Trafiki amnyanga'anya gari dereva, apinduka nalo mtoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trafiki amnyanga'anya gari dereva, apinduka nalo mtoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bnhai, Jul 17, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa PC Omary, amenusurika kufa baada ya kupinduka mtoni wakati akiendesha gari alilomnyang'anya dereva mmoja akimtuhumu kufanya makosa.

  Mbali na kupinduka mtoni, askari huyo mwenye namba F 1634 alimgonga na kumvunja miguu yote miwili mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Mpanda, Juma Kilombili(13) aliyekuwa akiogoa mtoni.

  Kabla ya tukio hilo, askari huyo alilikamata gari hilo Toyota Mark II namba T253 AHD linalotumika kama teksi baada ya kufanya makosa ya kawaida ya barabarani na kuamua kuliendesha mwenyewe ndipo alishindwa kulimudu na kutumbukia mto Misungumilo.

  Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Bi Matilda Walunde, baada ya gari hilo kutumbukia mtoni, lilimjeruhi vibaya kijana huyo ambaye alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu.

  Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili , dereva wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jinala Bw. Frank Nicholaus (23), alisema tukio hilo lilitokea Julai 12 saa 6 mchana wakati akimpeleka mteja wake eneo la Shule ya Wasichana Mpanda.

  Alisema alipofika maeneo ya mto Misungumilo, alikutana na trafiki huyo ambaye alimsimamisha na kumyang'anya kadi ya gari huku akimwamuru ampeleke mteja huyo halafu arudi eneo hilo.

  "Niliporudi, aliniamuru kushuka kwenye gari, mimi nilimtaarifu bosi wangu kwa simu kuwa gari limekamatwa. Askari huyo alininyang'anya funguo na kujaribu kuliendesha, kwa kuwa nililiegesha pembeni mwa barabara alipowasha tu, liliserereka kwa kasi na kutumbukia mto uliokuwa karibu na kumgonga mtoto aliyekuwa akioga baada ya kufua nguo zake hapo mtoni,"alisimulia dereva huyo.

  Kwa upande wake mmiliki wa gari hilo aliyejimbambulisha kwa jina la Bw. Charles Kaholilo mkazi wa kitongoji cha Msasani Mpanda, alisema amepata hasara kubwa kutokana na uzembe na 'ujuaji' wa trafiki huyo kwa kuwa gari hilo limekufa injini yake kutokana na ajali hiyo.

  Mmoja wa wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa madai kuwa si msemaji wa hospitali hiyo, alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba baada ya matibabu ya awali wamemsafirisha kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa matibabu zaidi kutokana na kuvunjika miguu yote miwili na kupata majeraha mengine makubwa mwilini.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Bw. Isunto Mantage amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuongeza kuwa Jeshi hilo linamhoji trafiki huyo na atapandishwa kizimbani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.


  Source: Majira
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hao ndio walinda usalama wetu.kila kona ya nchi yetu ni vilio tu.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sasa hawa wakipigwa kama wezikama kule sirali watu watalalamika kuwa wananchi wanachukua sheria mikononi.
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kweli dawa yao ni ile aliyopata kusemwa na PM Pinda katika tatizo la Albino ingawa watu kama MKJJ wanapinga kwa nguvu zote
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mwenyewe kumbw nae siyo dreva....
   
 6. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbona hawa maaskari hawataki kujifunza kutokana na kesi ya Zombe na wenzake?

  Mimi naona waziri mwenye dhamana na wizara ya mambo ya ndani na ile ya usarama wa raia wanatakiwa kuachia ngazi mara moja, maana maaskari wamezidi kutufanyia vituko vya ajabu sisi raia, na wao kazi yao ni kukanusha kila jambo na kuwatetea,
   
 7. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #7
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ,,,,,,,,daaaaaaah mzee nimechoka,halafu sehemu yenyewe sasa SIMBAWANGA!!!,sijui alitegemea nini huyu??,sasa hapa nani anabeba mzigo huu,serikali au trafiki mwenyewe??
   
 8. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na kinachouma zaidi utasikia huyo Traffic anaachiwa au kamanda polisi mkoa anamtetea, huu ni ujinga sana na inauma sana kwa kweli
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  ushauri wa bure! trafic police akikuomba kadi ya gari, leseni ya kuendeshea gari, au funguo za gari, usimpe!! mwonyeshe tu!

  Huwa wanatabia ya kung'ang'ania leseni au kadi hadi utakapotoa kitu kidogo au kulipa fine kwa kosa la kawaida kabisa!!!! wanajua huna ujanja kwani anakuwa ameshikilia leseni yako!! kama ni kadi peke yake tambaa mtu wangu, utagongesha muhuri TRA siku nyingine!! Watu wenyewe wa kulinda usalama wako wapi?
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja Mkuu, nidhamu ya askari polisi imepungua mno, watu wengi wanauawa kiholela na wauaji ni polisi. Tena hili tukio ni la kizembe kabisa.
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Sumba - wanga
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkiambiwa raia wema wamechoka watu mnasema ooh lazima zifuate taratibu haya sasa wazee wa taratibu mtueleze sasa taratibu gani kijana dereva huyo anatakiwa kuzifuata.
  Hapo Geshi la polisi lazima liingie hasara na kubeba hasara yote hiyo.
   
 13. K

  Kitoto Akisa Member

  #13
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya kupeana kazi kwa vimemo, ona sasa !jamani vigari vyenyewe tunanunua kwa hela ya ngama! kwenda kutiana hasara kijingajinga kiasi hiki, wakipigwa ooooh raia kauchuka sheria mikononi, sasa huyu askari ye sheria inamruhusu kkukamata na kuendesha gari ya mtu! kuna siku tutaja laumiana bure oooh. Mi nimepiga box ughaibuni, nimesota kinoma bongo, Mungu kasikia dua zangu nimenunua gari langu linifae mi na familia yangu, mjingamjinga mmoja analeta mambo yake! haya nyie hayeni tu siku hiyo na inakuja.sasa kati ya huyu trafic na dereva nani hajui?
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  HAKIKA SIJUI HAPO ITAKUWAJE. SIJUI KAMA INSURANCE ITALIPA HAPO KWANI HUYO ASKARI HAKUA LICENCED KUENDESHA GARI HILO.

  POLE SANA KIJANA ALIYEGONGWA NA KUVUNJIKA MIGUU. mOLA ATAKUPA AFUENI UPONE HARAKA
   
 15. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  vijana wa mjini wanasema imekula kwake.
  Pole nyingi kwa kijana majeruhi,hiyo ndo hali halisi ya nchi ye2 rushwa kila kona iya nchi.
  Mugu 2saidie waja wako!!!!!
   
 16. b

  bnhai JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Umeshaambiwa atafikishwa mahakamani, sasa tatizo liko wapi? Na waathirika wanatakiwa wafungue kesi za madai
   
 17. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  haya ndo mambo ya askari wetu. tatizo moja askari hawa wakikusimamisha tu wanakuwa wamesha kuhukumu. tabia chafu kuliko zote ni kama kunyan'ganya kadi, sticker ya bima, lesseni au hata gari kama huyo zuzu alivyofanya.mwaka 2007 ilishanipata mimi kwa wale wenzangu wa dar. ilikuwa ni may day 2007, askari wa upelelezi wakiwa kwenye patrol saa tano asbui, mimi nimetoka mwananchi communication pale tabata navuka reli kuingia barabarani nikitaka kuelekea buguruni, gari ya polisi, ikiwa imetahguliwa na daladala, zote zikiwa kwenye lane ya kushoto kabisa , nami naingia barabarani kwenye lane ya ndani, yaani kulia kwao, ghafla daladala ikasimama juu kwa juu ikila kicha, gari ya polisi ikalazimika kuhamia lane ya kulia - ambako mbele yake mimi nipo. nilichoelewani kuwa daladala hakumtendea pilisi sawa kwa kusimama kwa ghafla. so mimi nikaendelea kwenda kwa mwendo wa kawaida tu , nikavuka njia pand a tabata, naelekea buguruni, baada tu ya kufika matumbi, ile gari ya polisi ikaaanza kunipigia horn, na kuniwashia taa, ( mbaya zaidi ina namba za iraia), s nikadhani gari yangu inatatizo, nikaona nisimame, nilisimama baada ya kufuka daraja, hawa mapolisi wakaja wakasimama mbele yangu. wamvaa kiraia, gari ni ya kiraia, so huwezi jua nani ni nani. hapo jamaa akashuka akataka kufungua mlango wangu, mimi sikufungua, nkashusha kioo, akaomba leseni. nikamwuliza wewe ni nani?? wakati huo mwenzake yu- kimya. anayetaka leseni akasema kwa hasira , unafanya makosa halafu nualeta ubishi, akataka kubandua sticker ya bima. nikamwambia ndugu usipo jitambulisha nakuthibitishia hutawezakufanya chochote ktk gari hii. ndiyo akasema mimi inspecta wa polisi. wewe unataka kusambabisha ajali sku ya mei mosi, nitakufutia leseni upoteze kazi. nikasema mimi sikuzaliwa dereva kama unahiyo mamlaka ya kufuta leseni , futa. akasema nipe leseni twende kituoni yaani buguruni nikamwambia leseni sikupi mpaka nione kitambulisho chako, akasema leta funguo huku akisogez mkono kwenye switch. nikamzuia, mwenzake akasema affande si umpe kitambulisho!!. ndiyo akatoa, nikamwonyesha lesseni. akataka kuchukua , nikamwambia ukichukua leseni hiyo ukaondika nayo. ujue gari hii haiondoki hapa. so wewe nenda, akaona pagumu akanipa lesseni , akamwamuru mwenzake afuatane na mimi. yeye akiendesha ile gari yao, mimi na mwenzake kuelekea buguruni. tulipofika buguruni nikapelekwa kwa incharge- ni mama mtu mzima yupo kwenye late 50s,pale wakawa wanasema mimi ni dereva hatari. yupe mama alisema sentensi mbili tu,," kijana hujambo", nikasema sijambo shkamo mama, akaitika marahaba. mbaya wangu akazidi kubweka huyu kijana ni hatari sana. mama akajibu "kama ni hatari mpelekeni cental". mimi na askari aliyepanda gari yangu tukaanza kuelekea central, palepale nikamwonya huyu aliyekuwa kwenyegari yangu kuwa kazi yao isiwajengee maadui, mimi kuvunga sheria nahitaji kuwajibishwa na si kuaibishwa. nikamwambia mwonye mwenzio asiharbu kaisha yake kwa jambo asilojua. yule askari akasema nisimame, nikasimama , akaenda kuongea na mwenzake, baada ya muda mfupi akarudi akasema twende , tukaelekea central, lakini nikapita atm, nikachukua pesa. tulipofika nikaamuliwa nipark kwa watuhumiwa , nikapak. mbaya wangu akaja. nikapelekwa kaunta. pale nikaulizwa nikatoa maelezo. wakaenda kukagua gari yangu. baada ya kuona hata gari ilivyo smart wakaona aibu, hawakuwa na la kusema nikaambiwa niondoke. sasa hawa ndo askari wetu , hawatumii akili , wao ni nguvu tu!!!..wanawafanya watu hata waogope kupeleka watoto kuwa mapolisi
   
 18. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Thanks but no thanks na huo "ushauri wa bure" maana ni ushauri famba: Askari akikuomba leseni "usimpe," sasa ataisoma vipi kama hujampa? Askari lazima aichunguze leseni, huwezi kushika kileseni mkononi unamwambia soma, inaweza kuwa ni kikaratasi feki! Ukiombwa leseni lazima umpe!

  Hii stori nayo ni ya kilabuni, kama ya kutunga.

  Umetoa mlolongo wa hadithi ya magari ku cut infront of police car, halafu issue ikageuka kuwa gari smart! Askari wame spend mchana kutwa na wewe halafu wanakuja kukuachia baada ya kukuta gari "ilivyo smart," kwani walikusimamisha kwa sababu walidhani gari chafu?

  Askari wanakupeleka kituoni wakakubali usimame kutoa hela kwenye ATM, za nini? Usije kuwa umetoa rushwa halafu unataka kututungia hadithi hapa eti walikuachia kwa kuwa gari "ilivyo smart." Save me the literature...
   
Loading...