Traffic Police na SUMATRA Dodoma hili linawahusu

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,677
32,983
Jana majira ya saa 5 asubuhi tulipanda daladala moja inayokwenda UDOM, ilitoka na abiria kadhaa waliosimama, kufika eneo la posta na kuendelea likajaza abiria kupita kiasi, na yapata kilomita moja toka hapo kuna askari wa usalama barabarani waliokagua basi lile na kuliruhusu kuendelea na safari, baada ya kufika kwenye ule mlima karibu na ukumbi wa Chimwaga, gari likazidiwa na kuzima, dereva akawa analalizisha kuliwasha huku likitaka kuporomoka kurudi nyuma, baada ya abiria kupiga kelele za kumlazimisha kondakta afungue mlango naye akiwa hataki ndipo wakatoa vitisho akafungua na abiria kushuka huku wengine wakibaki ndani na dereva akijaribu kuliondoa kwa lazima lakini likawa linarudi nyuma huku kondakta akiweka mawe na mengine yakikatika.

Binafsi niliona ile ni hatari kwasababu eneo lile lina kona kali na mteremko mkali pia, ipo haja kwa vyombo hivyo viwili kushirikiana kukagua usalama wa daladala za UDOM, hasa msongamano/ujazaji wa abiria na pia kama magari yale yapo salama.

Hata hivyo nilishangaa baada ya muda dereva aligeuza gari kwa namna anayojua yeye na kuondoka kurudi mjini huku abiria wakitelekezwa eneo la tukio.
20180927_112023.jpg
20180927_111547.jpg
20180927_111514.jpg
20180927_111525.jpg
20180927_111509.jpg
 
Jana majira ya saa 5 asubuhi tulipanda daladala moja inayokwenda UDOM, ilitoka na abiria kadhaa waliosimama, kufika eneo la posta na kuendeleablikajaza abiria kupita kiasi, na yapata kilomita moja toka hapo kuna askari wa usalama barabarani waliokagua basili lile, baada ya kufika kwenye ule mlima karibu na ukumbi wa Chimwaga, gari likazidiwa na kuzima, dereva akawa analalizisha kuliwasha huku likitaka kuporomoka lirudi nyuma, baada ya abiria kupiga kelele za kumlazimisha kondakta afungue mlango naye akiwa hataki ndipo wakatoa vitisho akafungua na abiria kushuka huku wenginge wakibaki ndani na dereva akijaribu kuliondoa ka lazima lakini likawa linarudi nyuma huku kondakta akiweka mawe na mengine yakikatika.

Binafsi niliona ile ni hatari kwasababu eneo lile lina kona kali na mteremko mkali pia, ipo haja kwa vyombo hivyo viwili kushirikiana kukagua usalama wa daladala za UDOM, hasa msongamano/ujazaji wa abiria na pia kama magari yale yapo salama.

Nilishangaa baada ya muda dereva alogeuza gari kwa namna anayojua yeye na kuondoka kurudi mjini huku abiria wakitelekezwa eneo la tukio.
Labda Gari ilikuwa na tatizo mkuu lakini siyo kwa sababu ya kusimamisha watu,

Watu wenyewe siku hizi wa kg 50 ata mjae pomoni kwenye Vitz inatembea sembuse "I.C" mkuu.
 
Tatizo abiria wanaona gar limejaa bado wanalazimisha kupanda eti wasomi wapo UDOM bora hata bangi ninayovuta Demiss hapaa
 
Tatizo abiria wanaona gar limejaa bado wanalazimisha kupanda eti wasomi wapo UDOM bora hata bangi ninayovuta Demiss hapaa

Ukijengeka utamaduni wa kuwateremsha waliozidi inaweza kuwa tiba mojawapo
 
Back
Top Bottom