Trafic wa Bamaga mnatukwaza Asubuhi

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Habari zenu ndugu zangu.

Hawa polisi trafic wanaosimama pale Bamaga hasa nyakati za asubuhi wanatukwaza kweli kweli hasa sisi tunaotumia barabara ya Bagamoyo na Mandela.

Kuna ukarabati wa barabara unaendelea kwenye hii barabara, hii inapelekea muda mwingi kuisha kuisha kwenye foleni. Mfano unatumia 30- 40 mins kutoka Lugalo mpaka Mwenge mataa.


Sasa cha kushangaza hawa trafic wanasimamisha lila daladala na kuanza kujichekesha na kuomba rushwa. Mmeruhusiwa kuomba rushwa lakini mjue kwa kufanya kwenu hivyo mnatuchelewesha sisi abiria kwenye shughuli zetu.

Natoka wito kwa mapolisi hawa hasa yule dada mwembamba aliyekomaa sura waache kusimamisha kila gari, daladala bila sababu za msingi tena asubuhi.

Kwakuwa magari ya abiria yanapita mchana kutwa hapo. Nawashauri muombe hizo rushwa baada ya masaa ya watu kwenda kwenye shughuli zao kuliko mfanyavyo sasa hivi wakati wa busy hours.

Najua wakubwa zenu wapo humu watasoma na kufanya kazi sio wafanyie kazi taarifa za maandamano tu

Nataka kamanda wa trafic kinondoni/ mabatini ajue kwamba kwanza pale mnasimama wengi sana sana. Pia mnaomba rushwa hadharani na kufanya hivyo mnasimamisha kila daladala bila kujali kwamba watu wanawahi.

Mtu usimame kwenye foleni kisha foleni ukiimaliza usimamishwe na mla rushes/trafic halafu anaanza kujichekesha kisa apewe 2000/=?
Tabia mbaya sana hii
 
Kama wale wa mataa ya VETA ni mafisadi wakubwa wasipo angalia mbinguni hawaendi, pale pamekaa hovyo hovyo badala yakuelekeza watu sasa kazi yao ni kuomba rushwa tu macho mekunduuu kukodolea elf 10 10 za watu
 
....Eti buku mbili,kuna siku nilikuwa na jamaa akampa hela elfu 2000,akamwambia elfu tano hiyo,nikamuuliza sasa akigundua ni elfu 2000?,akanambia hawezi kuangalia pale watu watamwona:D:D:D
hiyo ni sawa na kunya halafu unasogeza uvunguni.

konda hawezi fanya ujinga aina hiyo,maana anajua mambo yataharibika mita kadhaa mbele tu hapo.
 
Kama wale wa mataa ya VETA ni mafisadi wakubwa wasipo angalia mbinguni hawaendi, pale pamekaa hovyo hovyo badala yakuelekeza watu sasa kazi yao ni kuomba rushwa tu macho mekunduuu kukodolea elf 10 10 za watu
tuko kwenye right track nasema uongo ndugu zanguuuu
 
Back
Top Bottom