Traffic na rushwa:tufanye kitu gani kukomesha ama tuache Hali Kama ilivyo

Hivi 2000,5000 ni rushwa kweli??? Unajua wakubwa wa wakubwa wa wakubwa wao wanakulaga kiasi gani??? Ndo maana ukaambiwa ya kubrush viatu maana sidhani hata kama inamnunulia mlo ashibe.
Naumiaga mno nikiwaona wanapigika juani na hapo ukute boss anahesabu yake kila siku
Kama hatupendi rushwa tuanze kupigia kelele hawa wajuu maana wanakula kuliko hizi 2000 zinazotupigisha kelele.
Kuna wakati sisubiri hata nipigwe mkono, kama niko kweye foleni yupo karibu namtoa hata ya maji. 2000 au 5000 haifilisi pochi
Uko sahihi mkuu.
Kuna mizee inakula nchi kupitia makaratasi huko maofisini, tena rushwa zao ni millions
Trafiki kwa mshahara gani tunaomlipa mpaka asile rushwa hizi laki mbili au hela gani? Watu wanalipwa 11m kwa mwezi kazi yao kupiga makofi kwenye meza.
Trafiki hajaumbiwa kuteseka, kuna mijitu inakwepa kodi baada ya siku mbili iko kwenye orodha ya matajiri Tanzania.
 
Sitetei rushwa kwakuwa najua madhara yake hasa kwenye utoaji haki.
Lakini tutazame motive ya suala la rushwa kwa trafiki.

Tuanze kwa kujiuliza ugumu wa mazingira ya kazi hususan jiji la Dsm, joto kali, vumbi na jua kali.

Sasa tutazame mshahara wa huyo trafiki ambao wengi ni rank to file Constable Basic salary yake haivuki 500K. Take home yake ina range kwenye 400K.

Tutazame kwa mlengo huo huo mtu ni Sajini wa Polisi, Salary yake Basic haizidi 800K take home haitozidi 700K.
Mtu huyo ana familia, watoto wanasoma, wakati mwingine amepanga, kijijini kwao kuna msururu wa ndugu anawasapoti.

Mtu huyu akipata 30 to 50K per day ni fedha nyingi sana ambazo zinazidi salary yake mara mbili au tatu.

Sisi sote tunahitaji maisha mazuri, kuna watu hudhani wao ndo wanahitaji maisha mazuri, wanalipana maposho ya mavazi, furniture, usafiri, mawasiliano n.k

Kwahiyo trafiki ndo yuko Tanzania kuwa msindikizaji? Serikali iboreshe maslahi ya watu wake ili tupate uhalali wa kuwalaumu. Kuna watu kwenye taasisi za umma huko mtu wa kawaida kabisa salary yake 3m. Ana access ya kukopa 100m+
Hii nchi sio ya watu baadhi ni yetu sote
Unafahamu kwamba Polisi wote Tanzania wanalipwa posho ya shilling laki tatu kila mmoja bila kujali vyeo?

Je unafahamu hao madereva wa canter za wahindi mishahara yao ni laki mbili kwa mwezi?

Nani mwenye maisha magumu hapa kati ya dereva wa muhindi na traffic?
 
Unafahamu kwamba Polisi wote Tanzania wanalipwa posho ya shilling laki tatu kila mmoja bila kujali vyeo?

Je unafahamu hao madereva wa canter za wahindi mishahara yao ni laki mbili kwa mwezi?

Nani mwenye maisha magumu hapa kati ya dereva wa muhindi na traffic?
Huna cha kunisimulia kuhusu maslahi ya polisi labda uniulize mimi nikwambie.
Kazi ile na risk wanayopata posho ya laki 3 ni upuuzi tu sio hela hiyo.
 
Huna cha kunisimulia kuhusu maslahi ya polisi labda uniulize mimi nikwambie.
Kazi ile na risk wanayopata posho ya laki 3 ni upuuzi tu sio hela hiyo.
Kazi ipi ya risk wanayofanya Polisi, kwa akili yako ya kuvukia barabara unadhani polisi wote wapo kwenye kikosi cha Anti robbery?

Unajitia upofu hujui kwamba kuna Polisi hawavai hata hayo magwanda na kazi zao ni ofisini tu?
 
Back
Top Bottom