Mbali na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali kuondoa rushwa na kuongeza mapato serikalini, lakini bado trafic wetu nao wanabuni mbinu mbali mbali kuhujumu mapato ya serikali na kujiongezea kipato isivyo halali.
Serikali imehakikisha inanunua kamera kuzibiti mwendo (Tochi) kwa ajili ya Trafic kuwadhibiti wanaokwenda mwendo kasi sehemu ambazo spidi ya magari inatakiwa iwe ndogo kulingana na sehemu husika, lakini cha kushangaza yanatokea haya ambayo nimeyashuhudia leo.
Nikiwa natokea Bukoba asubuhi maeneo ya mkoa wa Geita mbele ya Kasamwa nilisimamishwa na trafic akiyekuwa na kamera na kunitaka nilipe fine kwa kuzidisha mwendo, kamera yake (Tochi) ilionyesha ninilikuwa na speed ya 83 kwa saa badala ya 60 zinazotakiwa. Wakati nipo katika harakati za kulipa fine ilikuja basi namba 1 (jina kapuni) kutoka Mwanza ikielekea Bukoba ikiwa kasi, lakini cha kushangaza yule Trafic mwenye kamera hakuimulika hiyo basi kutaka kuhakikisha mwendo wa basi hilo, Basi lilipomkaribia alilisimamisha na kwenda kwa dereva dirishani na kupena mkono na huyo dereva na kisha kupeana kitu ambacho trafic alikiweka mfukoni na kuagana na huyo dereva kwa tabasamu kali huku trafik akimwambia usinitibulie huko mbele (akimaanisha asiwape ishara wanaokuja kuwa wapo hapo). Baadae tena muda mfupi kidogo likaja basi lingine namba 2 (jina kapuni) nalo lilikuwa kasi, hakulimulika pia, Akalisimamisha akatoka nadhani ni konda yule wakasima mbele ya basi ambapo si rahisi abilia kuwaona na trafik kupewa pesa, nilishuhudia akirudisha na chenji, Duh! Nilishangaa sana nikamuuliza yule trafik aliyekuwa akiniandikia fine mbona hayo mabasi hayakumulikwa tochi? Akajibu spidi yake yote mawili ilikuwa ndogo inaonekana kwa macho, kitu ambacho sio kweli, akanionyesha unaona kuna basi limepita super sumi wamelipa, nikamjibu inaelekea nyinyi mnamabasi yenu ambayo mnapeana chochote na hivyo hamyamuliki kujua spidi yake, hakujibu.
Kamanda Mpinga kazi kwako, majipu hayo.