Trafiki akijitahidi kumtongoza mzungu kwa kiingereza huku akivunja sheria za barabarani

projectman

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
349
486
Askari wa usalama barabarani akijaribu kumtokea mzungu kwa kutumia kingereza cha madarasa,
hata hivyo askari huyo hakufanikiwa maana hao wazungu walikuwa wakimpima tuu akili zake na uwezo wake wa kufikiria huku ikiwa ni fedheha kwa taifa la Tanzania na watanzania kuonekana kuwa wote tunafanana na akili zake..

Askari wetu wa barabarani ni vyema kufanya kazi wakati wa kazi na sio kutafuta bahati kwa kuwaona weupe ndio wenye bahati.

Acheni mchezo na kazi
 
Attachments

  • Sabinus Paul[via torchbrowser.com].mp4
    3 MB · Views: 123
Tukio Zanzibar nimesikia bububu ikitwaja. Babu Ali wee ati nitaruhusu overspeeding mukipata matitizo namba yangu ya simu hii! Shame where is the professionalism ?
 
Sasa akiwekwa ndani hata kwa miezi 6 kwa kumkejeli rais unadhani wanafamilia watasahau kweli?
 
Tukio Zanzibar nimesikia bububu ikitwaja. Babu Ali wee ati nitaruhusu overspeeding mukipata matitizo namba yangu ya simu hii! Shame where is the professionalism ?

Bado tuna safari ndefu sana kwenye swala la professionalism aisee!!!, sasa kama huyo anafanya hivyo kwenye front end sijui itakuwaje kwenye back end
 
Askari wa usalama barabarani akijaribu kumtokea mzungu kwa kutumia kingereza cha madarasa,
hata hivyo askari huyo hakufanikiwa maana hao wazungu walikuwa wakimpima tuu akili zake na uwezo wake wa kufikiria huku ikiwa ni fedheha kwa taifa la Tanzania na watanzania kuonekana kuwa wote tunafanana na akili zake..

Askari wetu wa barabarani ni vyema kufanya kazi wakati wa kazi na sio kutafuta bahati kwa kuwaona weupe ndio wenye bahati.

Acheni mchezo na kazi
Duhh mpaka nimeona aibu mimi Ally ametisha "evere zingi in the road is not problem"
 
Daaah!! Aisee!! Hii ni aibu kubwa daah! Hao wazungu nafikiri ni wa Russia,nimesikia kama lugha ya Putin!! Kama kuna Sheria ya kumbana huyo Askari atafutwe tu,ameliaibisha jeshi la Polisi..
 
Angewapiga fine kwanza ndiyo achukue namba hapo ningemwona kweli anajiamini
Awapige fine tena!! Wakati lugha ya kutongozea kaitafuta sana.Lugha ya kuwaambia mmepigwa fine hope angeongea hata kilugha chake cha asili maana kuvunja yai(kuongea kiingereza) ni wito!!
 
Back
Top Bottom