Traffic na dereva

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Jamaa kakamatwa barabarani na trafic kazidisha speed

DEREVA:Kunatatizo lolote mkuu?

POLICE:Umezidisha speed mheshimiwa
DEREVA:Ehh! kumbe
POLICE:Naomba leseni yako
DEREVA:Ningekuwanayo ningekupa,sina mkuu
POLICE:Eti huna leseni?
DEREVA:Niliipoteza kwa kuendesha huku nakunywa
POLICE:Nipe kadi ya gari
DEREVA:Nayo sina mkuu
POLICE:Kwanini?
DEREVA:Hii gari nimeiba na mwenye gari nimemwua,yupo kwenye buti kama unataka kumwona

Polisi kajivuta nyuma hatua chache kapiga simu kituoni,ndani ya dakika 5 gari za polisi zimelizunguka lile gari.

POLICE 2:Dereva toka nje ya gari.Yule jamaa akatoka
DEREVA:Kuna tatizo lolote afande?
POLICE 2:Askari wangu kanipigia simu unagari la wizi,na umemwua mwenyegari umemweka kwenye buti hebu fungua buti
Dereva kafungua buti na hapakuwa na kitu.
POLICE2:Hili gari ni lako?
DEREVA:Ndio afande kadi yake hii hapa
Polisi2:Kashikwa na mshangao baada ya kuona kadi ya gari
POLICE 2:Leseni yako iko wapi?
Dereva kaingiza mkono mfukoni katoa leseni
DEREVA:Hii hapa afande
Polisi 2 kashikwa na mshangao tena,
POLICE2:Haya asante bwana mkubwa, askari wangu aliponipigia kaniambia,una gari la wizi,umemwua mwenye gari na huna leseni

DEREVA:Halafu nahisi tu huyo mshenzi atakua amekudanganya kwamba nilikuwa naendesha kwa speed kubwa




 
Hii Ulaya tu, hawa wa kwetu wangekwisha malizani sku nyiiingi!
 
dk 5 kwa hii tanzania? wp hapo mkuu
Usishangae kwa Tanzania. Trafiki wetu wanapokamata gari wako shapu sana kwani wanajua kuna mlo pale.
Lakini wanapopigiwa simu kuambiwa kumetokea ajali na watu wamekufa, hapo sahau.
 
Back
Top Bottom