Traffic Police na mashine za kupiga faini

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,143
1,291
Mashine za kutoza ushuru zimekuwa ni sehemu ya uniform kwa traffic police sasa hivi.

Naweza kusema kila Traffic polisi watatu unaowaona barabarani wawili wana hizi mashine za kulipia faini kwa makosa ya barabarani.

Fedha zinazokusanywa ni nyingi sana lakini fedha hizi hazitumiki katika kutoa elimu na mafunzo juu ya usalama barabani.

Kuna watumiaji wengi sana wa barabara ambao wanahitaji elimu kuhusiana na usalama wa barabarani kama vile wanafunzi, waendesha bodaboda, waendesha mabasi na malori makubwa.

Serikali ingewapa kipaumbele katika usalama wa barabarani kutokani na fedha zinazokusanywa.

Fedha zinazokusanywa kwa ajili hii zinapelekwa kwenye shughuli nyingine matokeo ni kwamba ajali za barabarani zinaongezeka na vifo ni vingi
Hii miradi mikubwa tunayoambiwa tunajenga kwa pesa zetu, kiasi kingine ni sehemu ya faini za makosa ya barabarani.

Traffic police wako mstari wa mbele kukusanya mapato kuliko kutoa elimu.
 
Back
Top Bottom