Trafiki anaswa na TAKUKURU akiomba rushwa ya ngono

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Askari wa kikosi cha usalama barabarani, Peter Albert Moshi anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kuomba rushwa ya ngono kwa mama wa mtoto aliyegongwa na pikipiki ili aweze kukamilisha taarifa za uchunguzi wa ajali hiyo.

Kamanda wa wa Takukuru mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi amesema leo Januari 7, askari huyo amekamatwa jana akiwa nyumba ya kulala wageni maeneo ya Soweto Mjini Moshi.

Amesema awali askari huyo alikuwa akichunguza ajali ya pikipiki ambayo ilimgonga mtoto huyo na kusababisha kuvunjika mkono ambapo mpaka sasa anaendelea na matibabu.

"Askari huyu alimwomba rushwa ya ngono mama wa mtoto aliyegongwa na pikipiki ili aweze kukamilisha taarifa ya uchunguzi wa ajali husika na kumpelekea mtuhumiwa ambaye ni dereva wa pikipiki mahakamani," alisema Kamanda Wikesi.

Ameongeza; “Katika uchunguzi wetu tumebaini huyu askari alikuwa akimsumbua mama wa mtoto kwa muda mrefu kuwa kama anataka haki ya mwanaye ipatikane basi hana budi kumpatia rushwa ya ngono na hivyo kusababisha shauri kuchelewa kupelekwa mahakamani.”

"Baada ya kuona usumbufu umezidi na mtuhumiwa hana nia ya kukamilisha kazi yake taarifa ililetwa Takukuru na mtego ukaandaliwa na ndipo mtuhumiwa alipokamatwa nyumba ya wageni akiwa hana nguo akitaka kutimiza azma yake," amesema.
 
Huyo kamanda mwenyewe wa TAKUKURU ni mwanamke huyu hawamuachi lazima wamnyoe.

Tabia chafu sana,hata kama alimtamani huyo mama ilikuwa heri amuonee huruma kwanza huyo aliyeumia kisha asubiri huruma ya huyo mwanamke kama angemuelewa,haki inapindishwa kipumbavu sana sometimes huyo mtoto amepata ulemavu wa kudumu.
 
Dhambi ni mbaya Sana! Kazi ya shetani ni kiharibu, kuchinja na kuharibu(yohana 10:10) unaenda jela yamkini hata kufukuzwa kazi kwa sababu ya dhambi ya uzinzi! Unaacha Familia taabani, jamani tuikimbie dhambi kwa kumpa Bwana Yesu maisha na kupata wokovu, haya mateso ya dhambi tutaepukana nayo!
 
Back
Top Bottom