Trafigura yafidia waathirika Ivory Coast=Je hii inawezekana North Mara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trafigura yafidia waathirika Ivory Coast=Je hii inawezekana North Mara?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Sep 21, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Trafigura yafidia waathirika Ivory Coast

  Imeandikwa na Peter Musembi

  [​IMG]
  [​IMG][​IMG]
  Taka zilimwagwa katika maeneo 15 ya mjii mkuu AbidjanKampuni moja ya mafuta nchini Ivory Coast imekubali kulipa fidia ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 46 kwa watu wanaosema waliathiriwa na sumu iliyotokana na taka za kampuni hiyo mwaka 2006.
  Kampuni hiyo ya Trafigura yenye ofisi zake mjini London, Amsterdam na Geneva, imesema watu 30,000 kila mmoja atapokewa kiasi cha dola za kimarekani 1,546.
  Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza ya takribani dola za kimarekani milioni 200 ambazo kampuni hiyo iliilipa serikali ya Ivory Coast mwaka 2007 kuwafidia waathirika.
  Serikali ilitoa fedha hizo kwa ndugu wa familia wa watu 16 ambao vifo vyao inaaminika vilisababishwa na sumu ya taka hizo.
  Trafigura na wanasheria wa waathirika wamekubaliana kuwa uhusiano kati ya taka zilizomwagwa na vifo vilivyotokea haujathibitishwa.
  Taarifa ya pamoja ya kampuni hiyo na wanasheria wa Uingereza wanaowawakilisha raia wa Ivory Coast, Leigh Day and Company, wamesema katika hali mbaya ya kutisha uchafu huo ulisababisha dalili zinazofanana na ugonjwa wa mafua.
  Msemaji wa walioathirika ameshutumu makubaliano hayo akisema fidia hiyo haitoshi na kwamba walitarajia kiasi cha juu zaidi kulipwa.
  ''Gharama za matibabu zilizotumika kwa zaidi ya miaka mitatu inazidi kiasi hicho cha fidia,'' Mkuu wa Chama cha Watu walioadhirika na Taka zenye Sumu, Quattara Aboubabacar ameiambia BBC.
  Anaamini athari huenda zinazendelea kutokea hadi leo.
  Trafigura imesema imeridhishwa na makubaliano hayo ya fidia lakini kampuni hiyo inakabiliwa kupelekwa mahakamani kuhusu kesi hiyo.
  Taka hizo zenye kemikali zilisazalishwa na Trafigura na kusafirishwa hadi mwambao mwa Ivory Coast kwa meli ijulikanayo kama Probo Koala.
  Katika mwezi wa Agosti 2006 takataka kutoka katika meli ya Trafigura zilimwagwa katika maeneo 15 ya Abidjan mjii mkuu wa Ivory Coast.
  Kampuni moja ya eneo hilo ilikodishwa kushughulikia takataka hizo, lakini iliishia kutawanya takataka katika maeneo mabalimbali ya mjii mkuu huo.
  Kemikali za taka hizo zilileta harufu mbaya ya kutisha katika maeneo hayo.
  Katika wiki zilizofuatia umwagwaji taka hizo, maelfu ya watu waliripoti dalili zilizofanana kuathirika kiafya ikiwemo matatizo ya kushindwa kupumua, kuumwa na kuharisha.
  RIPOTI YA UMOJA WA MATAIFA
  Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kwa uchache vifo 15 vilisababishwa na sumu ya taka hizo.
  Ripoti hiyo imesema kuna ushahidi wa awali wa kutosha kuwa vifo vilivyoripotiwa na matatizo ya kiafya vinahusiana na taka hizo kutoka katika meli ya mizigo.
  Kampuni hiyo ya Trafigura imeshutumu ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa ni ya mapema sana na si sahihi.
  Trafigura daima imekuwa ikisisitiza kuwa haihusiki na umwagaji taka huo na kwamba ulifanywa na kampuni iliyoikodisha kushughulikia taka.
  Na pia inakanusha kuwa taka hizo zenye sumu zingeweza kusababisha magonjwa hatari yanayodaiwa na wakazi wa maeneo hayo, ikiwemo kuchubuka ngozi, kutokwa damu na matatizo ya kushindwa kupumua.


  Source: www.bbc.co.uk/swahili
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo North mara ni mgodi wa wacanada na ndo wale wale wanatawala UN. Lakini NGOs zikiamua kuishitaki Barrick, wananweza kulipa fidia.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana,
  Tatizo la North Mara ni serikali yetu. Imekuwa bubu hata imeshindwa kulalamika. Barrick imewahi kushtakiwa kwingineko inakofanya shughuli za
  uchimbaji na kudaiwa fidia. Sisi serikali imewakumbatia kiasi kwamba anayetishiwa ni mkuu wa Mkoa tu.
   
Loading...