Traffic mataa ya chang'ombe wafanya kitendo cha kinyama kwa wananchi

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
2,000
Jioni hii mataa ya veta hapa sheli ya oil com traffic wamempiga notification dereva aliyekuwa na abiria kwenye gari ndogo private yenye namba za usajili T135 AMU toyota korola kwa kosa la kuzidisha abiria wakati gari hiyo ilikuwa na watu wazima watatu na watoto wadogo wawili.

Dereva huyo hakuwa na pesa cash ikabidi aanze kupiga simu kwa ndugu zake wamtumie pesa, traffic wakakasirika eti anawapotezea muda...unyama ulioje wakatoa upepo matairi yote ya mbele gari ili dereva asitoroke,,je huu ni uungwana?? Hii ndio sheria ya usalama barabarani kwa traffic kutoa upepo kwenye matairi ya magari ya watu?

Najaribu kuweka picha inagoma, nitaiweka si mda.
my take: vitendo vya namna hii kwa mlinzi wa roho na mali za raia vinasababisha chuki kwa utawala uliopo madarakani...huu sio utu.

Attachments

 • image.jpg
  File size
  1.2 MB
  Views
  493
 • image.jpg
  File size
  1.2 MB
  Views
  457

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
13,157
2,000
Mkuu weka na picha ikiwezekana someni na namba za traffic haraka sana ili documentation iwe poa, kama na kapicha kwa traffic mnaweza kuchukua wakati akishawaruhusu. Yaani wanajiamlia tu hii nchi hovyo kabisa.
 
PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,894
1,225
....ni unyama huo, wanatumia weakness za raia kutoelewa utaratibu na wanazidi kuvunja sheria wanazotakiwa kuzisimamia; kawaida Dreva akiandikiwa Notification inabidi aende kulipia faini Ofisini ambapo ndo kuna muhasibu anayehusika na mambo ya Fedha, sasa hizi faini zinapokelewa barabarani na Askari maadamu amevaa Uniform nani ana zi-control!!!
 
Sangomwile

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
3,111
2,000
Ningekuwa mimi ni kuingia kwenye gari kimya kimya,baada ya hapo ni kilio kwa ndugu wa trafick.
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,777
2,000
Jioni hii mataa ya veta hapa sheli ya oil com traffic wamempiga notification dereva aliyekuwa na abiria kwenye gari ndogo private yenye namba za usajili T135 AMU toyota korola kwa kosa la kuzidisha abiria wakati gari hiyo ilikuwa na watu wazima watatu na watoto wadogo wawili.

Dereva huyo hakuwa na pesa cash ikabidi aanze kupiga simu kwa ndugu zake wamtumie pesa, traffic wakakasirika eti anawapotezea muda...unyama ulioje wakatoa upepo matairi yote ya mbele gari ili dereva asitoroke,,je huu ni uungwana?? Hii ndio sheria ya usalama barabarani kwa traffic kutoa upepo kwenye matairi ya magari ya watu?

Najaribu kuweka picha inagoma, nitaiweka si mda.

Hawa traffic wanatakiwa wapewe vyeo kabisaa. Kama wamemfanyia hivi mpaka T2015CCM ni sawa na kumuua nyani bila kumtazama usoni.
 
Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
3,426
2,000
Ndio maana leo wamenisimamisha nakijitochi chao mi nikachapa lapa. Wassengge sana. Najua sina makosa wangenipotezea muda tu.
 
T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
2,000
Hawa traffic wanatakiwa wapewe vyeo kabisaa. Kama wamemfanyia hivi mpaka T2015CCM ni sawa na kumuua nyani bila kumtazama usoni.
Unakosea mkuu tupendane... Mleta mada ameripoti unyama wa polisi kwa raia, hajasema kuwa ni yeye ndio ametendewa, au ulitaka awasifie? Hebu tuache siasa kwenye mambo ya msingi plz
 
SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,509
2,000
kushinda juani siku nzima nako kunachaNgia.big up mloona mbal na kuwajengea vbanda vya kupumzkia,ila kama wamefanya hivyo tusubir siku watavyorusu magar ya njia 4 yote kupita kwa pamoja ili yakutane kat kat,nna was bange inayokamatwaga kama uwa inateketezwa yote,usikute wamepuliza ushaid tena kibich cha a town,mkuu ebu angalia vzur katika mazingira ya kawaida ilo jambo aliwezekan! usikute hao trafik,dereva na watoto n wasanii wa bongo muv wanashut filamu
 
bysange

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
4,431
2,000
Trafiki wakibongo ni shida zaidi ya shida yenyewe ilivyo,pole uliyekutwa na mkasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom