Trafic watatu wagongwa na gari dogo Arusha

mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,521
870
Muda mfupi uliopita kwenye saa 7:30 mchana askari wa usalama Barabarani( traffic) watatu pamoja dereva wa daladala wamegongwa vibaya na gari katika eneo la kanisani opposite na jengo jipya la NSSF.......ambapo inahofiwa traffic mmoja amefariki hapahapo( damu zilikuwa zinamwagika masikioni na puani) na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya pamoja huyo dereva.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajli hiyo .....traffic hao walisimamisha daladala iliyokuwa inatoka mjini kuelekea kijenge na kuanza kumhoji ambapo ilibidi ashuke chini baada ya kupaki gari pembezoni mwa barabara....ghafla gari hilo dogo lillokuwa linatoka mjini (clock tower)lilikuja kwa kasi mahali waliposimama na kuwagonga wote wanne...Dereva aliyesababisha ajali ameshakamatwa palepale eneo la tukio.
 
Nimeipata hii taarifa nikiwa natokea CRDB Bank hapa juu ya posta! Duh so sad:shock:
 
Nimepigiwa simu kutaarifiwa juu ya kadhia hii ya kutisha.
Nahisi gari hiyo ndogo iliyosababisha ajali ilikuwa na wahalifu!
Ni confirmed kwamba huyo askari trafiki amefariki kabla ya kufika hospitali.
 
Nimepigiwa simu kutaarifiwa juu ya kadhia hii ya kutisha.
Nahisi gari hiyo ndogo iliyosababisha ajali ilikuwa na wahalifu!
Ni confirmed kwamba huyo askari trafiki amefariki kabla ya kufika hospitali.

Nimeongea na jamaa mmoja anasema huyo aliyekuwa anaendesha gari dogo alikuwa anaovertake bila mpango ndio ajali ikatokea...
 
Inawezekana ikawa ni makusudi ya huyo dereva wa gari ndogo kuwagonga traffic hao, tafadhali apimwe kwanza akili

Mungu amweke pema marehemu na majeruhi wapone haraka. Polisi watatu walikuwa wanafanya au wanazungumza nini na dereva wa daladala?
 
Mara nyingi nimekuwa nawashauri wanausalama barabarani, mara nyingine hata kuwakemea tabia ya kufanya check point mahala popote bila kujihakikishia usalama wa kupaki magari wanayoyasimamisha, usalama wao wenyewe, usalama wa wananchi waenda kwa miguu na waendesha magari wengine. Ninadhani eneo linalosemwa sio eneo salama kufanywa check point. Ona sasa balalaa hili. Poleni sana kwa ajali hii.
 
si tu kuwa salama bali hata mahali walikogongwa ni vigumu au si busara kusimama pale. Yani hata kupishana gari mbili inakuwa tabu inakuwaje waegeshe gari pale?ujue pale upande mmoja kuna ka garden na upande wa pili ni barabara ,nadhani wanausalama waweke cheki point mahala flan wala si kuviziana...watu wanasema ni makusudi lia siwalaumu labda hawajawai kuendesha chombo cha moto...hawafikirii kuna kufeli breki wakati trafki ameshaingia barabarani akuzuie, hawafikirii kuna kujarm gear pads na breakpads,wanadhani gari inaendeshwa kimalaika malaika!si ivo...nimepita pale nikaona ile noah ilivoharibika vibaya, shoo na kioo cha mbele ni chenga ...anyway poleni kwa wote...
 
Nimeongea na jamaa mmoja anasema huyo aliyekuwa anaendesha gari dogo alikuwa anaovertake bila mpango ndio ajali ikatokea...

anaovertake vipi wakati upande wa kushoto ndo upande ajali na ndo line ya magari yanayotokea mjini?labda uniambie alikuwa spidi kali sana ghafla akaona askari mbele yake...pale kwenye maua huwezi kiuovertake kushoto wakati ndo njia yako na hakuna service road,howwwwwwwwwww??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom