ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,555
- 44,729
Sikuelewa Kwanini rais wa awamu ya Tano(RIP) alitamka hadharani kwamba wapewe hela ya ku brush viatu.hayo yamepita je sisi Kama jamiiforum member tumeonyesha mchango gani katika kudhibiti Hili suala maana Sasa imekuwa waziwazi kabisa hiki kitengo Cha barabarani hawana aibu wanapewa hela na madereva kuanzia 1000,2000,5000 na kuendelea.sijui madereva na nyie huwa mnatoa hio hela kwa sababu gani unakuta anasimamisha gari halafu hawaongei chochote Bali lugha Ni kaposho kidogo..Sasa nahoji Kama Serikali yetu imeshindwa kutolea hili Jambo tamko na imeishia kupiga piga tu mikwara juu juu sisi tunaamuaje je kuna haja tuanzishe kampeni maalumu yenye lengo la kupaza sauti Zaidi pengine rais wetu wa Sasa mama Samia ataliongelea au tuache tu maisha yaendelee Hawa maofisa wa Serikali waendelee kupoozwa na madereva maana isije kuwa abiria wenyewe na madereva wanaona sawa halafu sisi tukajifanya kimbelembele mwisho wa siku wabongo wakaishia kutuchora tu.