya kazi wameongeza....walikua wanahakikisha abiria tumefunga mikanda..na ukaguzi wa kistaharabu wa hapa na pale...
 
Kuna mtu mmoja nilimsikia analalamika kwa kuletewa bill ya milioni arobaini (40,000,000/-) kutoka taasisi ya umma na alivyohoji uhalali wa hiyo bili wakamwambia asipolipa wanamfungia biashara zake. Basi kwa shingo upande akalipa ili kuepuka kufungiwa huku akijaribu kufuatilia haki yake kwa sababu ya kuogopa kupoteza wateja wake!

Ninashangaa sana na sijui kama wengi wetu tumeshashtuka pale traffic police wanapokuwa na malengo ya kukusanya fine badala ya kulinda na kuwafundisha madereva (encouraging) kujua na kufuata sheria za barabarani. Juzi juzi jamaa yangu alilipishwa na trafic mmoja sh. 30,000/- bila kosa lolote na ndio nikaona hizi kampeini zingine ni kuiongezea nchi laana tu maana huyu rafiki yangu ndio pesa aliyokuwa kabakiwa nayo tu mfukoni!
Yaani kwenye miji kama Dar es Salaam magari mengi ni mabovu lakini matrafiki wanakamata yale ambayop wanadhani yatawasaidia 'kufikia malengo' yao na bila aibu wanatangaza kuwa wamekusanya billion 2 huku ajali zikiongezeka kila uchao!
 
Bado ni ndogo sana, hapo hawajafanya chochote. Zilizoishia mifukoni mwao ni nyingi kuliko hizo. !
 
Kumbe kwa nchi nzima wanaweza pata 10bil
Sasa inakuwaje wanaishi maisha mabaya mno kama sio wanadamu?
Hizo nyingi ni daladala ndio wamechangia
Hizo hela zote zinazokusanywa kwenye tozo za traffic zinaendaga Hazina kwenye mfuko Mkuu wa Serikali,ni sehemu ya mapato ya Serikali na si Polisi.Polisi hupata mgao wa bajeti km ilivyopangwa na serikali kupitia Bunge.
 
Back
Top Bottom