Traffic Police wa Tanga Hawasomi Road Traffic Act 1973?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Traffic Police wa Tanga Hawasomi Road Traffic Act 1973?.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by gayella, Aug 15, 2011.

 1. g

  gayella Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana FJ naomba mnisaidie hasa upande wa sheria, mimi nina gari siku moja asubuhi na mapema nilimwomba mdogo wangu aendeshe gari kunipereka stand ya basi nilikuwa nasafiri, aliingia barabara ya 12 ambayo ni 1way nyembamba sana wala haina packing space ila madereva huwa wanapose kidogo wakishusha abiria wao. Ndivyo hivyo bwana mdogo alifanya hivyo nilipomwomba apose kidogo ili niulize mpigadebe aliyekuwa dirishani kwangu ni wapi Raha leo basi zinapack?. Baada ya kutoka hapo kwa mbele yake huwa kuna kibanda cha hawa ndugu, basi alitupiga mkono dogo akasimama. Traffic akamuuliza, "naomba leseni yako akampa pili naomba kadi ya gari akampa, alikaa kidogo anafikiri mara, kwa nini ulisimama barabarani kijana akamweleza kwa vile ni 1way na offisi ipo hapo nilikuwa nauliza tu kituo ni wapi isitoshe nyuma yangu kulikuwa hakuna gari. Traffic akasema, pack hapo na ulipe faini 20000, mimi nikamwoba msamaha maana wakati huo dk 2 zimebaki basi iondoke na huwa inaondoka kwa muda. akasema lazima ulipe, basi mimi nikamwambia si hoja naomba nikashushe mizigo yangu maana muda umeisha ili dogo aje kituoni alipe isitoshe kadi na leseni unazo. polisi alikataa kabisa anataka gari iende kituoni, basi katika kubishana huko niliamua kushusha mizigo kufuata basi. basi tayari imekwisha ondoka basi nilbaki na tiketi na dogo kaenda kulipa 20000.Je, swali linakuja
  1. Ni razima faini za traffic zikalipiwe kituoni wakati huohuo?
  2. Naweza kudai hasara ya nauri aliyoniingiza hasara

  polisi huyu yupo mabawa na namba yake mkihitaji nitaitoa. Hilo ndilo lilinikuta wana JF
   
Loading...