Rogie
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 7,584
- 6,694
Habari JF
Nimekutana na issue sijaielewa leo and I would like to share with you perhaps I am a bit out of the know.
Nimetoka Kinondoni hadi Magomeni Morocco nikataka kuingia kulia nipitie barabara ya Tandale Uzuri Traffic Police akanigomea na kunilazimisha niende hadi Magomeni Hospitali. Kufika Magomeni Hospital baada ya kusubiri kwenye foleni nikataka nikunje kuelekea Morogoro Road Traffic Police akanikatalia tena akinitaka ninyooshe nielekee Magomeni Mikumi.
Wakuu hili ni sahihi? Au busy hours huruhusiwi kukunja?
UPDATES 18.02.2016
KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA KATIKA MAKUTANO YA NJIA KTK MOROGORO ROAD HASA MAGOMENI
Naomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara ktk makutano ya barabara ya morogoro/kawawa eneo la magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo.
Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia (No right turn). Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:
1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia na kurudi hadi magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea kinondoni (Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights). Ama unapofika magomeni mapipa ukitokea jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la moroko hotel karibu na kanisa la RC utapinda kulia kuelekea kinondoni (kuna alama ya mchoro brbrn eneo hilo la mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo).
2. Ukitokea kinondoni kuelekea ubungo(kuna kibao cha maelekezo kupande wa kushoto karibu na kanisa la KKKT kabla ya kufika traffic lights) dereva atakapofika mataa atapaswa apinde kushoto kama anaelekea jangwani na atakapofika Bondeni hotel (kuna alama chini brbrn na kibao cha maelekezo) atapinda kulia kuingia brbr ya kawaida kurudi mataa ndipo aendelee na safari yake ya kuelekea upande wa ubungo.
3. Ukitoka Kigogo round about kuelekea jangwani (kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na petrol station kabla ya kufika mataa) dereva atapaswa apinde kushoto kama anaelekea ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia kurudi traffic lights na kuendelea na safari yake kuelekea jangwani/mjini.
4. Pia eneo la njia panda mabibo /morogoro rd na junction ya mikumi kwa shekhe yahaya hairuhusiwi kupinda kulia kwa wale wanaotokea ubungo. Vibao vipo vinaelekeza namna ya kupita kwenda mabibo au mikumi.
NB.
Mabadiliko hayo yanatokana na uwepo wa barabara za BRT. Madeva waliowengi wanaendesha kwa mazoea na cyo kufuata sheria za barabarani kwa maana alama na michoro iliyopo barabarani. Naamini kila dereva akizingatia na kuheshim utaratibu na alama zilizopo, hakutakuwa na tatizo lolote wala hakuna dereva atakayekamatwa. Baadhi wanaposimamishwa na askari ili waelimishwe matokeo yake wanakuwa wakali. Haki na wajibu lazima viende pamoja.
Naomba kuwasilisha.
WASAMBAZIE WENGINE UJUMBE HUU.
RSA TANZANIA.
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE